Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mhariori wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, AbsalomKibanda, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 10, 2013 kwa mazungumzo. Kibanda alimtembelea Mhe. Makamu ili kumwelezea hali yake kiafya inavyoendelea baada ya matibabu. Picha na OMR
Monday, June 10, 2013
STAR TV YATANGAZA KUJITOA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES......TCRA YAGOMA NA KUDAI KUWA SHERIA HAIRUHUSU KUJITOA
BAADA ya Televisheni ya Star TV kutangaza kujitoa kurusha matangazo yao kupitia kingamuzi cha Star Times, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema sheria na leseni ya huduma, inazuia kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo, TCRA imesema inafanya uchunguzi na leo itakutana na uongozi wa Star TV na Star Times, kuzungumzia suala hilo ili hatua za udhibiti, zichukuliwe kuwezesha wananchi kupata haki ya msingi ya kupata matangazo ya kitaifa kupitia televisheni hiyo.
Star TV walitangaza kutoonekana kupitia Star Times siku chache zilizopita. Uchunguzi wetu umebaini kuwa, jana waliwasilisha barua ya hatua hiyo kwa kampuni ya Star Times kupitia mwanasheria wa kampuni yao.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy aliliambia HabariLeo jana kuwa na wao wamesikia taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari Lakini, alisema Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, haitoi fursa kwa watu wenye televisheni kujitoa ama kujiweka kwenye ving’amuzi watakavyo.

Subscribe to:
Posts (Atom)