Friday, May 3, 2013

UPDATE: MATOKEO YOTE YA KIDATO CHA NNE 2012 YAMEFUTWA NA YATASAHIHISHWA UPYA

Habari kutoka bungeni ni kwamba matokeo yote ya  kidato  cha  nne yamefutwa na yatasahihishwa upya ( Re -grading ) haraka iwezekanavyo..

Taarifa ya tume iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza sababu za kufeli vibaya kwa watahiniwa wa kidato  cha nne  imesomwa  bungeni  leo  na  mh.LUKUVI.

LUKUVI amesema sababu zilizosababisha  wanafunzi  wafeli   ni upungufu wa waalimu, mazingira magumu a kufundishia, idadi kubwa ya shule za sekondari iliyopelekea idadi kubwa ya watahiniwa  na  utaratibu  mbovu  wa  baraza  la  mitihani  uliotumika  bila  kuwashirikisha  wadau  wa  elimu

Mh.  LUKUVI amesema kuwa NECTA haikufuata vigezo vya kuwafaulisha wanafunzi kwa kufuata STANDARDIZATIONS na CONTINOUS ASSESSMENTS. ...
Hivyo  basi, matokeo  hayo  YAMEFUTWA  na  MATOKEA  YATAFANYIWA RE-GRADING

Magazeti ya leo Ijumaa ya 3th May 2013





NEEMA KWA WALIOFELI FORM 4:..MARKS ZAO ZITAPANGWA UPYA

 TUME ya kuchunguza sababu za kufeli kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya mitihani ya kuhitimu mwaka 2012 imekamilisha kazi yake na taarifa za uhakika zilizolifia gazeti hili zinasema , upangaji alama zao utafanyika upya.

Kama ambavyo gazeti hili lilivyobaini katika uchunguzi wake wa kiuandishi kwamba kulifanyika mabadiliko ya utoaji alama kwa ajili ya mitihani waliyofanya wanafunzi mwaka huo (2012) bila maandalizi kwa wadau, tume hiyo imependekeza alama zipitiwe upya (regrading).

Katika alama za awali, alama D anapoyopewa mtahiniwa baada ya mtihani wake kusahihishwa ilikuwa ni kuanzia alama 21 kwenda mbele na F ilikuwa 20 kushuka chini lakini katika mabadiliko yaliyoleta ‘maafa’ ya kufeli kwa watahiniwa wa mwaka jana, alama D ilianzia 35 na kuendelea, wakati ile ya kufeli (F) ilianzia alama 34 kushuka chini.

FIFA YAWARUDISHA MALINZI NA WAMBURA KUGOMBEA TFF

Kuna taarifa kwamba wagombea wawili, Jamal Malinzi na Michael Wambura wamerudishwa kuwania nafasi walizokuwa wakipigania kuzipata katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Taarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeandika barua ambayo imeshatua Fifa tayari kuwarejesha Malinzi, Wambura na wengine waliokuwa wanagombea.

Uongozi wa TFF unatarajia kuzungumza muda mfupi ujao kuanzia sasa katika ofisi zake katika eneo la Ilala jijini Dar es Salaam.

Tayari Salehjembe ametega masikio kuhusiana na kitakachotokea na atatutaarifu kama ni hiki kutoka ndani au kutakuwa na mabadiliko.

"TANZANIA NI MUHIMU KULIKO CHADEMA.....SIPO TAYARI KUSUSIA MCHAKATO WA KATIBA".....HAYA NI MAJIBU YA PROFESA BEREGU KWA DR SLAA

Kutoka Raia Mwema:

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, "If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country", akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

MASWALI MATANO ALIYOULIZWA GADNER G KUHUSIANA NA WOSIA WA KIFO CHA LADY JAYDEE

Jana  Lady Jaydee  alitoa  wosia  akidai  kuwa  SIKU  AKIFA  RUGE  wa  CLOUDS  fm  asiguse  katika  mazishi  yake  na  Radio Clouds  Fm  isithubutu  kutangaza  wala  kutia  neno  lolote  katika  msiba  huo......

Gadner  G  ameamua  kuvunja  ukimya  na  kuufafanua  wosia  huo kupitia  TBC FM  wakati  alipohojiwa  na  mtangazaji  Dan Chibo  katika  kipindi  cha  The Takeover na  haya  ndo  mazungumzo  yao...

Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.

Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?