MSINGI wa kila kitu duniani ni kujifunza. Hakuna kinachoshindikana katika kujifunza! Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watu huwa wana asili ya ubishi. Hapo ndipo mwanzo wa matatizo.
Ndugu zangu, huzuiwi kubisha au kubishana, lakini uwe na hoja za msingi zinazoshibisha kile unachokikataa. Ndivyo ilivyo hata katika mapenzi.
Ni vyema kuwa mtu wa kujifunza kila siku. Usishangae kuona ndoa ya Antony na Loveness inadumu kwa muda mrefu. Wanaishi kwa amani na maendeleo katika maisha yao yanaonekana wakati kwako moto unawaka kila siku.
Kujifunza!
Ili uwe bora na uhusiano wako uwe wenye amani siku zote, kubali kujifunza. Mwangalie mpenzi wako, yukoje? Jifunze kutoka kwake. Anapenda nini? Anachukia nini?
Ukijifunza hayo tu pekee, itakuwa hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye kujenga uhusiano wenye amani na upendo. Angalizo moja muhimu, wakati unajifunza au upo na mpenzi wako katika uhusiano, achana kabisa na maisha ya maigizo.
Ukianza maigizo katika uhusiano wako, ni wazi kwamba hata kwenye ndoa vile vile utakuwa mtu wa maigizo tu! Unajua kati ya mambo muhimu ambayo binadamu anatakiwa kuwa nayo makini kwa kiwango cha mwisho cha uwezo wake wa kufikiria ni pamoja na ndoa.
Unapozungumzia ndoa, ujue moja kwa moja unajadili suala la maisha yako. Hapo ndipo ukomavu wa upeo wako unapoonekana. Ndoa si fasheni. Haihitaji kukurupuka...unakutana na mtu disko leo, halafu miezi mitatu baadaye unatangaza ndoa, ni vichekesho!
Kama ndoa ingekuwa ni fasheni, basi mtu angeweza kufunga ndoa na huyu leo, halafu fasheni mpya ikija anaacha na kuoana na mwingine.
Kwa bahati mbaya si hivyo. Ndoa ni maridhiano ya moyo. Unatakiwa kutulia sana wakati wa kufanya uchaguzi wa mtu wa kuingia naye kwenye ndoa. Iko hivi; kama umechagua mwenzi asiye sahihi, uwe tayari kuumia maisha yako yote. Kulia maisha yako yote. Kutokuwa na furaha maisha yako.
Nani anayependa jambo hili litokee? Bila shaka hakuna. Hii ndiyo sababu mada hii ikawepo hapa kwa ajili yako.
Yapo mambo muhimu sana ambayo watu wamekuwa wakiyapuuza kabla ya kufanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa. Ukishaingia ndani ya ndoa, hakuna njia ya kutoka tena, hata ikiwepo si sahihi. Inakuchafua. Inaharibu historia ya maisha yako ya uhusiano.
Uamuzi wa ndoa si wa kujaribu. Unatakiwa kujihakikishia kwamba ni kweli umevutiwa na kila kitu cha mwenzako, kwamba utakuwa naye katika shida na raha. Hayo ndiyo mambo ya kuzingatia.
Nimeshaandika mengi kuhusu sifa za anayetakiwa kuoa au kuolewa (gazeti hili na gazeti dada Risasi Mchanganyiko), lakini nasogea mbele zaidi na kuangalia sababu za kumpenda mtarajiwa wako katika ndoa.
Zipo sababu za msingi sana ambazo unatakiwa kuwa nazo kabla ya kuingia kwenye ndoa ambayo mimi hapa kwenye Let’s Talk About Love naiita kifungo!
Twende tukaone.
KWA NINI HASA?
Lazima nifafanue hili kwanza kabla ya kuendelea. Hivi unafikiri ni kwa nini ni lazima kujiuliza sababu za kumpenda mwenzi wako?
Yes! Ni kwa lengo la kujiwekea usalama katika ndoa yako ijayo. Kujiandalia amani na pumziko la kweli. Kwenye mapenzi ya dhati pekee ndipo vinapopatikana vitu nilivyovitaja hapo juu.
Kwa maneno mengine unatakiwa kuelewa kwamba, ndoa siyo maigizo. Unatakiwa kuangalia vigezo vya muhimu kabla ya kuamua kuchukua uamuzi huo.
NDIYE ULIYEMTARAJIA?
Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu ni kama mwenzi huyo ni wa ndoto zako. Je, yukoje? Marafiki, siku zote kabla ya kuamua kufanya chochote lazima ujiulize kama ndicho ulichokuwa ukikifikiria.
Hata kwa upande wa mwenzi wako, lazima ujiridhishe. Ni kweli ni yule uliyekuwa unamtarajia? Ana sifa unazohitaji? Acha tabia ya kujifariji kwamba utampenda taratibu ndani ya ndoa, hicho kitu hakipo!
Hakuna kujifunza kupenda katika ndoa, lazima ujihakikishie mwenyewe kuwa mwenzi wako ni yule mwenye sifa ulizokuwa ukizitarajia. Hili ni la msingi, maana unaweza kuwa naye siku mbili, ukatamani mwingine nje, kwa nini? Kwa sababu si yule mwenye sifa ulizotarajia.
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers. Ameandika vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na Who is Your Valentine? vilivyopo mitaani.
Friday, July 6, 2012
THEA AJIFUNGUA MTOTO SIYO RIZIKI
MSANII mwenye heshima kunako tasnia ya filamu za Bongo, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ (pichani) amejifungua lakini mtoto wake akiwa amefariki dunia.
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Thea alijifungua mtoto wa kike kwa njia ya kawaida usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita katika Hospitali ya Marie Stopes lakini akawa siyo riziki.
“Unajua familia yao haikutaka mapaparazi wajue kuwa Thea yupo hospitali kwa ajili ya kujifungua kwa sababu hawapendi magazeti hivyo hapa nimefanya kuwaambia tu msinitaje jamani,” kilisema chanzo hicho.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa mwili wa kichanga hicho ulizikwa katika Makaburi ya Mwananyamala jijini Dar juzi Jumanne asubuhi.
Jitihada za kuwapata Thea au mumewe Mike Sangu ili kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda.
Tanzania Asilialive.blogspot.com inawapa pole sana Mr na Mrs Sangu Tunaamini yote ni mipango ya mungu poleni sana.
Chazo: Globalpublishers

