Thursday, March 7, 2013

KAULI YA KAMANDA KOVA...............

Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu! Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi    Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu
 chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo lililotokea jana,

MAAFANDE WAHUSISHWA NA TUKIO LA UTEKAJI WA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSALOM KIBANDA HII NI KAULI YA ABSALOM KIBANDA BAADA YA KUTEKWA...............

"Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na

kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza kunishambulia.

Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia mwenzake

afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu 'kushuti'

(kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.

“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la

kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia,

walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi

waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye

majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa..."

MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA: MFUMO WA ELEKRONIKI UMEKWAMA....ZOEZI LINAANZA UPYA

 Huku Wakenya wakiendela kusubiri kwa hamu kubwa kumjua mshindi wa kura ya urais kufuatia uchaguzi wa Jumatatu, wasiwasi unaongezeka baada ya kukwama kwa mfumo wa uwasilishaji matokeo kwa njia ya elekroniki.

Kufuatia hitilafu hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imesema kwamba inategemea sasa matokeo yatakayowasilishwa na wasimamizi wa uchaguzi kutoka majimbo yote 290 kote nchini ili kuanza upya shughuli ya kujumlisha kura za urais.

BARUA YA MWANAFUNZI ALIEMALIZA FORM 4 2012 KWA WIZARA YA ELIMU

 Pliz my name is MKUWA RAJAB I am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don’t like me.

 I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put ...majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to O.

Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama. Ze gavament shud change my marks to dishen 2, because the youth are ze future of my country.

 If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more maks becoz of ze future. Pliz mzee put on ze yua fb wall so ze Plezident will see.......

Kwa hisani ya James Pricenton Brighton

TFF YASALIMU AMRI YA SERIKALI...UCHAGUZI UTARUDIWA UPYA

Serikali imelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuandaa upya mchakato wa uchaguzi wake mkuu uliolalamikiwa na wadau mbalimbali wa soka nchini, kiasi cha wengine kufungua kesi mahakamani kuupinga.

TFF imeshitakiwa mahakama za Mwanza na Tanga, baada ya baadhi waliokuwa wagombea wa nafasi mbalimba kuenguliwa kwenda kortini kupinga kufanyika uchaguzi huo mpaka kesi zao za msingi zitakaposilizwa.

Kabla ya mchakato huo, TFF pia imetakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya katiba kabla ya Aprili 15, na baada ya hapo kuitisha pia Mkutano wa Uchaguzi kabla ya Mei 25 mwaka huu.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA URAIS KENYA KWA MUDA HUU

 Hadi kufikia muda huu, Kenyatta anaonekana kuongoza kinyang'anyiro hicho.Matokeo kamili yanatariwa kutangazwa kesho.

Wakati huo huo tume ya uchaguzi nchini humo (IEBC) ilikiri kuwa mitambo yake ya kuhesabu kura kwa njia ya kisasa ilishindwa kuhimili vishindo vya zoezi hilo na kulazimika kuhamia kwenye mfumo wa zamani (manual) wa kuhesabu kura.

Magazeti ya leo Alhamisi ya 7th March 2013






MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI "ABSALOM KIBANDA" APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahahariri na Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd,Absalon Kibanda akipakiwa kwenye ndege ya Kampuni ya Flightlink tayari kwa safari ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa Matibabu baada ya kuvamiwa  na watu wasiojulikana na kujeruhiwa vibaya,alipokuwa akirudi nyumbani kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.