Friday, March 22, 2013

WAKILI MAWALA NYAGA AJIUA KWA KUJITUPA TOKA JUU YA GHOROF

Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la Mwananchi, ARUSHA-- Giza limeukumba Mkoa wa Arusha baada ya kutokea vifo vya ghafla vya watu maarufu. Jana Wakili Nyaga Mawalla alifariki baada ya kujirusha kutoka ghorofani akiwa jijini Nairobi, Kenya alikokwenda kwa matibabu.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Nyaga alikufa baada ya kujirusha kutoka katika jengo la ghorofa ya hospitali aliyokuwa akitibiwa jijini Nairobi usiku wa kuamkia jana.

Mfanyakazi wa Kampuni ya Mawalla Advocate, John Minja aliliambia gazeti hili kuwa mwili wa marehemu ulitarajiwa kurejeshwa nchini jana.

MAANDAMANO YA CHADEMA KESHO: MBOWE ADAI YAKO PALE PALE NA WATAANDAMANA MBELE YA RAIS WA CHINA

 LICHA ya serikali kuyapiga marufuku maandamano yaliyoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuishinikiza kumwajibisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Naibu wake wajiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne 2012, chama hicho kimesema yapo pale pale.
Chama hicho kimewaomba wananchi wote waliochoshwa na kufelishwa kwa watoto wao, kunyimwa elimu bora wajitokeze kuandamana kwa nguvu zote, na wanafunzi wote waliofeli pia wajitokeze kudai elimu bora kwani ni haki yao.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana na kutoa msimamo huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema “wananchi wajitokeze kwa wingi ili kilio chao kisikike duniani kote.”

Alisisitiza kuwa maandamano hayo yatafanyika mbele ya ugeni wa Rais wa China, Xi Jinping ili kufikisha kilio hicho na kamwe haikubaliani na sababu ya serikali kuyazuia kwa sababu ya ugeni huo.

RIPOTI YA POLISI: MADAI YA KULAWITIWA KWA WANAFUNZI WA IFM SI YA KWELI

 Kamati iliyoundwa kuchunguza vitendo vya udhalilishaji na kuporwa vitu vyao  wanavyofanyiwa wanafunzi  wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaoishi  katika hosteli zilizopo Kigamboni Manispaa ya Temeke imebaini hakuna wanafunzi waliofanyiwa vitendo hivyo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Polisi jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova baada ya kuwahutubia wanafunzi hao katika Viwanja vya Machava, ilijumuisha wanafunzi wanne wa IFM na wakuu wa upelelezi kutoka kanda hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Englebert Kiondo, alisema kamati hiyo ilichunguza kwa kina madai hayo ya wanafunzi, lakini hakuna na hata moja walilobaini kuwa na ukweli .

JACK CHUZI WA BONGO MOVIE ABADILI DINI NA KUOLEWA....


 
 Katika Hali ya Kushtusha na Kufuraisha....Staa wa Bongo Movie Jack Pentezel amewashtusha wengi baada ya Kuamua kubadili dini kuwa Muislamu kisha kuolewa na Mpenzi wake wa Muda Gadner Dibibi....

wadau wengi na wapenzi wa Bongo Movie wamekuwa wakihoji juu ya Ndoa Hiyo iliofungwa kisiri sana na kwa haraka,Je Ndoa Hiyo Itadumu? Je ni kweli wamehamua kukaa kwenye Maadili ya Ndoa..? au Ni kama Mchezo wa Mjini kubadilishana Dini na kuoana mwishowe ni kuachana....Tusubiri Tuone.....

Mpekuzi  inapenda kumtakia Jack Pentezel na Mumewe Gadner Dibibi Baraka Tele,Amani na Upendo utawale kwenye Maisha yao ya Ndoa..

" MIMI NI MTI WENYE MATUNDA MILELE....SIOGOPI KUPIGWA MAWE"... HUU NI UJUMBE WA DIAMOND

MSANII wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinam ameendelea kujinadi kupitia mitandao ya kijamiii huku akiteka hisia za mashabiki wake kwa kutuma baadhi ya picha zinazomuonyesha akiwa jukwaani akifanya 'makamuzi' pamoja na kutuma ujumbe wa kujipongeza kwa kazi anayoifanya

Kupitia mtandao wake wa 'Instagram' msanii huyo alituma ujumbe uliosomeka hivi "Mimi ni mti wenye matunda milele siogopi kupigwa mawe"

Ujumbe huo ulionekana kuteka baadhi ya mashabiki wake huku wengine wakituma ujumbe za kumpongeza kwa kuwa na imani hiyo huku akionyesha kutoteteleka kwa jambo lolote linalomkabili ambalo linaonyesha kutaka kumdondosha kimuziki

Maneno ya ujumbe huo pia umeonekana kutumiwa katika nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Muziki gani' ambayo wameshirikiana na msanii Ney wa Mitego

RIPOTI YA GAZETI LA IJUMAA KUHUSU WABUNGE KUTEMBEA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM )

 MITANDAO mingi ya kijamii na kurasa binafsi za mawasiliano zinazopatikana ndani ya simu za viganjani kama Instagram, WhatsApp na BBM (Blackberry Messenger) zinazomilikiwa na baadhi ya wasichana wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) zimejaa mambo ya ngono na kashfa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Unyemeleaji taarifa uliofanywa na Ijumaa kwa muda mrefu kwenye huduma hizo za mawasiliano ya kisasa  umebaini wanafunzi wa kike wamewabatiza jina la ‘mabuzi yao’ baadhi ya wabunge.

Bila kupepesa mitandao hiyo imekuwa pia ikitumiwa na wasichana hao kuuza miili yao huku ufahari kama si ujanja ukiwa ni mtu kujipatia bwana mwenye cheo cha ubunge ambaye anaaminika waleti yake haikaukiwi fedha kutokana na posho za vikao na utumishi wa umma.

MAHAKAMA KUU YAITISHA MAFAILI YA KESI YA LWAKATARE

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwasilishe majalada ya kesi ya ugaidi inayomuhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake katika kesi hiyo, Ludovick Joseph.

Hati ya kuitisha majalada hayo ilitolewa jana alasiri na Msajili wa Mahakama Kuu, baada ya mawakili wanaomtetea Lwakatare kuwasilisha maombi ya marejeo ya mwenendo wa kesi hiyo, iliyofunguliwa katika Mahakama ya Kisutu.

"NAWASHANGAA WANAOPOTEZA MUDA KUYAFUATILIA MAISHA YANGU"....WEMA SEPETU

Msanii anayetafuta mafanikio kwa kasi, Wema  Sepetu amesema kuwa haoni sababu ya watu kutishiana maisha hasa kwa kipindi hiki ambacho maisha yapo juu.

Wema alisema hayo kufuatia hivi karibuni  kutishiwa maisha na watu asiowafahamu na  kulazimika kuongeza ulinzi nyumbani kwake na  kila anapokuwa anatoka.

Alisema maisha ni magumu na kila mmoja  anatakiwa afanye kazi kwa bidii ili kufikia  malengo, badala yake watu wanaanza kutishiana  maisha.

"Nawashangaa watu wanaoendelea kuwafuatafuata  wengine wanapata wapi ujasiri huo na hali ya  maisha ilivyo ngumu na kuhitaji muda mwingi wa  kufanya kazi ili kujikwamua,"alishangaa Wema.

Aidha, aliongeza kuwa hana adui wala mtu ambaye  anamdai au kitu kama hicho hivyo watu  wanaomtumia mesaji za vitisho anahisi wana chuki  binafsi na si kingine.