Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa, amedai kuwa ikibainika kuwa CHADEMA ndio waliohusika katika kulipua bomu katika mkutano wao wa 15/06/2013 atakifuta.
Tendwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix cha East Africa Television akijibu swali la mtangazaji wa kipindi Adrian Stepp kuhusu hatua zitakazochukuliwa...
Alipoulizwa kama itathibitika kuwa CCM ndio walihusika kulipua bomu hilo amedai kuwa hawezi kukifuta kwakuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni kufanya mapinduzi ya kalamu.
Tuesday, June 25, 2013
MH. SUGU AMEACHIWA KWA DHAMANA BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) amekamatwa na Jeshi la Polisi Mjini Dodoma na kuachiwa kwa dhamana.
Mwandishi wetu akiwa Mjini Dodoma anasema kwamba Mbunge huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kutoka katika vikao vya Bunge.
Sugu alikamatwa na kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma na baada ya kuhojiwa aliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti kituoni hapo kesho asubuhi kwa mahojiano mengine.
Hata hivyo taarifa za awali za tukio la kukamatwa kwa Mbunge huyo wa Chama Cha Manedeleo na Demokrasia (Chadema) zinadai kwambwa inatokana na kosa la kutoa maneno ya uchochezi, matusi na dhihaka kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.

SUGU AKAMATWA KWA KUMTUSI WAZIRI MKUU
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi amekamatwa kwa kile kinachodaiwa ni uchochezi na kumkashifu Waziri Mkuu Mzengo Pinda. Hivi karibuni, Mh. Sugu alidai kuwa Tanzania haijawahi kuwa na waziri mkuu mpumbavu kama Mizengo pinda. Tunaendelea kufuatilia undani wa habari hii:
Jeshi la Polisi limemjibu Joyce Kiria Je Majibu haya ni sawa kwa mama Huyu?
Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi?
Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)

Mume wa Joyce Kiria Henry Kilewo akiwa ndani ya pingu na vijana wengine kwa tuhuma za ugaidi
Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi
yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani
Tabora kwa mara ya kwanza
Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
Kamanda Henry Kileo ndani ya pingu akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.

Inaumiza kiukweli msikia Joyce kiria alichoandika katika facebook yake
Jana baada ya kufanya hili zoezi na familia yangu namshukuru Mungu Wakili wetu Peter Kibatala alinipigia sim majira ya alasiri akanitaarifu ya kwamba Mume wangu yupo Tabora na yuko salama. isipokuwa amepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka mawili, UGAIDI na KUM'MWAGIA MTU TINDIKALI....Am speechless familia yangu tunaitaji maombi yenu sana kuliko mnavyofikiria
Subscribe to:
Posts (Atom)