Wednesday, November 28, 2012

"NIKIACHIKA TENA NITAOLEWA UARABUNI...." JACK WOLPE


PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa uarabuni.

Wolper amesema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka  tena kuwa na mpenzi wa  Kibongo.

“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’.

JENEZA LILOBEBA MWILI WA MAREHEMU SHARO MILIONEA.

                           Hili ndilo jeneza lililobeba mwili wa marehemu sharo milionea.
                                     Nyumba ya Milele ya ndugu yetu Sharo Milionea Apumzike kwa Amani
Marehemu Sharo milionea Akiondolewa Hospitalini Kuelekea Katika Nyumba yake Ya milele

Hatimae Baba Mdogo wa Mwigizaji wa Filamu Marehemu John Maganga Aeleza Mkasa Mzima toka Alipoanza kuumwa Mpaka kifo chake

Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.

Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.

Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.

Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.

Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.

Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.

Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea.

Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.

Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena, amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake.Alisema baba mdogo wa muigizaji Stephano.

Abiria wa treni Watoa mpya ya kufungia mwaka, wageuzanalo kwaajili ya kuwahi siti.

 Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe iwasili stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha Majumbani Kwao. Baadhi ya Abiria wakiwa wamewahi kwaajili ya Kupanga foleni ili waweze kupata siti huku wengine wakichuchumaa kutokana na kulisubiri kwa muda
 Abiria Wakiteremka katika treni linalofanya safari zake ndani ya Jiji la Dar mara lilipowasili Katika Kituo cha Stesheni karibu na central polisi tayari kwa safari ya kurudi tena Ubungo
 Baadhi ya Abiria waliogeuza na treni hilo wakiwa wamepandia Kituo cha Kamata Ili kuwahi Siti ambapo walipelekea sintofahamu kwa baadhi ya abiria waliokuwa kituoni hapo na kutaka kupanda kwenye hilo behewa kukuta likiwa tayari limeshajaa kutoka na abiria kugeuza na treni hilo wakati utaratibu huwa haurusiwi na ikifika mwisho abiria wote wanatakiwa kushuka
 Mmoja wa Abiria aliyegeuza na treni hilo ambapo walipandia Kamata kwa lengo la kuwahi kiti akibishana na mmoja katika ya abiria ambao walikua kwenye foleni muda mrefu wakisubiria treni hilo kufika ili waweze kuingia ndani na kupata siti ambapo alikuta behewa hilo likiwa limeshajaa na kuanza kubishana huku abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo wakitaka abiria waliogeuza na treni hilo kushuka
 Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa jina la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika kituo cha Stesheni tayari kwa kurudi nalo ubungo huku baadhi ya behewa kuwa limeshajaa kabla hata halijafika kituoni hapo kutokana na abiria kugeuza nalo kwa lengo la kuwahi siti. Behewa ambalo lilikuja likiwa limeshajaa ni behewa lenye namba 3644 ambalo abiria wake walikua wamepandia njiani kwa nia ya kugeuza nalo ili waweze kupata siti.
 Abiria wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya treni la mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini jana

Katika hali isiyo ya kawaida jana kwenye majira ya Saa 11: 20 Jioni katika kituo cha Treni kilichopo stesheni mkabala na Kituo Cha Polisi Cha Cetral kuliibuka Jambo la kushangaza wakati abiria wanaosubiria treni inayofanya kazi zake ndani ya jiji la dar kuona behewa moja likiwa limeshajaha tayari kutokana na abiria kupandia njiani na kugeuza nalo kwa lengo la kuwahi siti na kupelekea abiria waliowahi kituoni hapo na  kupanga foleni kwaajili ya kuwahi siti kuambulia patupu.

Abiria waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika pale ambapo walikuta behewa hilo limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika kwenye kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi . Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakua kitu ambacho utaratibu hauruhusu. Utaratibu uliopo ni kwamba hata kama abiria amepandia katikati anatakiwa kuteremka pindi treni hilo linapofika mwisho wa kituo ndipo akate tiketi kwaajili ya kupanda tena na kurudi nalo lakini hali imekuwa tofauti hapo jana baada ya abiria hao kutokushuka na tiketi kukatiwa ndani na kupelekea abiria waliokuwa wakisubiri treni hilo kusubiri kwa muda mrefu.

Lukaza blog imeweza kunakili sauti za abiria ambao waliokuwa wakilalamika juu ya utaratibu huo uliofanywa na wafanyakazi ambao sio waaminifu na kupelekea usumbufu kwa abiria ambao wamewahi kupanga foleni.

TENGA, WIZARA WATETA KUZUIWA AKAUNTI YA TFF

 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lina imani kuwa mazungumzo kati yake, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yatamaliza tatizo la kushikiliwa akaunti ya TFF kutokana na malipo ya kodi ya mishahara ya makocha wa kigeni.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga alizungumza na waandishi wa habari jana juu ya uamuzi wa TRA kushikilia akaunti ya TFF ikiielekeza Benki ya NMB kukata sh. 157,407,968 ikiwa ni malipo ya Kodi ya Mapato ya Mshahara wa Mfanyakazi (P.A.Y.E) ya makocha Marcio Maximo na wasaidizi wake.

Katika mzozo huo wa muda mrefu, TFF imejitetea kuwa haiwezi kulipa kodi hiyo kwa kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ndiyo mlipaji wa mishahara ya makocha hao, ikiwa ni ahadi ya Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete ya kulipia makocha wa michezo tofauti, ukiwemo mpira wa miguu.

