Thursday, August 16, 2012

Redd’s Miss Ilala 2012 kuanikwa leo

Naye Mkurugenzi wa Machozi Entertainment, Gadner G Habash, alisema kwamba kutokana na vigezo vya warembo hao ni kutoka ndani ya vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa kambini wakijinoa kwa wiki mbili sasa katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, hapa Jijini.

Alisema Walimbwende hao wamekuwa akinolewa na Miss Ilala 2008,  Sylvia Mashuda, ambaye pia ni mshindi wa pili Miss Tanzania 2009, akimfuatia Nasreen Karim aliyetwaa taji.

Nayo Kamati ya maandalizi ya shindano la Redd’s Miss Ilala 2012, leo inatarajiwa kuwaanika warembo 15, watakaowania umalkia wa taji hilo, linaloshikiliwa na Miss Tanzania, Salha Israel.

Hadi kufikia sasa wadhamini waliothibitisha kudhamini kudhamini shindano hilo ni pamoja na City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Uhuru One, 88.4 Clouds FM na Redd’s Premium Cold.

Kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss Ilala 2012 kitarindima Septemba 7 mwaka huu, katika sehemu ya nje ya Nyumbani Lounge.

Magazeti Ya leo Alhamisi 16th August 2012

KAULI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAJINA YA WALIOWEKA FEDHA USWIS.

Kambi rasmi ya upinzani bungeni imesema italazimika kuweka wazi taarifa na majina ya watu wenye umiliki wa fedha katika benki nchini Uswis zinazofikia bilioni 315.5 kama serikali haitatoa hizo taarifa.

Waziri kivuli na msemaji mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Wizara ya fedha na uchumi Zitto Kabwe amesema hizo fedha zililipwa na makampuni ya utafutaji mafuta na gesi kwenye pwani ya mkoa wa Mtwara, kampuni ambazo zilipewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.

Nimemkariri Zitto akiongea bungeni kwamba “kambi rasmi ya upinzani bungeni imepata taarifa kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu zilizopita ni miongoni mwa wamiliki wa fedha hizi, sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi katika pwani ya mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006, kambi rasmi ya upinzani inaitaka serikali kutoa taarifa rasmi ya hatua gani ambayo imechukua mara baada ya kutolewa kwa taarifa kutoka benki ya taifa ya Uswis, tunaitaka serikali kuliambia taifa hatua itakazochukua kurejesha fedha hizi na nyingine zozote zilizofichwa ughaibuni”

Kuhusu ishu ya mjadala kuhusu kampuni ya BAE system ya Uingereza, Mh Zitto amesema “ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenchi ya rada na fedha ambayo Tanzania iliilipa benki ya Barclays, je chenchi ya rada ilikua na thamani yoyote kifedha? mjadala wa ununuzi wa rada hauwezi kuisha kwa kufurahia kurejesha chenchi tu, mjadala huu bado mbichi kabisa kwani tunataka ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona taifa lilipata hasara kiasi gani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wote walioliingizia taifa hasara”

Baada ya Zitto Kabwe kumaliza kuwasilisha, Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka aliomba mwongozo kwa spika na kusema “tuhuma hii ni kubwa sana nilitaka kuomba mwongozo wako kwamba nani abebe mzigo huu, ni Zitto ataje majina ya wanaohusika au serikali iwataje hao wanaohusika katika utoroshaji wa fedha hizo ambazo zimeenda ughaibuni ili kila mmoja abebe msalaba wake pale itakapothibitika kwamba fedha za wananchi wa Tanzania zimepelekwa nje ya nchi bila kufata taratibu za kisheria”

KITU ALICHOKIFANYA RAIS MUSEVEN KWA MGANDA ALIESHINDA OLYMPIC,

 Baada ya kurudi home, Maelfu ya waganda wamempokea Stephen Kiprotich mshindi wa medali ya dhahabu kwenye riadha ya Olympic 2012 ambapo ameifanya Uganda itangazwe mshindi wa medali hiyo baada ya miaka 40.

Kiprotich ambae ni askari magereza alieshinda kwenye mbio za wanaume jumapili iliyopita ndani ya Olypic 2012, amezawadiwa cheki ya dola za kimarekani elfu 80 ambazo zimetolewa na Rais Yoweri Museveni ambae pia amempandisha cheo mara tisa kwenye kazi yake ya uaskari Magereza.

Standard Media wameripoti kwamba mzigo ulikua mzito manake watu walipanga foleni kumpokea Stephen huko Entebbe akiwa amebebwa kwenye gari ambalo lilikua na plate namba iliyoandikwa UG GOLD.
                                                     Nyumba aliyokua akiishi Stephen.

Watu walikua wengi mpaka waliziba njia ambapo magari yaliyokua kwenye msafara yalikosa pa kupita wakati yakielekea ikulukumpeleka Stephen kunywa chai asubuhi na Rais Museveni.

Baada ya Kiprotich kupewa cheki yake ya dola elfu 80, alimuomba rais Museveni kuwajengea wazazi wake nyumba kaskazini mashariki mwa Uganda ambapo rais Museveni amekubali kujenga hiyo nyumba ya vyumba vitatu.

Kwenye line nyingine ni kwamba rais Museven ameahidi kwamba katika muda ujao, mwanamichezo yoyote wa Uganda atakaeshinda medali ya kimataifa, atakua analipwa shilingi shilingi milioni moja za Uganda kila mwezi.