Friday, May 24, 2013

TANZANIA,KENYA ZAVUTANA JUU YA VIJANA WALIOUWAWA NAROK

                                            Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas

MIILI  mitatu ya watanzania wa jamii ya Kisonjo waliouwawa katika eneo la Narok wilayani Kajiado nchini Kenya imeingia katika sura mpya mara baada ya Serikali ya Tanzania kushindwa kuirejesha nchini miili hiyo huku serikali ya Kenya ikidai kuwa hawakuwa watanzania

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa tayari mtu mmoja ambaye ni askari polisi anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi ingawaje alisema kwa sasa jina la askari huyo linahifadhiwa kwa ajili ya  upelelezi

Sabas alisema kuwa wanamshikilia askari huyo kwa kosa la upotevu wa silaha ambayo inasadikiwa kuwa ilitumika katika tukio uhalifu linalohusishwa na mauji ya vijana hao watatu wa Kitanzania nchini Kenya.

Kuhusu Marehemu hao, kamanda amesema kuwa Serikali ya Kenya kupitia Jeshi lake la polisi ndio wanajukumu la kurejesha  Miili yao hapa nchini .

Magazeti ya leo Ijumaa 24th May 2013




Flaviata Matata atoa wito kwa serikali kuhusu ajali ya MV Bukoba

Miss Universe Flaviana Matata akiwa na Mkurugenzi wa Compass communicayion, Maria Sarungi wakiwasha mshumaa kwenye kaburi la Marehemu mama yake mzazi aliyefariki katika ajali ya MV Bukoba mwaka 1996.

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameiomba serikali kutangaza Mei 21 ya kila mwaka kuwa siku maalum ya maombolezo ya wasiku maalum ya maombolezo ya wahanga wa MV Bukoba.
Ajali ya MV Bukoba ilitokea Mei 21 mwaka 1996 na kuua watu zaidi ya 1,000 na serikali kutangaza siku tatu za maombolezo ya kutokana na kuzama kwa meli hiyo iliyotokea kwenye Ziwa Victoria. Katika ajali hiyo, Flaviana alipoteza mama na kaka yake.

Flaviana ambaye kwa sasa anafanya shughuli za kuonyesha mitindo nchini Marekani na Uingereza, amekuwa mstari wa mbele kuadhimisha siku hiyo kwa kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation.

Akizungumza Kwa niaba ya Flaviana Matata Mkurugenzi wa Compass Communications Company Limited Maria Sarungi Tsehai alisema pamoja na ajali hiyo kuua watu wengi, lakini inasikitisha kuona jambo hilo kwa sasa limekuwa kama kumbukumbu kwa wahanga wa ajali hiyo tu na si vinginevyo.
Maria ambaye alisema hayo katika misa maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo iliyofanyika kwenye makabuli ya Igoma, Mwanza alisema kuwa wakati umefika sasa wa kutangaza siku ya kitaifa ya maombolezo na kwani ajali hiyo imeacha Watanzania wakiwa na huzuni kubwa.

Alisema kuwa wanashukuru sana kwa miaka hii miwili wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa Marine Service Company Limited na kampuni ya ndege ya Fastjet, ambapo mwaka jana walikabidhi vifaa vya kujiokolea (maboya) 500.

Azam marine waleta meli mpya 'Kilimanjaro iv'


                                                                         Kilimanjaro iv
KAMPUNI ya Azam Marine, inaleta boti mpya ya Kilimanjaro iv, ambayo inatarajiwa kuwasili nchini nchini, kuanzia mwishoni wa mwezi huu, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 700 na kutumia muda wa dakika 70 kwa safari moja ya kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Hii ni boti mpya kabisa katika muendelezo wa boti za Kilimanjaro, ambayo itakidhi mahitaji ya wasafiri wa eneo hili kwa kuwa inabeba sifa zote, ambazo ni Usalama, Kasi zaidi na Unadhifu. Kaa tayari kwa mzigo mpya kutoka Azam Marine.

Chanzo: Binzubeiry

HATIMAYE DR. SLAA AKUBALIWA KUOANA NA MPENZI WAKE...

HATIMAYE Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi( KWA  SASA  NI  MCHUMBA WA DR. SLAA) , Maimbo baada ya kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.

Hukumu hiyo ya rufaa ya  madai ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa leo na Hakimu Aniseth Wambura ambapo alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo kwasababu haina mantiki ya kisheria.

Hakimu Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili 2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon Mutakyamilwa  dhidi ya Maimbo ambapo mahakama hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na alikuwa akimtesa mkewe.

HALI BADO NI MBAYA MTWARA....WANAFUNZI WAWILI WAMETANDIKWA RISASI, MMOJA AMEFARIKI HAPOHAPO

 Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo..
 Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni. 
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.