“Hili ni suala nyeti ambalo linahitaji kumalizwa kwa mazungumzo baina ya pande zote. Ninataka kuwahakikishia kuwa suala hili linazungumzwa na tayari nimeshafanya mazungumzo na maofisa wa Wizara na tumekubaliana kukutana na pande zote  wakati wowote; iwe leo jioni au kesho.

“Ni matumaini yangu kuwa suala hili litakwisha na jana nimetoka Kampala (Uganda kwenye Kombe la Chalenji) moja kwa moja na kwenda kuzungumza na viongozi wa Wizara na wamekubali kwamba tuongee pande zote kulimaliza suala hili.

Precision Air katika Facebook na Twitter

 Baada ya shirika la ndege la Precision Air kununua ndege yao mpya aina ya ATR 42-600 na kuwa shirika la kwanza Africa na duniani kumiliki na kutumia ndege aina hiyo, sasa inawapa fursa mashabiki wake katika mtandao wa facebook na twitter kuwa wa kwanza

kuruka na ndege hiyo.
 Ndege hiyo hiyo ya kisasa ambayo uzinduzi wake rasmi umepangwa kufanywa tarehe 5 ya mwezi December, ina siti 50 na inatarajiwa kufanya safari zake kati ya Dar es salaam na Kilimanjaro.

Katika uzinduzi huo Precision Air itatoa zawadi kwa washindi watatu (3) kutoka katika ukurasa wao wa facebook. Ili kushinda itakubidi utembelee ukura wao wa facebook (www.facebook.com/Precisionairtz), kwanza bonyeza LIKE kama bado hujajiunga na ukurasa huo halafu SHARE picha ya ndege hiyo iliowekwa kwenye ukurasa huo kisha waambie marafiki zako waLIKE na kuCOMMENT kwenye picha yako ulioSHARE, Watu watatu (3) watakaoongoza kwa kua na LIKEs na COMMENTs nyingi kwenye picha yao walioShare moja kwa moja kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Precision Air watakua washindi.

                                   Hi ndio picha ya shindano unayotakiwa kuSHARE ili kushinde
[ ANGALIZO : Unatakiwa kushare picha moja kwa moja kutoka kwenye facebook page ya Precision Air]

Mshindi wa kwanza kwa kua na LIKEs na COMMENTs nyingi zaidi atashinda tiket ya buuure kwenda kokote ambako ndege za Precision Air zinakwenda, pia atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600  na mwisho atahudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.

Mshindi wa pili atapata fursa ya kuruka na ndege mpya ATR 42-600  na pia atahudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya. Na mshindi wa tatu yeye atapata fursa ya kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa ndege hi mpya.
Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa zao za;

facebook [www.facebook.com/precisionairTz],
Twitter [www.twitter.com/PrecisionAirTz]

na YouTube [www.youtube.com/PrecisionAirTz].

Ndege za fastjet zazinduliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, yakamilisha makubaliano ya ubia na Swissport

Shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu Afrika, fastjet, leo limeizundua ndege yake ya kwanza ikiwa nachapa yake kamili, siku mbili tu kabla ya kuanza safari za anga Tanzania. Kwenye hafla iliyofanyikakwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kamabarage (JKIA),Dar es Salaam, maafisa wa serikali, watendaji wa fastjet na wataalamu wa safari za anga walishuhudia ndege aina ya Airbus A319 ikipaa kwenye anga ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Kuanzia Alhamisi, 29 Novemba, fastjet itafanya safari mbili kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo – Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza, zote zikiwa ni safari zenye wasafiri wengi wa ndani. Tiketi zilianza kuuzwa wiki mbili zilizopita na fastjet imeshuhudia mahitaji makubwa, zaidi kuliko matarajio ya awali. Mpaka sasa idadi ya tiketi zilizonunuliwa ni sawa na safari 60 za ndege iliyojaa, na mauzo yanaendelea kwa safari za mwakani. Nauli zitakuwa za wastani wa dollar $80, lakini zinaanzia bei ya chni kabisa ya $20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali kwa wateja watakowahi kununua tiketi.

Akizungumza mjini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winter, alisema:

“Leo ni siku ya kusisimua sana, na siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika, shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama na ubora.”

Akizungumzia uzinduzi wa leo, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Airbus – Wateja, alisema:

Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”

Magazeti ya leo Jumatano 28th November 2012

Hii ndilo gari la sharo milionea lililvyoharibika katika Ajali iliyosababisha kifo chake.



                          Wakazi wa Tanga wakiangalia gari alilopata nalo ajali sharo Milionea

 Mbuge wa jimbo la Muheza Hebert Mtangi akiwasili nje ya jengo la chumba cha Kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Muheza kwa ajili ya kushuhudia Mwili wa Msanii Sharo Milionea aliyekufa kwa ajali akitokea Dar es Salaam kwenda lusanga Muheza mkoani tanga. Ajali hiyo imetokea Katika kijiji cha Songa Kibaoni.
Wakazi wa Wilaya ya Muheza na maeneo mengine wakiwa wamefurika nje ya chumba cha Maiti cha Hospitali Teule Muheza wakisubirikushuhudia Mwili wa sharo Milionea Aliyefariki kwa ajali ya gari

Airtel Wamlilia Sharo Milionea....