Wednesday, August 15, 2012

HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kanuni ya 99(7), toleo la mwaka 2007 na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,napenda kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Wizara ya Fedha – Fungu 50 Wizara ya Fedha, Fungu 21 Hazina, Fungu 22 Deni la Taifa na Fungu 23 Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali. Vile vile Fungu 10 Tume ya Pamoja ya Fedha na Fungu 13 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

Mheshimiwa Spika, mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Fedha yanaomba kuidhinishiwa na Bunge lako tukufu jumla ya shilingi Bilioni 4,208 (trilioni 4.2) ili yaweze kutekeleza majukumu yake. Mafungu haya maombi yake ya Fedha ni sawa na asilimia 28 ya Bajeti nzima ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2012/13.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha ndiyo msimamizi mkuu wa Uchumi wa nchi ikitekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo, kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani na ya nje, kusimamia matumizi ya Serikali, kusimamia utendaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma, kusimamia manunuzi ya Serikali na Taasisi na Mashirika ya Umma,

kusimamia Deni la Taifa na dhamana za Serikali, kutafuta suluhisho na kusimamia mfumo wa kodi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kupambana na Fedha haramu. Sambamba na hayo ni kusimamia na kutekeleza mpango wa kupunguza umasikini nchini kupitia utekelezaji wa MKUKUTA II.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na mafungu yote yaliyo chini yake ndio moyo wa Serikali na hivyo ni lazima kuitazama Wizara hii kwa jicho kali na kutilia mashaka kila jambo ambalo inalifanya ili kuhakikisha kuwa moyo huu hausimami maana madhara yake ni kwa taifa zima na watu wake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia Waziri Kivuli wa Fedha inatekeleza wajibu huu kwa Uzalendo, Uadilifu na kwa misingi ya Uwajibikaji. Tumetekeleza wajibu huu na tunaendelea kuutekeleza bila kujali maneno na kuweka maslahi ya Taifa letu mbele ya kila kitu kingine. Maslahi ya Taifa ni zaidi ya vyama vya siasa, mahala tunapotoka au dini tunazoamini. Maslahi ya Taifa ni kwa ajili ya Watazania na hasa Watanzania milioni 30 (The Bottom 30M) ambao bado wanaishi katika ufukara mkubwa sana wakikosa huduma muhimu za jamii na wanaoishi vijijini ambapo hakuna umeme, barabara hazipitiki na wanahangaika kutwa kutafuta maji safi na salama. Maslahi ya Taifa sio faida ya wachache wenye kuishi mijini au wanasiasa wanaotafuta ushawishi kwa umma bila kujali matakwa ya Umma. Watanzania wanyonge wa vijijini wanajua maslahi yao ni nini. Wanajua kina nani wanapigania maslahi ya Wanyonge.

Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012

 Wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2012 wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa Bunge Jana mjini Dodoma.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa wosia kwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2012 bungeni jana mjini Dodoma. Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti , kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.Wanafunzi hao 10 wasichana na 10 wavulana wamepewa cheti na Waziri Mkuu, kopyuta ya pakato (laptop) na fedha taslimu shilingi laki mbili kwa kila mmoja.

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka wanafunzi wote nchini kuwa na nidhamu , kujituma na kufuata maelekezo vizuri ya walimu wao na kuepuka makundi mabaya ili kuweza kupata mafanikio katika masomo yao.

Aidha Waziri Mkuu Pinda amewaasa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita wa mwaka huu kutumia uhuru vizuri watakaoupata kwenye maisha ya vyuo vya elimu ya juu bila kurudi nyuma katika maendeleo ya masomo yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Pinda Bungeni mjini Dodoma kabla ya kuwatunuku vyeti vya kuwapongeza wanafunzi hao 19 kati 20 waliofanya vizuri katika mtihani huo,kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo mmoja wao, Jamal Juma yuko nje ya nchi.

Wanafunzi hao ambao wote walipata ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani huo, saba kati yao wanatoka katika shule ya wasichana ya Marian, watatu Mzumbe, wawili Fedha na wengine wawili Kibaha. Waliobakia mmoja mmoja anatoka Kilakala, Ufundi Ifunda, Tabora girls, Tabora boys, Minaki na Mpwapwa.

“Mmefanya vizuri. Mnastahili ! Hongereni Sana. Tunataka ufaulu wenu uwe mzuri zaidi kwa vile sasa ninyi mnakweda kujenga weledi. Mnakuwa wataalamu wa fani Fulani. Tumieni muda wenu kujifunza zaidi kutafuta maarifa zaidi na kuvumbua mambo makubwa zaidi yatakayowasaidia ninyi wenywe na jamii kwa ujumla kujiletea maendeleo,” alisema Waziri Mkuu Pinda.

Aliongeza kuwa ni vizuri utaratibu huo wa kuwatambua wanafunzi bora uwe endelevu na ikiwezekana wapatiwe fursa ya kuendelezwa katika vyuo vikuu vya kipekee nje ya nchi hususan kwenye fani zitakazojenga uwezo kwa taifa.

