Tuesday, August 28, 2012

Ghasia Mombasa Baada Ya Aboud Rogo Kuuawa

Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa kiisilamu ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa pwani mwa Kenya.

Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa

Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini Mombasa.

Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.

Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.

Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa za mchana.

Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.

Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab

Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.

Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.

Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Sensa Ya Watu Na Makazi, Kasoro Zashamiri

SENSA ya Watu na Makazi jana iliingia siku yake ya pili, huku kasoro kadhaa ikiwamo ukosefu wa vifaa, upungufu wa makarani na watu kugoma kuhesabiwa vikiripotiwa.Katika baadhi ya maeneo hadi jana, wananchi walikuwa hawajaanza kuhesabiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutokana na ukosefu wa vifaa na makarani.

Ofisa Uhamasishaji wa Sensa Taifa, Said Ameir alikiri kupata taarifa za kasoro hizo lakini akaeleza kushangazwa na chanzo chake, akisema: “Vifaa tulivigawa maeneo mbalimbali nchini kulingana na mahitaji. Tunashangazwa na taarifa hizo kwamba hata wengine wamekosa reflector (makoti ya kuakisi mwanga) na vitambulisho.”

“Tunachofanya sasa ni kuchunguza tatizo hilo limeanzia wapi na limesababishwa na nini. Vilevile tunajitahidi kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinapelekwa sehemu hizo ili kazi hiyo iendelee kama kawaida.”
Alisema pamoja na kasoro hizo, kazi hiyo inaendelea vizuri na itakamilika ndani ya siku saba kama ilivyopangwa.

Kasoro

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

 Release No. 133
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Agosti 27, 2012

KOMBAINI COPA COCA-COLA YAENDA AFRIKA KUSINI
Kombaini ya Copa Coca-Cola Tanzania (Dream Team) yenye wachezaji 16 imeondoka Leo (Agosti 28 mwaka huu) asubuhi kwenda Afrika Kusini kwenye kambi itakayokuwa chini ya makocha wa Chelsea.

Makocha watano kutoka timu ya Chelsea ya Uingereza ndiyo watakaoongoza kambi maalumu ya kimataifa ya Copa Coca-Cola yenye wachezaji 140 kutoka nchini 15 itakayofanyika jijini Pretoria kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 8 mwaka huu.

Robert Luke Udberg, Russel William Banyard, Oliver Staurt Woodall, Shane Jason Hughes na Dean Aaron Steninger kutoka Chelsea FC Foundation ndiyo wanaounda jopo hilo la makocha litakalowanoa vijana hao wenye umri chini ya miaka 17.

Wachezaji wanaounda Dream Team iliyotokana na michuano ya Copa Coca-Cola iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 24 hadi Julai 15 mwaka huu ni Abrahman Said Mohamed (Zanzibar), Ayubu Alfan (Dodoma), Baker Hamad (Tanga), Edward Joseph (Ruvuma), Hassan Kabunda (Temeke) na Joseph Chidyalo (Dodoma).

Wengine ni Mtalemwa Katunzi (Morogoro), Mwarami Maundu (Lindi), Nankoveka Mohamed (Ilala), Nelson Peter (Morogoro), Rajab Rashid (Mwanza), Said Ramadhan (Kagera), Shiza Kichuya (Morogoro), Shukuru Msuvi (Temeke), Tanganyika Suleiman (Kigoma) na Tumaini Baraka (Kilimanjaro).

Nchi nyingine zitakazokuwa na washiriki katika kambi hiyo ni wenyeji Afrika Kusini, Burundi, Cameroon, Congo Brazzaville, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Swaziland, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Hii ni mara ya sita mfululizo kwa kampuni ya Coca-Cola kupeleka Dream Team kwenye kambi za kimataifa. Mwaka 2007 na 2008, timu hiyo ilikwenda Brazil wakati mwaka 2009, 2010 na 2011 ilikuwa Afrika Kusini.

                                  Boniface Wambura Mgoyo
                                        Ofisa Habari
            Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Msimamo Wa Mnyika Juu Ya Mauaji Ya Morogoro

Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.

Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano.

Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video. Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam.

Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa. States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years’ resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot.

Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya  wengi.

John John MNYIKA,
27 Agosti, 2012

Magazeti ya Leo Jumanne 28th August 2012