AUNT APIGWA NDOA UARABUNI
HABARI za chini kwa chini zinadai kuwa, staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson (pichani) amefunga ndoa huko Dubai katika nchi za Falme za Kiarabu ‘UAE’ na mwanaume anayejulikana kwa jina la Sunday Dimonte, Ijumaa linashuka na kilichopatikana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndoa hiyo ilifungwa Juni 17, 2012 na kuhudhuriwa na rafiki wa karibu wa Aunt aliyejulikana kwa jina moja la Rehema bila ndugu, jamaa na marafiki kutoka Bongo.
KISA CHA KUFUNGA NDOA HARAKA
Habari zinadai kuwa, Aunt alifikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kumwambia hawezi kuvumilia umbali uliopo kati ya Tanzania na Dubai hali ambayo Aunt alihofia kupigwa chini.
SHEREHE KUBWA BONGO
Hata hivyo, mpashaji wetu aliweka wazi kuwa baada ya ndoa hiyo, Aunt ameanza maandalizi ya sherehe kubwa Bongo ambapo atawashirikisha mashostito wake.
“Unajua Aunt amefunga ndoa kule bila kuita nduguze kutokana na umbali, lakini atakaporudi Tanzania ataangusha sherehe ya nguvu ambapo sasa, nduguze, jamaa na marafiki wataalikwa,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA AUNT DUBAI
Ijumaa lilimsaka Aunt kwa njia ya simu ya kiganjani akiwa Dubai, alipopatikana na kuulizwa kama kweli amepigwa pingu za maisha, alifunguka:
“Ni kweli nimefunga ndoa huku Dubai lakini nimesikiasikia kuna watu wanasema nilifanya siri. Siyo siri, ila huku ni mbali na huko nyumbani Tanzani, isingekuwa rahisi kuita watu wangu wa karibu.”
Paparazi: Kwa hiyo ndiyo imetoka hiyo?
Aunt: Hapana, nitakaporudi nyumbani nitafanya sherehe, nitaalika watu, hata wewe, tena itabidi unichangie jamani.
WABONGO WANA WASIWASI
Wakati Aunt akikiri kwa kinywa chake kufunga ndoa, baadhi ya Watanzania waliozinyaka taarifa hizo wanadai wana mashaka.
“Mh! Eti jamani, ni kweli Aunt amefunga ndoa Dubai? Mbona siamini. Au kafunga ya kwenye filamu?” alihoji staa mmoja wa filamu aliposikia ishu hiyo. Chazo:Globalpublishers

MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST. AGREY JIJINI MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA BODABODA
Vedasto Pius baada ya kupigwa vibaya na wananchi.
Mwananchuo mmoja kutoka Chuo cha Ualimu cha ST Aggrey kilichopo Uyole jijini Mbeya, anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma za kuiba pikipiki ya kusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.
Mgonja amesema tukio hilo lilitokea mnamo Julai 2 mwaka huu majira ya saa 8 mchana katika daraja lililopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara ya kuelekea Isanga, Jijini Mbeya.
Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada ya tuhuma za kuiba pikipiki yenye No T 438 BZU aina ya T-BETTER mali ya JOSEPH KAPASI (23) mkazi wa Ilomba jijini hapa.
Kwa upande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae mtuhumiwa alipoanza kuendesha vizuri alitokomea na pikipiki hiyo. Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikutwa eneo la Isanga akielekea barabara ya Chunya akiwa na pikipiki hiyo ndipo alipoanza kupewa kipigo na wananchi wenye hasira kali mpka mauti kumfika.
PICHA KWA HISANI YA http://mbeyayetu.blogspot.com/
Pikipiki inayodaiwa kuibiwa na Vedasto Pius

HASHEEM THABEET KUJIUNGA NA OKLAHOMA CITY THUNDER(OCK)
Habari ambazo zimetambaa, zinasema kwamba mtanzania anayecheza katika ligi ya kikapu nchini Marekani,(NBA) Hasheem Thabeet, atajiunga na timu ya Oklahoma City Thunders kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa Oklahoman, Ingawa mkataba kamili haujawekwa wazi inasemekana kwamba Hasheem ataingia kwa mkataba wa kulipwa mshahara usiopungua $880,000 katika mwaka wa kwanza wa mkataba huo.
Oklahoma City Thunders au OKC kama wanavyofahamika miongoni mwa mashabiki wa mpira wa kikapu na ligi ya NBA, itakuwa ni timu ya nne kwa Hasheem Thabeet kuichezea tangu aliposaini na Memphis Grizzlies kufuatia kuwa wa pili katika NBA Draft mwaka 2009 mbele kwa nafasi moja kutoka kwa mchezaji mwingine anayechezea Thunder hivi sasa,James Harden.
Hata hivyo,Hasheem ameonekana kutokuwa na mwanzo mzuri sana ndani ya NBA tofauti na alipokuwa chuoni Connecticut ambapo aliwahi kuwa Defensive Player Of The Year. Katika michezo 135 ndani ya NBA, Hasheem ana kiwango cha point 2.2, rebound 2.7 na 0.9 blocked shots.
Kwa muda mrefu OKC walikuwa wakimtaka Hasheem na walisikitika mwaka 2009 alipochukuliwa na Memphis.
Ni mwanzo mwingine kwa Hasheem Thabeet na kwa jinsi OKC walivyo,basi huenda tukashuhudia msimu tofauti kabisa wa NBA na bila shaka msimu tofauti kwa Hasheem Thabeet.

BAADA YA MSECHU KULALAMIKA, DAMIAN AZUNGUMZA UKWELI.
Wa kwanza kulia ni Mtanzania Damian staa wa single ya hakuna matata
ambae jumatano July 4 2012 ametoa single mpya inaitwa Taratibu.
Peter Msechu wa tatu kutoka kushoto.
Kama ulifatilia, stori ya aliyekua mshiriki wa Tusker Project Fame Peter Msechu wiki iliyopita kuhusu kulalamikia washiriki wa Tanzania kutolewa kwenye Tusker Project mwaka huu, hatimae mmoja kati ya walengwa hao amekubali kuzungumza kilichotokea.
Msechu alilalamikia wawakilishi wote wawili wa Tanzania Project fame kutolewa na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza washiriki wake wote kutolewa mwaka huu.
Alisema “walijiamini kupitiliza, siku Imani Lissu ameingia kwenye kipindi cha hatari cha kutolewa kulikua na time kwa washiriki waliobaki kumchagua mshiriki gani abaki kwa kupiga kura lakini ukiangalia Damian kama Mtanzania hakumpigia kura mtanzania mwenzake kubaki angalau hata kuonyesha ule uzalendo, sasa hiyo kwa mimi ambae nimeshiriki tulikua tukionywa sasa sijui mwaka huu kama hawakuonywa?
Kwenye sentensi ya pili Msechu alisema “Kwa Damian ambae ndio alibaki kuiwakilisha Tanzania Tusker Project mahojiano ambayo aliyafanya baada ya kuingia kwenye kipindi cha hatari cha kuomba kura mwisho wa siku alisema hawa majaji walionifanya niingie kwenye kipindi cha hatari walifanya maamuzi mabovu”
Damian alisema maneno yafuatayo “by the way ule ni mchezo tu kwa sababu vitu vingine tunapangwa, kunakua na muongozaji ambae anasimamia hizo ishu, unapewa Idea za nini cha kufanya ili kuchochea kitu fulani, hausemi vile kwa mtazamo wako kwamba Majaji wamekosea, unaambiwa cha kufanya ili kuifanya Tusker Project iwe stori zaidi…. mimi niliikubali hiyo idea kwa sababu walinipa sababu kwamba unajiweka sokoni wewe mwenyewe kwa hiyo lazima uonyeshe kwamba wewe sio dhaifu, ambapo mwongozaji alisema pia kwamba tunatakiwa tuwape majaji upinzani, sio kufika mbele yao tu na kila kitu unasema asante… lakini unaweza kuwauliza maswali unaweza kuwaambia chochote majaji kwa hiyo ile kuongea vile ilikua sehemu ya mchezo” Chanzo: millardayo.com