Waziri Mkuu alisema kati ya shule 10 ,ambazo wanafunzi hao wanatoka, wawili ni kutoka shule za kata, ambao ni Ester Marcel toka shule ya sekondari ya wasichana ya Olele Kilimanjaro na Brighton Lema toka shule ya sekondari ya Kitangiri, Mwanza.

“Napenda niwape pongezi za pekee wanafunzi hawa kwa jihudi kubwa walizozionesha. Kufaulu kwao kunadhihirisha kwamba shule hizi za kata tukiweka bidii kwa kuziwezesha zaidi zitafanya vizuri zaidi kama ilivyo katika shule nyingine,” alisisitiza .

Waziri Mkuu pia aliwataka walimu wote nchini kushirikiana na wazazi na serikali kwa pamoja kufundisha watoto kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kama wanafunzi hao waliotunukiwa vyeti hivyo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi hao watazawadiwa pakato (laptop) na sh. 200,000, pia kila shule iliyotoa mwanafunzi bora itazawadiwa sh. milioni moja katika hafla maalum itakayofanyika jioni.

Wanafunzi hao wanatoka katika mchepuo wa PCM ambao ni 16 na mmojammoja toka mchepuo wa PGM, CBA, ECA na HKL.

Naye Spika wa Bunge la Jamhuri, Anna Makinda aliwataka wanafunzi hao kuwa makini na makundi kwa kuyasilikiza huku wakitumia akili zao huku akitoa changamoto shule nyingine kujitahidi kufanya vizuri.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo


Mabaki ya Helikopta mbili za Uganda ambazo ziliripotiwa kutoweka siku ya Jumapili zimepatikana mashambani nchini kenya.
Kanali Cyrus Oguna ambae ni msemaji wa jeshi la Kenya amesema hatma ya watu 14 waliokuwemo ndani ya chombo hicho haijulikani.
Ndege hizo mbili zilikuwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikipelekwa nchini Somalia kuongezea nguvu kikosi cha umoja wa Afrika kilichoko huko.

Helikopta ya tatu ambayo pia ilikuwa katika msafari huo ilitua kwa ghafla katika eneo la mlima Kenya siku ya Jumapili.

Kanali Oguna amesema wote waliokuwa katika helikopta hiyo ya tatu waliokolewa.

Ni helikopta moja peke yake ndio faulu kutua vizuri na kuongeza mafuta katika mji wa Garissa ulioiko kaskzzini mwa Kenya.

Helikopta hizo nne ambazo zimetengezezwa Urusi ziliondoka siku ya Jumapili Uganda zikelekea Somalia kabla ya kukumbwa na mkasa huo.

Masalia ya helikopta hizo mbili ambazo awali ziliripotiwa kutoweka zilionekana juu ya mlima Kenya na maafisa wa Shirika la Wanyama pori, limeripoti gazeti la Daily Nation la Kenya.

Msemaji wa jeshi Kanali Oguna ameimbia BBC kwamba kikosi cha jeshi la Kenya linaelekea katika eneo hilo la Mlima Kenya , ambao ndio mlima wapili kwa urefu ,afrika.

Afisa huyo amefafanua kwamba moja ya helikopta hizo imeharibika kabisa ilhali ya pili imeharibika kiasi.

Helikpta hizo zilikuwa zinaelekea nchini Somalia kuongezea nguvu vikosi vya Umoja wa Afrika ambavyo vinajitayarisha kuvamia mji wa Kismayo na kuwafurusha wapiganaji wa Al Shabaab toka mji huo ambyo ndio ngome yao kuu.

 Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili

Magazeti ya Leo Jumatano 15th August 2012

Polisi: Tuko Tayari Kumlinda Ulimboka


HOFU YATANDA NYUMBANI KWAKE, MILANGO YATIWA KUFULI
JESHI la Polisi limesema liko tayari kumlinda kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka iwapo atahitaji ulinzi huo.Kauli hiyo imekuja siku mbili tangu daktari huyo wa magonjwa ya binadamu arejee nchini, huku usiri ukiwa umetawala taarifa zake kutokana na kutokuwapo kwa ndugu, jamaa au rafiki aliyekuwa tayari kusema chochote kumhusu.

“Nitachoweza kusema ni kwamba nashukuru mwanangu amerejea salama, lakini siwezi kusema chochote kuhusu mambo yanayomuhusu yeye,” alisema baba mzazi wa Dk Ulimboka, Mzee Mwaitenda.

Tofauti na juzi ambapo nyumbani kwake kulikuwa na watu kadhaa akiwamo Mweitenda, jana mageti yote ya nyumba hiyo iliyoko eneo la Kibangu, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, yalifungwa na hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Katikati ya hofu hiyo ya usalama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema Jeshi lake haliwezi kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka bila yeye mwenyewe kuomba.

"Kwanza walishaamua (madaktari) kuchagua ulinzi, sisi tufanyeje? Atakapoona kuna ulazima atatujulisha," alisema Kenyela na kuongeza;

"Hatuwezi kupeleka askari bila kuombwa. Ukipeleka halafu akasema hawahitaji, itakuwa embarrasing (fedheha) sana. Sisi tunajua amerudi na tunamtakia heri aendelee vizuri, apone na aungane na wenzake,"

Kamanda Kenyela alifafanua kuwa nyumbani kwa mtu ni eneo la faragha ambalo polisi hawawezi kwenda bila kuombwa na kufanya hivyo, ni kitu kisichokubalika.

