MGOGORO wa gesi umeingia sura mpya, baada ya viongozi wa dini mkoani Mtwara kuungana na wananchi kupinga usafirishwaji wake kwenda Dar es Salaam, huku Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, akitoa ufafanuzi wa faida za mradi huo kwa taifa.
Mbali na ufafanuzi huo, Waziri Muhongo amemlipua Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji kwa msimamo wake wa kuungana na wananchi hao, akieleza kuwa hamwelewi kwa kuwa wabunge akiwamo yeye, walishirikishwa vilivyo kwenye mradi huo na kulipwa posho lukuki.
Viongozi wa dini waliojitosa kwenye mgogoro huo ni Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Newala, Oscar Mnung’a na Askofu Mteule wa Kanisa la KKKT, Dayosisi Mpya ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbedule.
Kwa nyakati tofauti, viongozi hao wamepinga mradi wa kusafirisha nishati hiyo kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa hawaoni ni namna gani utawanufaisha wakazi wa Mtwara.
Askofu Mnung’a alisema anapingana na uamuzi wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na badala yake kuishauri Serikali ijenge mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara.
“Lazima wananchi wa Mtwara waamke, tumejifunza kule Songosongo, gesi imekwenda Dar es Salaam, si Kilwa wala Lindi iliyofaidika na gesi ile… gesi ibaki Mtwara, mikoa ya kusini iimarishwe,” alisema Askofu Mnung’a na kuongeza:
Wednesday, January 2, 2013
Marehemu Juma Kilowoko anatarajiwa kuzikwa ijumaa saa 5 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Wasanii wakiwa wamejitokeza katika msiba wa mwenzao.
Watu wakiwa msibani huku wakijadili mambo mbali mbali. Msiba wa Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' umewagusa wengi na kuleta simanzi. Marehemu Juma Kilowoko anatarajiwa kuzikwa ijumaa saa 5 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam

RAIS JAKAYA KIKWETE AMLILIA SAJUKI
Rais Jakaya Kikwete
Rais Dk. Jakaya Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha msanii maarufu wa kujitegemea hapa nchini, Juma Kilowoko maarufu kwa jina la kisanii la Sajuki, kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 Januari, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Enzi za uhai wake, Marehemu Juma Kilowoko alianza kujishughulisha na Tasnia ya Sanaa kwa kujiunga na kundi maarufu la sanaa la Kaole kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa msanii wa kujitegemea ambapo aliendelea kupata umaarufu katika tasnia ya michezo ya kuigiza na filamu na kufanikiwa kutengeneza filamu nyingi.
Baada ya kuanza kuugua mwaka 2010, Marehemu Kilowoko aliwahi kupatiwa matibabu nchini India mwaka 2011 na kurejea akiwa amepata nafuu kubwa kiasi cha kumwezesha kutengeneza filamu nyingine, lakini alianza kuugua tena hadi mauti yalipomkuta.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaam, leo, imemkariri Rais Kikwete akisema kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa mno na kifo cha Msanii Juma Kilowoko ambaye ametoa mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha sanaa hususan michezo ya kuigiza na filamu hapa nchini.
"Kwa hakika kifo cha msanii huyu ni pigo kubwa kwa Tasnia ya Michezo ya Kuigiza na Filamu ambayo inaendelea kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa Watanzania”, amesema Rais Kikwete katika Salamu hizo za Rambirambi.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, nakuomba wewe Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara unifikishie salamu zangu za rambirambi na pole nyingi kwa Familia ya Marehemu Juma Kilowoko kwa kuondokewa na Kiongozi na Baba wa Familia.
“Natambua uchungu ilio nao Familia ya Marehemu Kilowoko, lakini nawahakikishia kwamba binafsi niko pamoja nao katika kuomboleza kifo cha mpendwa wao. Nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi roho ya marehemu Juma Kilowoko, Amina”.
Aidha Rais Kikwete ametoa pole kwa wasanii wote nchini hususan wanaojishughulisha na masuala ya michezo ya kuigiza na filamu kwa kumpoteza mwenzao na hivyo kuleta simanzi na huzuni kubwa miongoni mwao. Hata hivyo amewataka kuwa wavumilivu na kuchukulia kifo hiki kama changamoto kwao katika kuendeleza tasnia ya michezo ya kuigiza na filamu hapa nchini.

