Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati
Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo
wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais),
Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu
kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika
sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la
Singida jana Januari 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya
kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu
Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na kiongozi wa kanisa la KKKT
nchini Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya
kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi hiyo huku Askofu mpya wa
KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia katika sherehe
ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida jana
Januari 6, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa
Kanisa la KKKT baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo
katika kanisa la KKKT la Singida jana Januari 6, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013
PICHA NA IKULU
Monday, January 7, 2013
RAIS JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU NNE KATIKA MKOA WA TABORA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa
Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili
mkoani humo jana kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe Fatma Mwassa wakati alipokuwa akisoma ripoti hiyo mbele ya Rais mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.
(PICHA NA IKULU)

MIRAJI MRISHO KIKWETE ATEULIWA KUWA “MAKAMU WA RAIS” WA IBF/AFRIKA MAENDELEO YA VIJANA
+Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji unaanza January mwaka mpya 2013.
Katika kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
Aliendelea kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha, kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
Aidha, Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
Katika mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.
Lengo kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.
Katika mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203 duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika miradi mbalimbali.
Uteuzi wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati muafaka.
Miraji ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana mchango mkubwa sana katima kuendeleza vijana nchini Tanzania.
Rais Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi kitefu.
Miraji Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.

Subscribe to:
Posts (Atom)