Tuesday, July 24, 2012

Fight for your real Love Wema




MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ametajwa kuwa kichocheo cha kurejea kwa penzi la vijana wenye umaarufu mkubwa nchini kwa sasa, Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ na Wema Isaac Sepetu.

Uwazi, lina mkanda wa video, unaowaonesha Diamond na Wema pamoja kwa mara ya kwanza, baada ya muda mrefu wa kutupiana maneno mengi ya kashfa, huku kila upande ukimshusha hadhi mwenzake.
Diamond na Wema, walinaswa kwenye Tamasha la Kigoma All Stars, lililoandaliwa na Zitto kisha kufanyika Julai 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Shukurani kwa Zitto, kwani kupitia tamasha hilo, Diamond na Wema, waliweza kudhihirisha kwa kila mtu kwamba uhusiano wao sasa umerejea upya kwa kuambatana kimahaba ndani ya Mkoa wa Kigoma.

SAFARI ILIVYOKUWA TAMU
Watu wengi wakijua kwamba kuna uhasama mkubwa kati ya Wema na Diamond, Julai 17, mwaka huu, ilikuwa ni mshangao wa aina yake kwa waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Kigoma, baada ya vijana hao kushuka wakiwa wameongozana.

Diamond akiwa amevaa shati jekundu na tai nyeusi, chini akiondokea suruali ya jeans rangi ya bluu iliyopaushwa kimodo, huku Wema akitokelezea kwa koti la rangi ya maziwa, ndani blauzi nyeusi, halafu wote wameyaficha macho yao kwa miwani nyeusi, waliwaka vilivyo ndani ya Ujiji, Kigoma.
Baada ya kuwasili Kigoma, Wema na Diamond walielekea Hoteli ya Tanganyika Beach (ipo ufukweni mwa Ziwa Tanganyika) ambako walipata pumziko walilohitaji kabla ya nyota huyo wa wimbo wa Mbagala, hajaelekea Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye Tamasha la Kigoma All Stars a.k.a Leka Dutigite.

WEMA ALIFUATA NINI KIGOMA?
Minong’ono ilitawala kila kona ya Mkoa wa Kigoma kwamba Wema amekwenda kuwakilisha Leka Dutigite, hivyo wakataraji kumuona Uwanja wa Lake Tanganyika, akitoa sapoti yake kwenye tamasha hilo.
Wapo ambao waliacha shughuli zao kwa ajili ya kwenda kumuona Wema tu uwanjani lakini waliambulia patupu, kwani mrembo huyo hakuonekana kabisa.
Kutokana na hali hiyo, wale waliovumisha stori kwamba Wema amekwenda Kigoma a.k.a Lwama, walionekana wazushi wasiofaa kusikilizwa, bila kujua kwamba mtoto alijificha ndani ya Hoteli ya Lake Tanganyika Beach.

HAKIKA WANAPENDANA
Kama ukaribu wao ulisababishwa na tamasha lililoandaliwa na Zitto peke yake, basi wangekuwa na muonekano ‘feki’ sehemu chache wanazopita lakini kinyume chake wao walithibitisha wanapendana haswaa!


Diamond, alishindwa kujichanganya na wasanii wenzake aliokuwa nao kwenye shoo ya Kigoma kama akina Said Juma ‘Chegge’, Peter Msechu, Banana Zorro, Mwasiti Almasi na wengineo, badala yake muda mwingi aliutumia kuwa umbali wa mita sifuri kutoka alipo Wema.
‘Mtundu’ wa nyimbo mbili mpaka sasa, Nai Nai na Baadaye, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ndiye pekee aliyekuwa jirani na vijana hao maarufu, walioamua kurejesha penzi lao kupitia mwavuli wa shoo hiyo.

Kwa upande mwingine, ni kama vile waliamua kwenda kufanya tambiko nyumbani asili kwa mume mtarajiwa, yaani Diamond kwa sababu chimbuko la Wema ni Mkoa wa Tabora, japo baba yake, Balozi Isaac Abraham Sepetu, amejichimbia Zanzibar kwa miaka mingi.
Mtu mmoja, mwenye hulka ya kutopitwa na mambo, akamueleza ripota wetu kuwa Julai 18, wasanii hao walikwenda Hifadhi za Gombe na Mahale, mkoani humo lakini jioni yake, Diamond aliongozana na Wema mpaka kwa babu yake, eneo la Ujiji Posta, mkoani humo ambako walisomewa dua na Babu Nasibu.