"Mimi kama kamanda sijapokea ombi lolote kutoka kwa Ulimboka wala kusikia tishio lolote dhidi ya usalama wake. Akiona kuna haja ya kulindwa, aseme tutakwenda," alisema.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova alisema hawezi kuzungumzia ulinzi wa Dk Ulimboka kwa sababu tayari madaktari waliomba ulinzi UN.

UN wagoma kuongea
Msemaji wa Mwakilishi Mkazi wa UN nchini, Hoyce Temu hakutaka kueleza endapo taasisi hiyo ya kimataifa ilikubali ombi hilo au la akisema, suala la ulinzi halipaswi kuwekwa hadharani.

Alifafanua kuwa iwapo suala hilo litawekwa hadharani ni sawa na kuwapa nafasi maadui kujua namna mipango ya ulinzi ilivyopangwa.

"Suala la security (usalama) kama lilivyo si suala la kuwekwa wazi kwa public (umma)," alisema Temu.

Mwanzoni mwa Julai mwaka huu, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kikieleza kuwa hakina imani na polisi.

Chama hicho kiliomba ulinzi huo baada ya kuwapo na madai kwamba kuna kikundi cha watu kimekusudia kumuua Dk Ulimboka wakati akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa endapo UN ilikubali kutoa ulinzi kwa Dk Ulimboka alijibu "haikuwa lazima kwa UN kutujibu."

Aliongeza, "Sisi tuliwasilisha barua, tukitoa malalamiko yetu, namna gani watafanya kazi ya ulinzi siyo lazima watujibu, wao wanataratibu zao za kufanya kazi."

Daktari wake anena

Profesa Joseph Kahamba alisema hajaonana na Dk Ulimboka tangu arejee nchini Jumapili ila anaamini anaendelea vizuri.Alipoulizwa imekuaje hajaonana na mgonjwa wake wakati yeye ndiye aliyemwandikia rufaa ya kutibiwa nje ya nchi alisema, "Siyo ajabu".

Alisema siyo lazima daktari aliyemwandikia mgonjwa rufaa ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kuwasiliana naye anaporudi kwa kuwa hili linategemea hali aliyonayo mgonjwa husika.

"Hapa kuna mambo mawili; kuna kurudi akitakiwa tena kulazwa na kurudi kwa maana ya kupona," alieleza Profesa Kahamba baada ya kuulizwa kama ni lazima daktari aliyetoa rufaa awasiliane na mgonjwa baada ya kurudi kwenye matibabu.

Aliendelea "Angerudi (Dk Ulimboka) kwa state (hali) ya kulazwa, lazima angefikia kwangu nimwone, lakini kama amepona, anaweza kwenda kusalimia ndugu na kunywa bia kwanza halafu baada ya siku, wiki au mwezi akaja nikaonana naye."

Profesa Kahamba alieleza "Tangu Ulimboka arudi sijaonana naye zaidi ya kufanya mawasiliano na wenzake kwenye simu ila amepona kwa kuwa hajarudi kwangu."

MAT: Mwacheni apumzike

MAT kimewataka waandishi wa habari kutoendelea kumfuatilia Dk Ulimboka ambaye ni kiongozi wa jumuiya hiyo kwa kile walichoeeleza anatakiwa kupata fursa ya kupumzika.Makamu wa Rais wa MAT, Dk Prinus Saidia alipotakiwa kueleza ni lini atajitokeza hadharani kufuta kiu ya Watanzania kuhusu kilichomsibu, alisema:“Yeye mwenyewe ametuomba tumwache apumuzike kwa muda na sisi tumeona hili ni sahihi. Tumemwacha kwanza hadi hapo atakapotuambia kuwa yuko tayari kuungana nasi.”

Dk Saidia alisema madaktari kwa umoja wao wamefurahi kuona Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima na kwamba hilo ndilo jambo bora zaidi kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

“Tunamshukuru Mungu Dk Ulimboka amerudi akiwa mzima, hili ndilo lilikuwa la msingi. Hata hivyo, suala liko wazi mgogoro baina yetu (madaktari) na Serikali haujafikia mwafaka. Inatakiwa pande zote zikae na kukubaliana na si upande mmoja kutumia nguvu,” alisema Dk Saidia.

Katika hatua nyingine habari kutoka ndani ya MAT zinasema viongozi wake wamekuwa wakifanya vikao vya ndani tangu juzi kujadili mambo mbalimbali likiwamo la kuandaa mazingira yatakayomwezesha Dk Ulimboka kuzungumza hadharani.

“Kuna vikao vinaendelea tangu jana (juzi), viongozi wanakutana kujadili mambo mbalimbali likiwamo namna Dk Ulimboka atakavyopata fursa ya kuzungumza,” kilisema chanzo hicho.

Dk Ulimboka alitekwa, kuteswa na kutupwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia Juni 26 mwaka huu.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz