Monday, September 17, 2012

Mwakyembe Atua Ujerumani

  Mhe. Waziri akiwa na Balozi wa tz Berlin Mhe. Ahmada R. Ngemera (kushoto) na Afisa wa Wizara ya mambo ya Nje, Ali Ubwa Mussa
  Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika Majadiliano na Uongozi wa Sekta ya Usafiri wa Anga, Germany
 Mhe. Waziri akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ndege za Airbus, nchini ujeruman (hayupo pichani) pembeni yake ni Mhe. balozi wa tz Berlin.
                     Mhe. Waziri akiwa ndani ya moja ya ndege iliyokuwepo katika maonyesho hayo.
         Mhe. Waziri na ujumbe wake wakiwa katika maonyesho ya Sekta ya usafiri wa Anga mjini Berlin.

Naomba nikutumie baadhi ya picha za ziara ya Mhe. Mwakyembe Berlin, Ujerumani. utaandaa maelezo mazuri wewe mwenyewe. Ila kwa ufupi ni kwamba Mhe. Waziri na ujumbe wake wapo Berlin kuanzia trh 15 hadi 19 sept, 2012. moja ya tukio muhimu ni kusainiwa Mkataba wa Ushirikiano wa Usafiri wa Anga (Bilateral Air Services Agreement - BASA) baina ya nchi hizi mbili tarehe 17 Sept. Aidha, leo tarehe 16 sept, Mhe. Waziri na ujumbe wake walitembelea maonyesho ya Kimaitaifa ya sekta ya Usafiri wa Anga yaliofanyika hapa Berlin. Aidha kwa nyakati mbalimbali, Mhe. na ujumbe wake watakutana na wafanyabiasha na wawekezaji mbalimbali hususani katika sekta ya usafiri (Anga, reli na meli).


Baada ya ziara ya hapa ujeruman, ujumbe wa wataalam (tu) aliofatana nao mhe. waziri utaelekea the Hague Uholanzi kwa ajili ya majadiliano mengine kuhusu usafiri wa anga tarehe 19 hadi 21 sept. Mhe waziri hatushiriki. NAOMBA SANA UIREKEBISHE STORI HII KABLA YA KUITOA ILI ITOE UJUMBE MZURI: SASA NAKULETEA MAELEZO YA PICS NLIZOKUTUMIA.

Dk.Titus Kamani Adai Anachafuliwa

MIKAKATI na kampeni za majitaka zenye lengo la kumchafua Mbunge wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu, Dk. Titus Kamani, zimeanza kubainika kwa kumhusisha na tena na tuhuma za mauaji.

Dk. Kamani, ambaye ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa mpya wa Simiyu, ameanza kuchafuliwa akihusishwa na tuhuma za kutaka kumuua aliyekuwa mbunge wa Busega, Dk. Raphael Chegeni.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, aliwahi kueleza bayana kuwa wamefanya uchunguzi wa kina na kubaini Dk. Kamani hahusiki na tuhuma hizo na kwamba, waliotuhumiwa wameshafikishwa mahakamani.

“Hatumtafuti Dk Kamani, tukimhitaji tutampata lakini katika uchunguzi wetu tumebaini tuhuma hizo hazimuhusu," alikaririwa Kamanda Barlow baada ya kuibuka kwa uvumi kuwa mbunge huyo alikuwa akisakwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, jana, Dk. Kamani amesema kumekuwepo na kampeni chafu za kuhakikisha jina lake linachafuka ili kudhoofisha harakati zake za kukitumikia Chama.

Amesema kuwa tangu alipojitosa kuwania nafasi hiyo, kumekuwepo na mikakati ya kumchafua inayofanywa na baadhi ya wanasiasa wakiwemo waliopo ndani ya CCM na kwamba, hilo amelibaini na atalifikisha kwenye vikao husika.

Dk. Kamani katika taarifa yake amesema kuwa, mbinu chafu hizo zimekuwa zikisukwa na wanasiasa hao kwa lengo la kumchafua na kumchonganisha na wapigakura wake pamoja na jamii imuone kuwa hafai.

“Makovu na visasi vya kushindwa katika uchaguzi uliopita kamwe havitaiharibu Busega wala kunidhoofisha kuwatumia wananchi wangu. Nafahamu hizi ni mbinu chafu kwa ajili ya kuniharibia katika harakati zangu za kuwania nafasi ndani ya Chama," alisema katika taarifa hiyo.

Tayari watu wanaotuhumiwa kuhusika katika njama za kutaka kumuua Dk. Chegeni
wameshapandishwa kizimbani kujibu mashitaka hayo.

Magazeti y leo Jumatatu 17th September 2012