RAHA NDANI YA TILAPIA HOTEL
Safari ya furaha kwa Wema na Diamond, ilihamia ndani ya Jiji la Miamba ya Mawe, Mwanza ‘Rocky City’ kwenye Hoteli ya Tilapia, iliyopo ufukweni mwa Ziwa Victoria, eneo la Capri Point, hiyo ikiwa Julai 19, 2012.

Habari zinapasha kuwa wawili hao, walipumzika kwenye hoteli hiyo kwa muda mfupi, wakati wanasubiri saa ya ndege yao ya kuwatoa Mwanza hadi Dar es Salaam ifike.

Ndege waliyopanda Diamond na Wema kutoka Kigoma, ilitua Mwanza saa 9:30 alasiri, hivyo kuanzia muda huo, waliutumia Tilapia Hotel mpaka saa 2:30 usiku, wakaripoti Uwanja wa Ndege wa Jiji la Miamba ya Mawe, kabla ya saa 3:50 usiku, usafiri huo wa anga, uliitupa mkono ardhi ya Mwanza mpaka Dar es Salaam.

AIR PORT DAR ES SALAAM
Mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra Sammi’, alionekana Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, kuanzia saa 4:45 usiku (Julai 19), hivyo kwa jicho la ripota wetu, ikawa wazi kwamba amekwenda hapo kumpokea mwanaye kipenzi, Diamond ‘Sukari ya Warembo’.


Kutokana na safari hiyo kuwa mguu wa Diamond uliambatana na wa Wema, kwenda kwenye shoo ya kutoa shukurani nyumbani kwao Kigoma, ni wazi Mama Nasibu (Mama Diamond) alikuwa pale pia kwa minajili ya kumlaki mkwe a.k.a Mka Mwana.

PW 415 YAWASILI DAR
Diamond na Wema, walipanda ndege ya Kampuni ya Precision Air, PW415 na ilipotimia saa 5:30 usiku, ilitangazwa kuwa ndiyo inawasili kwenye uwanja huo wa ndege wenye jina la muasisi wa taifa huru la Tanganyika na baadaye Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ‘Baba wa Taifa’.
Milango ya saa 5:52, Diamond na Wema, walipita kwenye mlango wa wanaowasili (arrivals gate), wakiwa sambamba na Ommy Dimpoz, walipokelewa na Mama Nasibu hadi sehemu ya maegesho ya magari uwanjani hapo.

Timu nzima, ilijipakia kwenye gari la Diamond aina Toyota Land Cruiser Prado, rangi ya fedha, wakatoweka eneo la uwanja huo.

DIAMOND KWA WASIWASI
Saa 6:14 usiku (Julai 20), Diamond alimpigia simu ripota wetu, eti akahoji kilichompeleka uwanja wa ndege. Mahojiano yalikuwa hivi;
DIAMOND: Kiongozi nilikuona Air Port, pale ulikuwa unafanya nini?
RIPOTA: Aah, kumbe uliniona? Mlivyojikausha nikadhani hamkuniona. Kuna mzigo wangu nilikuwa naufuatilia pale.
DIAMOND: Mzigo wapi? Naomba uniambie ukweli.
RIPOTA: Acha hizo dogo, unafikiri mimi nilikufuata wewe? Tena ningejua unafika leo, halafu ujio wenyewe ni huo, ningetega kamera zangu na tuwapige picha za kutosha.
DIAMOND: Aah, usifanye hivyo kiongozi.
Baada ya mazungumzo hayo, Diamond kila alipopigiwa simu hakupokea mpaka gazeti hili linanyanyuka kwenda kiwandani.

UFAFANUZI WA WEMA
Wema alipopigiwa simu na ripota wetu, alijibu kuwa yeye na Diamond hawajarudisha mapenzi, isipokuwa hivi sasa wako karibu kama marafiki wazuri kwa ajili ya kusaidiana mambo mbalimbali.
“Kusema ukweli kwa sasa sijafikiria kurejesha mapenzi na Diamond ila tupo karibu kama marafiki,” alisema Wema.

ZITTO NAYE
Jitihada za kumpata Zitto aweze kuzungumzia kurejea kwa penzi la Wema na Diamond kwenye tamasha aliloliandaa, hazikuzaa matunda. Muda wote naibu huyo wa Kambi ya Upinzania Bungeni, simu yake ilikuwa imezimwa.

WANANCHI WAMPONGEZA
Fununu kuwa Wema na Diamond wamerudiana zilivuma kwa kasi ndani ya mitandao ya kijamii na maoni ya wengi yakaelekeza pongezi kwa Zitto, kwani kabla ya hapo, mastaa hao walikuwa na uhasama mkubwa.

