Thursday, December 6, 2012

Yatima Wa Kituo cha Amani 'Wanapofuzu'!!

 Bi Erica Mwakalebela, Meneja wa Kituo cha Amani kinacholea watoto yatima wilayani Kilolo, akitoa nasaha zake leo mchana wakati akiwaaga baadhi ya vijana waliolelewa kituoni hapo, kusomeshwa na kuwakabidhi vifaa mbalimbali kulingana na taaluma zao.
 'Bonge la Mtu' Maregesi Gerson, ambaye leo hii amepewa 'ujiko' wa kuwa mgeni rasmi na kukabidhi zawadi mbalimbali kwa yatima wa Kituo cha Amani, wilayani Kilolo. Hapa alikuwa akitoa nasaha zake.
                   Zawadi mbalimbali ambazo vijana hao walikabidhiwa jana ili kwenda kuanzia ujasiriamali.
Walikwenda wadogo, sasa wamekuwa vijana. Kutoka Kushoto ni Claudia Mbugi (17), Waziri Kivamba (19) na Yusta Msangi (16) wakiwa na bahasha zao zenye vitita vya Shs 100,000 kila mmoja ili ziwasaidie wakaanze maisha.

Tiririka na habari kamili...www.kwanzajamii.com/?p=4574

Taarifa Kwa Umma: Usafiri Wa Tren Jijini Dar es Salaam

 Baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika tarehe 3 Desemba 2012 kauli yangu kuwa usafiri wa treni katika jiji la Dar es salaam kwamba kwa sasa unaingiza hasara ya wastani wa shilingi milioni 10 kwa siku tano, wanahabari mbalimbali kupitia simu na baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wametaka nitoe ufafanuzi kuhusu madai hayo.

Ieleweke kwamba nilitoa kauli hiyo wakati nikijibu swali la mwananchi kwenye mkutano wa hadhara tarehe 1 Desemba 2012 katika mtaa wa Saranga Jimboni Ubungo ambaye alihoji kuhusu ufanisi wa usafiri wa treni jijini Dar es salaam na hatua nyingine ambazo Serikali inapaswa kuchukua kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es salaam; hivyo katika hotuba yangu nilizungumza masuala mengi na kueleza mapendekezo niliyotoa kwa nyakati mbalimbali ya kuboresha mfumo mzima wa usafiri.

Nilieleza kwamba naunga mkono usafiri wa treni kuwepo jijini Dar es salaam na kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ilikuwa ni moja ya masuala niliyoahidi wananchi kwamba nitayafuatilia, na wakati huo wa kampeni wapo walionipinga ikiwemo kwa kuzungumza katika mikutano yao ya kampeni na hata katika radio.
Kazi ya mbunge ni kuwawakilisha wananchi katika kuishauri, kuisimamia serikali na kutunga sheria hivyo kwa msingi huo mara baada ya kuchaguliwa nilihoji bungeni kutaka hatua za haraka za kuanzishwa kwa usafiri huo na hatimaye Wizara ya Uchukuzi (wakati huo ikiwa chini ya Waziri Omar Nundu) mwaka 2011 ikajibu kuwa itatumia sehemu ya fedha kwenye bajeti kuanza matengenezo kwa ajili ya usafiri huo kuanza.

Kwa hiyo nilisisitiza kwenye mkutano wa hadhara usafiri huu kuanza mwaka huu 2012 ni matokeo ya kazi ambayo ilishaanza mwaka 2011, na nikawaeleza wananchi kwamba natambua mchango wa Waziri wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe katika kuongeza msukumo; hata hivyo niliwaeleza wananchi kwamba kama mbunge bado siridhiki na maandalizi yaliyofanyika na kwamba iwapo mapendekezo yangezingatiwa kwa wakati usafiri huo ungekuwa na mfumo na utaratibu bora kuliko ilivyo sasa.

DNA Yabaini Watoto Wengi Wa Kusingiziwa


ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.

Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.

Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Soma....  www.kwanzajamii.com/?p=4547

Magazeti ya leo Alhamisi ya 6th December 2012

Cheki Matokeo ya Mechi za UEFA Dec 5th 2012





Tuesday, December 4, 2012

CHAMPIONS LEAGUE


STORI KUHUSU USHINDI WA KILI STARS DEC 3 2012.

Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) itacheza nusu fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji 2012 Alhamisi (Desemba 6 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda.

Kilimanjaro Stars ambayo itacheza mechi hiyo na mshindi wa robo fainali ya Desemba 4 kati ya wenyeji Uganda na Ethiopia imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Rwanda Desemba 3 2012.

Mabao ya Amri Kiemba dakika ya 33 na John Bocco dakika ya 53 ndiyo yaliyoifanya Kilimanjaro Stars itinge nusu fainali na kuifungisha virago Rwanda (Amavubi) inayofundishwa na Milutin ‘Micho’ Sredojovic kutoka Serbia.

Vijana wa Kilimanjaro Stars wanaonolewa na Kim Poulsen walitawala pambano hilo, hasa kipindi cha kwanza kwa pasi fupi fupi. Kilimanjaro Stars imefungwa bao moja katika mechi nne ilizocheza tangu michuano hiyo ilipoanza Novemba 24 mwaka huu jijini Kampala.

Kilimanjaro Stars ambayo katika michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam mwaka jana iliishia hatua ya nusu fainali iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athuman Idd, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, John Bocco na Mrisho Ngasa.

Kwenye line nyingine mwandishi Shaffih Dauda ameandika kuhusu Michuano ya kombe la Uhai kuanza disemba 7 2012 ni kwamba michuano hiyo inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kumalizika Desemba 22 mwaka huu.

Wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.

Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo.

TAARIFA YA KILICHOENDELEA KUHUSU KESI YA MWIGIZAJI LULU DEC 3 2012.

Kesi ya mauaji ya marehemu Steven Kanumba inayomkabili movie star wa Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kutajwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku suala la umri wa mshitakiwa huyo likiendelea kuwekwa kiporo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO, Wakili wa Serikali KENNETH SEKWAO amesema upelelezi bado haujakamilika na kwa sasa ipo katika hatua ya kutajwa.

Mapema baada ya LULU kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA April mwaka huu, mawakili wanaomtetea waliwasilisha hoja ya kupinga umri wa mshitakiwa huyo na kutaka achukuliwe kama mkosaji mtoto kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18 hali iliyolazimu suala hilo kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamua kulirejesha jambo hilo kwenye mahakama ya Kisutu.

Pamoja na kurejeshwa kwa suala hilo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumekuwa na ukimya wa muda sasa, kesi ya LULU imeahirishwa mpaka Disemba 17 mwaka huu ambapo itakwenda kwaajili ya kutajwa.

Magazeti ya leo Jumanne ya 4th December 2012