ILICHOSEMA SIMBA KUHUSU NYOSSO NA OKWI KUHAMIA YANGA.
Nyosso.
BEKI wa Simba SC Juma Said Nyosso amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu hiyo baada ya mkataba wake mwanzo kumalizika hivyo kumaliza tetesi kwamba anaweza kuhamia kwa watani wa jadi, Yanga SC.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia blog ya BIN ZUBEIRY kwamba Nyosso alisaini mkataba huo Julai 1 mwaka huu.
Kaburu alisema kwamba Simba ina imani na beki huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na ndio maana imemuongezea mkataba.
Aidha, Kaburu aligusia suala la beki wao, Kelvin Yondan aliyehamia kwa watani wa jadi Yanga akisema bado ni mchezaji wao halali na wameshapeleka malalamiko yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wanasubiri majibu.
Kuhusu Tetesi za Emmanuel Okwi kuhamia Yanga kama ilivyoandikwa na magazeti kwamba amesaini mkataba usiku wa manane, Kaburu amekanusha hizo taarifa kwenye kikao na wanahabari ambapo alimpigia simu Okwi na kumuweka loudspeaker na wote kumsikia akikanusha ambapo kwa sasa anajiandaa kwenda kufanya soka la majaribio Italy.
Kaburu pia amesema mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu tayari amejiunga na wenzake kambini visiwani Zanzibar, ambako timu hiyo inashiriki Kombe la Urafiki.
Kaburu amesema Simba itaendelea kuwa Zanzibar hata baada ya michuano hiyo, wakijiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 14, Simba wakifungua dimba na URA ya Ugandea Julai 16.

HIKI NDICHO WAZIRI MKUU ALICHOMJIBU FREEMAN MBOWE BUNGENI KUHUSU DR ULIMBOKA.
Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema serikali imeagiza kuzingatiwa sheria ya vifo vyenye utata kwa kufanyika uchunguzi wa kina juu ya vifo hivyo ambapo pia amekanusha stori kwamba Tanzania imechafuka kwenye anga za kimataifa kutokana na matukio mbalimbali yaliyotokea.
Hii ni stori kutoka 104.4 Dodoma bungeni wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo ambapo ameamlfy kwamba kuwepo kwa hisia kuwa serikali inahusika katika mauaji ya raia sio sahihi na hata ishu ya Kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka Steven kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika sio vizuri ikatumiwa kama mfano.
Freeman Mbowe alimuuliza waziri mkuu kwamba “Mheshimiwa Waziri mkuu katika nchi yetu kwa muda mrefu sasa yamekuwepo mauaji mengi na baadhi ya vifo hivi vimekua na utata mkubwa na baadhi ya vifo hivi vimekua vikihisiwa kuhusisha vyombo vya dola kama vile jeshi la Polisi, lakini ni kweli kwamba hisia za dola kuhusika katika mateso na mauaji ya raia zimeendelea kuwepo na jinsi ninavyouliza swali hili sifa ya taifa letu iko mashakani katika anga za kimataifa kutokana na mateso ambayo yanaonekana yalikua na kusudio la mauaji ambayo alifanyiwa mwenyekiti wa madaktari Dr Steven Ulimboka”
Alichojibu Waziri mkuu ni hiki….. “Sio kweli kwamba jina la nchi yetu limechafuka, kuchafuka sana kwa lipi? ukisema hivyo ni lazima vilevile uwepo ushahidi wa dhati unaoonyesha kwamba ni kweli serikali inahusika, sasa umetumia mfano wa Ulimboka… sio mfano mzuri, we huna ushahidi kama ni serikali imefanya hivyo na hakuna mpaka sasa anaeweza kusema ana ushahidi huo, ndio maana tulisema mara ya mwisho kwamba ni vizuri jambo hili likafanyiwa uchunguzi wa kina ili tujue kilichotokea hasa ni kitu gani”
Kwa kumalizia kumjibu Freeman Mbowe, Waziri mkuu amesema “hainiingii kichwani hata kidogo kwa mtu ambae tumekua tunafanya nae kazi muda wote alafu sisi hao hao tuchukue hatua tena ya kutaka kwenda kumuadhibu kwa namna iliyotokea, haiingii kichwani”
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Waziri Mkuu amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili ambako hivi karibuni taasisi ya moyo itazinduliwa, ameamplfy pia kwamba hatua nyingine ni kuipandisha hadhi hospitali ya Jeshi Lugalo ili kuwa hospitali ya rufaa.

Subscribe to:
Posts (Atom)