Thursday, April 11, 2013

Ajali Yauwa Waandishi wa Habari, Ofisa Uhamiaji Handeni

                         Marehemu, Hussein Semdoe wa Mwandishi Gazeti la Mwananchi, Handeni.

WAANDISHI wa habari wawili pamoja na Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Handeni wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo majira ya saa nne asubuhi nje kidogo ya Mji wa Handeni. Waliofariki dunia ni Hussein Semdoe wa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Hamis Bwanga wa Radio Uhuru na Abood pamoja na Mariam Hassan ambaye ni Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Handeni.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifo vya marehemu hao. Akizungumza na www.thehabari.com mchana huu, Mkuu wa Wilaya hiyo alisema ajali hiyo imetokea wakiwa kwenye msafara kuelekea Ndolwa kupanda miti.

Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo, Muhingo alisema gari lililopata ajali ni la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, STJ 4673 ambalo ndilo lililokuwa likitumiwa na Ofisa Uhamiaji, Hassan pamoja na wanahabari hao.

JK mourns Thatcher

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete signs a condolence book at British High Commissioner's Office in Dar es Salaam following the death of former British Prime Minister Margareth Thatcher who died of stroke on Monday at the age of 87

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATANGAZA KUWASHITAKI WANAODAI KUWA "AMEGUSHI VYETI"

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema atawafikisha mahakamani watu wanaodai kuwa ameghushi vyeti vya elimu ya sekondari.  Mulugo alisema amechoshwa na kashfa hizo zinazosambazwa na baadhi ya watu atawafikisha mahakamani endapo wataendelea kumdhalilisha.

Mulugo alitoa kauli hiyo alipofungua mkutano wa mwaka wa Umoja wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania (TAMONGSCO0) jijini Mbeya.

“Wanasema eti nimeghushi vyeti, mara ooh sijui natumia jina la mtu. Nimechoshwa na maneno haya… ni kweli nimerudia darasa kama walivyorudia watu wengine, kwa nini iwe tatizo kwangu. Hata hapa tulipo wapo wengi tu waliorudia darasa.

“Kama kweli ningekuwa nimeghushi vyeti hivi leo ningekuwa naibu waziri wa elimu? Sasa nimechoshwa, nitawachukulia hatua watu hawa, siwezi kusema ni lini nitafanya hivyo ila nitakapoamua nitaanza,”alisema.

WAKATI RAGE WA SIMBA AKIJIANDAA KUIPELEKA MAHAKAMANI AZAM FC, CLUB HIYO IMEMJIBU NA KUMWAMBIA KUWA ITAMPATIA HADI NAULI YA KUMFIKISHA MAHAKAMANI

 KLABU ya Azam FC imetoa 'Go Ahead' kwa Simba kwenda mahakamani kwa madai ya fidia ya kuchafuliwa.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage alikaririwa mjini Dodoma alipokwenda kuhudhuria vikao vya bunge kuwa klabu yake inaandaa barua ya kuidai fidia ya Sh1.5 Bilioni.

Ni kutokana na klabu ya Azam kuwafungia wachezaji wanne kwa tuhuma za kupokea rushwa ambayo ni  Sh7 milioni ili wapange matokeo wakati wa mechi ya Simba na Azam FC Oktoba 26, mwaka jana ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo.

Magazeti ya leo Alhamis ya 11th April 2013




"KILA MTU ANAHAKI YA KUCHINJA NA KULA CHOCHOTE HATA CHURA"...HII NI KAULI MPYA YA RAIS MWINYI

RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amerejea kauli yake kuhusu mgogoro wa udini akisema kila mtu ana haki ya kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu asivunje sheria za nchi.

Mwinyi alisema anashangaa kuona watu wakigombania kitu kidogo kama kuchinja ilihali Tanzania ina utamaduni wa amani siku zote na kwamba kila mtu ana imani yake ya dini anayoiamini.
Kiongozi huyo mstaafu alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano juu ya utamaduni wa Kiislamu Afrika Mashariki ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji.

“Imani ni nafsi ya mtu na haitakiwi kumlazimisha kula nyama iliyochinjwa na mwenzie. Na kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu basi usile chinja yako, kula hata ukitaka kula chura, mjusi, konokono, kula utakacho ruksa ilimradi tu usiingie katika jinai,” alisema.