UNAKUMBUKA?
Malumbano yao kwenye vyombo vya habari? Diamond alipomfedhehesha Wema baada ya kukataa kupokea fedha zake alizomtuza kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam Machi mwaka huu? Je, kauli nzito za Mama Wema, Mariam Sepetu kwamba Diamond ni kijana mbaya na hafai?

JIULIZE SASA
Mpaka hapo bado unabisha kwamba mapenzi ni upofu? Unaendelea kukataa kwamba mapenzi hayaulizwi kwa nini? Diamond alipoachana Wema, alitua kwa Miss Tanzania namba mbili 2006-07, Jokate Mwegelo, je, penzi lao limeyeyuka au bado lipo kwa sura gani?

Kutoka Mwandishi Wetu:Globalpublishers.com

Waziri Kagasheki Amaliza Ziara Ya kutangaza Utalii Marekani

 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Sued Kagasheki akimkabidhi tuzo ya kinyago Bi. Jena Fox, mwanahabari kutoka Jarida maarufu la nchini Marekani la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Utalii nchini kufuatia uandishi mzuri wa makala mbalimbali za kutangaza ukanda wa utalii wa kusini katika soko la Marekani
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiwafnya mahojiano na mwanahabari Jena Fox kutoka jarida la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni.Katika mahojiano hayo Balozi Kagasheki alipata fursa ya kuelezea furdsa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Sloyce Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Wageni cha Marekani (USTOA) Bi. Peggy Murphy mara baada ya kufanya nae mazungumzo juu ya namna ya kuongeza idadi ya wageni nchini kutoka Marekani jijini  New York hivi karibuni.

Kesi Ya Lulu Yapigwa Tena Kalenda

KESI ya msanii wa fani ya filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, imeahirishwa hadi Agosti 20 mwaka huu, kutokana na Jaji anayeisikiliza, DK Fauz Twaib, kuwa na majukumu mengine.Akiahirisha kesi hiyo jana, Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Amir Msumi, alisema Jaji DkTwaibu, anakabiliwa na majukumu mengine.

“Jaji Twaib ni Mwenyekiti wa Baraza la Kodi na pia ni Mwalimu wa Sheria katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hivyo kwa sasa anatekeleza majukumu mengine katika nafasi hizo.Kwa hiyo kesi hiyo inaahirishwa hadi Agosti 20, mwaka huu,” alisema Msumi.

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, yanayodaiwa kufanyika April 7 mwaka huu nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kesi hiyo ya msingi haijaanza kusikilizwa, tayari imeshafikia ngazi ya Mahakama ya Rufani, baada ya kuibuka kwa utata wa umri wa mshtakiwa huyo.

Utata huo uliiobuka baada ya mawakili wanaomtetea msanii huyo, kuomba kesi isikilizwe katika Mahakama ya Watoto kwa madai kuwa mteja wao bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama, inavyoonyesha katika hati ya mashtaka. Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Watatu Wamekufa, 38 Wajeruhiwa Ajali Ya Basi La Tony Sley, Iringa

                                                   Basi la Tony Sley baada ya Kupata Ajali jana Usiku
               Hili ndilo basi la Tony Sley ambalo limepata ajali jana usiku na kuua watu watatu na kujeruhi 38
                              Majeruhi wakisubiri matibabu Hospitali ya mkoa wa Iringa.
                                    Majeruhi wakipatiwa huduma Hospitali ya mkoa wa Iringa
Majeruhi wa basi la Tony Sley Bi Agnesy Lukasi akiwa na mtoto wake Dina Lukasi (4) wakisubiri kupewa matibabu katika Hospital ya mkoa wa Iringa baada ya kufikishwa hapo usiku huu wakitokea eneo la ajali mlima wa Kitonga
                                  Mtoto akiwa ameshapatiwa Matibabu hospitalini Hapo
Ajali ya basi ya Tony Sley yenye namba za usajili T 218 ACH lililokuwa likitokea Tunduma mkoani Mbeya kwenda jijini D’Salaam imeua watu watatu wakiwemo wawili raia ya Zambia na mmoja mtanzania na kujeruhi wengine 38.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la kona za mlima wa kitonga kwenye barabara kuu ya Iringa –D’Salaam jana majira ya saa 12 za jioni baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kulipita lori lilolokuwa mbele yake.

Wakizungumza katika eneo hilo na Hospitali ya mkoa wa Iringa majeruhi wa ajali hiyo waliolazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilolo Ilula walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wao alisema Agnes Lukasi (30).