WAOMBOLEZAJI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU SAJUKI TABATA BIMA
Waombolezaji mbalimbali wakiwemo waigizaji wa filamu nchini Bongo Movie wakiwasili Tabata Bima nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko SAJUKI aliyefariki leo asubuhi kwenye Hospitali ya Muhimbili wodi ya Mwaisela, ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu, bado taarifa rasmi za mazishi ya mwigizaji huyo hazijatolewa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Tutaendelea kuwaletea taarifa kadiri tutakavyozipata hapa ni baadhi ya picha mbalimbali ambazo kikosikazi cha fullshangweblog kimezinasa katika eneo la msiba.
WIZARA YA HABARI, VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO TANZANIA YATUMA SALAAM ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA SAJUKI
Marehemu Sajuki akiwa katika picha ya pamoja na mke wake Wastara, Wastara ni mmoja wa wanawake wanaostahili kuigwa kwani amepigania maisha ya mume wake mpaka dakika ya mwisho, kwa hili ni imani yangu kwamba mungu atasimama naye katika kipindi hiki kigumu kwake na familia yake mungu ampe nguvu na uvumilivu.
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.
Dkt. Mukangara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.
Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ .
Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk
Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.
Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.
Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen
Imetolewa na:
Mkurugenzi
Idara ya Habari(MAELEZO).
Dar es Salaam.
2 Januari 2013

PICHA ZA MAOMBOLEZI MSIBA WA SAJUKI NYUMBANI KWAKE TABBATA BIMA JIJINI DAR ES SALAAM
Mke wa marehemu, Juma Kilowoko 'Sajuki', Wastara Juma, akiwa na simanzi nzito kwa kumpoteza mumewe.
Baba mzazi wa marehemu, Juma Kilowoko 'Sajuki' akiwasiliana na ndugu na jamaa msibani hapo.…
Dada wa marehemu Sajuki akilia kwa uchungu.
Bibi wa marehemu Sajuki akiwasili msibani leo.
Pichani juu ni baadhi ya taswira za waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki', Tabata- Bima jijini Dar es Salaam. Sajuki amefariki dunia leo alfajiri akiwa katika hospitali ya taifa Muhimbili ambapo alikuwa akitibiwa.

Hotuba Ya Rais Kwa Taifa
Utangulizi
Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Ni furaha na faraja kubwa kuifikia siku hii adhimu ya kuuaga mwaka wa 2012 na kuukaribisha mwaka 2013. Ni jambo la bahati ambayo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuumaliza mwaka huu salama. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao wangependa kuiona siku hii lakini hawakujaaliwa. Wametangulia mbele ya haki. Tuendelee kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema. Amin. Nasi tumuombe Mola wetu atujaalie fanaka tele katika mwaka ujao.
Mapitio ya Mwaka 2012
Ndugu wananchi;
Mwaka tunaoumaliza leo ulikuwa wenye mambo mengi mazuri na mafanikio makubwa, lakini, pia, ulikuwa na changamoto zake. Baadhi zilikuwa ngumu na zipo zilizokuwa za kusikitisha na kuhuzunisha.
Ajali za barabarani na majini ziliendelea kupoteza maisha ya watu wengi na kusababisha majeraha na ulemavu kwa maelfu. Ajali mbaya kuliko zote kutokea, mwaka huu, ilikuwa ile ya meli ya MV Skagit iliyotokea tarehe 18 Julai, 2012 ambapo watu 144 walipoteza maisha. Ajali za barabarani zilizosababisha vifo nazo ziliongezeka kutoka 3,012 mwaka 2011 hadi kufikia 3,144 na kusababisha vifo vya ndugu zetu 3,714.

BREAKNG NEWS:MWIGIZAJI WA FILAMU SAJUKI AMEFARIKI DUNIA
Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

Subscribe to:
Posts (Atom)