Wednesday, April 10, 2013

Magazeti ya leo Jumatano ya 10th april 2013




HIVI NDIVYO UHURU KENYATA ALIVYOAPISHWA NCHINI KENYA

                                            Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, akiapishwa.
                                        Rais Uhuru Kenyatta na 'First lady', Margaret Kenyatta.

MVUA YALETA MAAFA WILAYANI ARUSHA WANANCHI KADHAA HAWANA MAHALI PA KUISHI

 Hali ya mvua inayonyesha kwenye mkoa wa Arusha imewaacha wakazi wa vijiji vya Alkokola na venginevyo kadhaa kwenye kata hiyo wilaya ya Arusha wakiwa hawana makazi na mahala pakukaa baada ya mvua kunyesha usiku wa kuamkia Jumatatu.
Pichani ni maji yakiwa yanashuka kwenye maeneo ya Ngaramtoni ya Chini na Burka huku wakazi wa maeneo hayo wakiyakimbia maeneo yao kama walivyokutwa na kamera yetu.

Thatcher afariki dunia

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Thatcher (87), amefariki dunia  jijini London.

Thatcher, ambaye ni mwanamke pekee kushika nafasi hiyo Uingereza, alifariki dunia katika Hoteli ya Ritz alipokuwa akiugulia. Habari zilizopatikana zimeeleza kuwa Thatcher alifariki dunia kutokana na kuugua ghafla ugonjwa wa kiharusi.CHANZO MWANANCHI

"MIMI NDIYE NILIYEWAPELEKEA POLISI ILE VIDEO YA LWAKATARE"...MWIGULU NCHEMBA

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba, amekiri kuhusika na video inayomwonesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare.

Nchemba amekuwa akitajwa na viongozi wa CHADEMA kuwa anahusika kutengeneza video hiyo, kwa kuwa aliwahi kutamba wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni kuwa anayo video inayowaonesha viongozi wa chama hicho wakipanga mauaji.

Hata hivyo, tangu Nchemba atoe kauli hiyo Januari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilikaa kimya hadi Machi 12 lilipomkamata na kumhoji Lwakatare, siku moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa You tube na mtu anayejiita ‘Bukoba Boy’.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Nchemba alikiri kuwa ndiye aliyeipeleka video ya Lwakatare polisi na kwamba alifanya hivyo baada ya kuripoti kuandikiwa ujumbe wa simu wa kutishiwa maisha na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

"NIMEAMUA KUMSAMEHE LULU MICHAEL....YALIYOTOKEA NAMWACHIA MUNGU"...MAMA KANUMBA

Mama wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa upande wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia mungu

Akizungumza katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo humkumbuka mwanaye

Alisema kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto kwake, mume, rafiki, kaka  alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na alimfanya kuwa karibu kwake na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo imemfanya kuwa mpweke mpaka leo