Saturday, March 30, 2013

Kwaya ya Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali Rwanda kutua Dar es salaam


KUNDI la muziki wa kiroho la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda linatarajia kutua Dar es Salaam leo (Jumamosi) kwa ajili ya Tamasha la Pasaka kesho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa kundi hilo pamoja na mambo mengine litazindua albamu yao iitwayo Kaeni Macho katika tamasha hilo litakalofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tayari mambo yetu yanaenda vizuri na Kwetu Pazuri watawasili Jumamosi wakiwa wamepania kufanya mambo makubwa kwenye tamasha letu,” alisema Msama na kuzitaja nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo kuwa ni Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.

Alisema kundi hilo limefurahi sana kuja hapa Tanzania na ndiyo sababu wakaipa heshima Tanzania kuzindua albamu yao wakiwa na imani mashabiki wataipenda na kwamba hivi sasa wanatamba na albamu ya Mtegemee Yesu na wamemhakikishia watang’arisha tamasha la mwaka huu.

Alibamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegemee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda.

Licha ya kundi hilo, wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone,  Bonny Mwaitege, Upendo Kilahiro, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam kesho na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Magazeti ya leo Jumamosi ya 30th March 2013




RAIS KIKWETE ALIPOWASILI KWENYE ENEO AMBALO GOROFA LILIPOPOROMOKA JANA DAR ES SALAAM





Mkuu wa mkoa Said Meck Sadick akiwa na Rais Kikwete na Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es salaam Suleiman Kova, picha zote kutoka kwa mwandishi wa habari Mtoki ambae pia ni mmiliki wa mrokim.blogspot.com

Watu 40 wahofiwa kufukiwa baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Dar

 Watu zaidi ya 40 wanahofiwa kufukiwa na kifusi baada ya jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa kuporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana asubuhi.

Jengo lililoporomoka

Kuporomoka kwa ghorofa hilo lililokuwa katika Mtaa wa Indira Gandhi, kulizua huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la tukio kutaka kufahamu nini kimetokea.

Shughuli mbalimbali katikati ya jiji hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano, 13 kuokolewa huku zaidi ya watu 40 wakisadikiwa kufukiwa na kifusi cha udongo wa jengo hilo.

MUUAJI WA PADRE MUSHI - ZANZIBAR AMEKAMATWA LEO

                                                Father Evalist Mushi enzi za uhai wake
 Mtu anaesadikiwa kuwa ndie muuaji wa aliyekuwa Padre Evalist Mushi wa kanisa katoliki, visiwani zanzibar, amekamatwa leo alasili maeneo ya kariakoo, zanzibar.

Jeshi la polisi limethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, na kwenda nae kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Padri Mushi aliuwawa kwa kupigwa risasi mwezi uliopitwa wakati akiwa kwenye gari lake kuelekea kanisani kwenye ibada ya jumapili.

"SIPO TAYARI KUJIUZULU KWA KUOGOPA MAJUNGU YA VYAMA VYA UPINZANI".....NAIBU WAZIRI WA ELIMU

Victoria fm ya mjini Mwanza jana asubuhi kipindi cha matukio wameripoti kuwa wamefanya mahojiano na naibu waziri wa elimu Bw.Philip Mulugo kuhusu tuhuma zinazomkabili ambapo amesema hawezi kujiuzulu kwa kuogopa majungu ya vyama vya upinzani wanaopika uongo juu yake ili kuwika kisiasa.

Mulugo amekanusha madai yote yaliyoandikwa na gazeti la Mwananchi na kudai kuwa kama kuna mwenye wasiwasi na elimu yake aende akamuoneshe vyeti vyake vya elimu ya sekondari hadi vya taaluma na chuo alichosoma