Agnesy alisema kuwa kwa upande wake alikuwa amekaa siti ya mbele na wakati dereva huyo akifanya uzembe huyo walikuwa wakimshuhudia hata kujaribu kumuonya bila mafanikio.

Alisema kuwa katika basi hilo alikuwa na mtoto wake Dina Lukas (4) ambaye pia amejeruhiwa katika paji lake la uso.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamhanda ambaye alifika eneo la tukio pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa aliuthibitishia mtandao huu kuwa jumla ya abiria 38 ndio waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Aliwataja baadhi ya majeruhi ambao majina yao yamepatikana na kulazwa katika hospital teuli ya mkoa wa Iringa kuwa ni pamoja na Boyd Simwings(43) , Violet Chambale(35),Zilombo Wake(38),Warmen Mambwe (33),Eugen Maluge(39), Mwamba Andrew (27) , Bright Mwalukanga (33) na John Lemba( 30) wote raia wa Zambia.

Wengine ni Martine Shombe( 29) mkazi wa Tunduma, Zainabu Amuri (32) mkazi wa D’Salaam , Efrain Mwampashi (31) mkazi wa Tunduma, Sebastian Mhaya(25) mkazi wa Tunduma, Vedastus Benjamin (11) mkazi wa Tunduma, Mrashi Handu (38) mkazi wa Igulusi, Juma Ramadhan (40) mkazi wa Tunduma, Twaribu Juhim (39) mkazi wa Arusha, Muka Muka (26) mkazi wa Tunduma, Edina Ramadhan (3) mkazi wa Tunduma na Benjamin Enock (33) mkazi wa Mbeya.

Wengine ni Agness Lukas (30) mkazi wa Tunduma , Dina Lukas (4) mkazi wa Tunduma Beatrice Msakanti( 42) mkazi wa Zambia, Besa Shadrack (32) mkazi wa Zambia na Mary Mumba (48) mkazi wa Zambia pia.

Alisema majina ya majeruhi zaidi yatapatikana hivi karibuni baada ya majeruhi waliopo Hospital ya wilaya ya Kilolo Ilula kufika mjini Iringa.

Mbali ya majeruhi hao pia aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Cla Pily (32) na Dany Kawina (43) wote wafanyabiashara raia wa Zambia pamoja na Abel Nelson (32) ambaye ni mtanzania.

Kamanda Kamhanda mbali ya kueleza masikitiko yake juu ya ajali hiyo bado aliwaonya madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuendesha kwa uangalifu wa hali ya juu na kuwa jeshi lake mkoani Iringa halitalala kuwabana madereva wazembe.Mungu awapenye majerui wote kwa haraka waendelee na kazi zao na marehemu wapumzike kwa amani.  Chanzo: www.francisgodwin.blogspot.com

WAZIRI AJIUZULU ZANZIBAR KUTOKANA NA AJALI YA MV SKAGIT.



Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu kufuatia shinikizo za watu na maandamano.

Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.

Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa watu.

Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.

Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.

Taarifa kutoka ikulu zinasema kuwa, uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja.

.UKIMWI USIOSIKIA DAWA AFRIKA MASHARIKI NDIO HUU.

                                                        Makao Makuu ya WHO Geneva.
Inawezekana stori nyingine huwa unazichukulia poa, lakini hii usiichukulie poa hata kidogo.

Ninachotaka kukwambia ni kwamba aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekua ukiongozeka kwenye hili bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.

BBC wamesema, kuna ripoti ilimeandikwa na wataalam kwenye jarida la kisayansi la Lancet, ambapo uchunguzi kwa watu 26,000 ndio umekuja na hayo majibu.

Wataalamu hao wamesema hali hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawata zingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.

hali hiyo inazusha hofu zaidi katika bara la Afrika ambako hakuna njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa maradhi ya Ukimwi.

Watatifi kutoka shirika la Afya duniani-WHO na chuo kikuu London wamegundua kwamba aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa unapatikana zaidi kwenye nchi za Afrika Mashariki, Rwanda, Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda.

Yani wanasema asilimia 26% ya waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asilimia 14 katika nchi zilizo kusini mwa Afrika
Lakini kwenye nchi za mwa Marekani, Afrika Magharibi na kati hakuna kitu kama hicho.

Chanzo kikubwa cha hayo yote ni kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa ipaswavyo.

Hii stori imetoka siku tano tu baada ya kumsikia waziri mkuu Mizengo Pinda akiamplfy habari njema kuhusu maambukizi ya vizuri vya ukimwi kupungua Tanzania.

Magazeti ya Leo Jumanne 24th July 2012