Tuesday, May 28, 2013

BREAKING NEWS: ALBERT MANGWEA AFARIKI DUNIA....

Habari  zilizotufikia  ni  kwamba  msanii  Albert Mangwair  amefariki  dunia akiwa  Afrika  kusini

Chanzo  cha  kifo  hicho  bado  hakijafahamika  lakini  taarifa  za  awali  zinadai  kuwa  msanii  huyo  hakuamka  tangu  alipolala  jana.

Mtandao huu unaendelea  kuifuatilia  habari  hii 

R.I.P   Ngwair

"SINA SHAKA NA UMAARUFU WANGU"....LOWASSA

MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema hana shaka na umaarufu wake Monduli wala Tanzania kwa ujumla.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa Kata ya Makuyuni huku akikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupeleka mgombea wake katika Kata hiyo.

“Eti hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani Monduli ya Lowassa wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli?,” alihoji Lowassa na kuongeza:

“Ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu Monduli wala Tanzania.”

Katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona wakikiadhibu CHADEMA kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote nchini.

KESI YA JAYDEE YARUSHWA MPAKA JUNE 13.

 Lady Jay Dee akiwa na mumewe Gardner Habash wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni

Mwanamuziki Judith Wambura-Habash --Lady Jay Dee-- alifika katika mahakama ya Kinondoni leo kama ilivyotakiwa kwa mashitaka aliyofunguliwa hapo. Baadaye amefahamisha kuwa ameambiwa arudi tarehe 13 Juni 2013.
Kesi imetajwa tena tar 13 June 2013. Saa 5 asub.

PENZI LA WASTARA LAGOMBANIWA.....

  TAKRIBAN  wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.

Akizungumza na mwandishi wetu  akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.

“Jamani mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema Wastara.

Wastara alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure kwa sababu kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado anasikia harufu ya mumewe Sajuki.

“Bado harufu ya Sajuki ipo mwilini mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto wa mwenzao wanakosea sana, sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,” alisema Wastara mwenye mtoto mdogo aliyezaa na Sajuki.

JACK WOLPER ALIA NA MATAPELI YANAYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA JINA LAKE KUOMBA HELA WATU

Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.

Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies, mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela?

NEEMA KWA WALIOFELI KIDATO CHA NNE....UFAULU WAONGEZEKA, MATOKEO NI MUDA WOWOTE

Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.

Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.

Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.