Saturday, June 9, 2012

Picha za maonesho ya Karibu Fair 2012 yaliyofunguliwa na Naibu Waziri, Nyalandu
















Zifuatazo ni picha chache kati ya nyingi kutoka kwenye blogu ya tembeatz.blogspot.com zinazohusu maonesho hayo.Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu leo mchana amezindua rasmi maonesho makubwa ya sekta ya Utalii ya Karibu mjini Arusha. Baada ya kuwasili katika viwanja vya Maonesho, Nyalandu alipata wasaha wa kuzungumza na viongozi wa TTB, TATO pamoja na waandaji wa Karibu Fair 2012.
















Mhe Nyalandu akiteta jambo na mwenyekiti wa shirikisho la tour operators Tanzania, Mhe Mustapha Akunaay (kulia). Wengine ni Sam Diah mmoja wa waratibu wa maonesho sambamba na Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi wa Masoko wa TTB















Nyalandu akipata maelezo ya kampuni inayotoa huduma za helikopta hapa Tanzania ya Whirlwind. Anayempa Maelezo ni Capt. Neels ambaye alisema kampuni yake ipo mbioni kuleta helikopta 5 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Madhumuni ya mpango huo ni kuzitawanya katika maeneo mbalimbali ya nchi hii ili ziweze kutumika kwenye huduma za dharura haraka pale zinapohitajika. Sasa hivi wana helikopta moja nchini.


















Mojawapo ya sababu ya ziada ya kuzuru maonesho ya Karibu Fair 2012 mkoani Arusha katika Viwanja vya Magereza (karibu na Arusha Airport) ni kujionea hema la gorofa. Hema hili hutumika kwa malazi ya wageni wanapokuwa porini, hususan kwa wanaopenda kuweka kambi na kuacha kulala kwenye mahoteli. Moja ya makampuni yanayoshiriki Karibu Fair 2012 imeamua kuwaonyesha wageni na wadau bidhaa hii. Hema hili linahamishika.


















Kampuni inayotoa huduma za helikopta hapa nchini ya "Whirlwind: aviation inayoshiriki maonesho ya karibu fair ilifanya safari ya dakika kumi kuuzunguka uwanja wa maonesho, na KK wa blogu ya TembeaTz alikuwa ni mmoja wa abiria wa safari hiyo.