Monday, April 1, 2013

WALIOFUKIWA NA KIFUSI KWENYE MGODI WA MORRUM JIJINI ARUSHA YAFIKIA 20

WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba  mchanga aina ya Moramu katika machimbo  yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.

Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .

Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.

Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.

Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.

Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.


KIJIJI CHA MISUKULE FEKI CHAFICHULIWA BAGAMOYO, WACHUNGAJI FEKI WADAIWA KUWATUMIA ILI KUWAHADAA WAUMINI WAO

 INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.

Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.

Uchunguzi  zaidi umebaini kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.

BREAKING NEWS: ZAIDI YA WATU 18 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORRUM HUKO ARUSHA

                                         Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.
                                                 Mwili wa mmojawapo wa marehemu.
                                                         Majeruhi aliyeokolewa.
Watu zaidi ya 18 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa Morrum huko Moshono jijini Arusha.

Kwa sasa wanajeshi wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari majeruhi mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu.

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka.

Magazeti ya leo Jumanne ya 2April 2013




JACK WOLPER AJIPANGA KUMUENZI KANUMBA

STAA wa  Bongo Movies, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa anatarajia kumuenzi marehemu kwa kuachia vipande vya filamu ya After Death ambayo ni mwendelezo wa filamu ambayo ilichezwa na marehemu Steven Kanumba, Uncle JJ.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Wolper alibainisha kuwa anatarajia kuonesha vipande vya filamu hiyo katika siku ya Kumbukumbu ya Kanumba itakayofanyika Aprili 7, mwaka huu katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar.

 “Ni filamu ambayo nimeiandaa katika mazingira maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba ambaye kila Mtanzania anatambua mchango wake kwenye sanaa,” alisema Wolper.

HIZI NDO PICHA ZA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI- ZANZIBAR

  Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..

LADY JAYDEE ADAI KUWA CLOUDS FM NI WANAFIKI....WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII

                                                                    Lady Jay Dee
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.

"Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira"

"MI NAJITUMA KWA BIDII..Q-CHIEF ANAKAA NA KUVUTA BANGI HALAFU ANADAI NATUMIA NYOTA YAKE....NAOMBA ANIKOME"...DIAMOND

Hii  ni  kauli  ya  msanii Diamond kuhusu Q chief: mi nafanya kazi, mazoezi na dancers, nahangaika kutafuta sare, kuandika nyimbo nzuri, wakati nafanya yote hayo we unakula unga, halafu unakuja kusema nasafiria nyota yako, nisafirie nyota ya mla unga? mi staki, staki, agombane na wakubwa wenzake kina dully mi aniache na wadogo wenzangu staki...?

MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR IMEFIKIA 21 MPAKA SASA

 Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21.

MAHAKAMA YASEMA Uchaguzi Kenya ulikuwa huru na wa haki

                                  Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.

Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.