SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kutangaza safu mpya ya wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho, wasomi, wanasiasa na viongozi wa dini wameponda uteuzi huo wakisema chama hicho tawala, kisitarajie jipya kutoka katika safu hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, wadau hao walisema viongozi walioteuliwa wana upungufu, hivyo hawawezi kuwajibishana kwa kuwa wanaogopa kuumbuana.
Katika uteuzi huo Kikwete aliwateua, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM, akisaidiwa na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba upande wa Bara na Vuai Ali Vuai upande wa Zanzibar.
Wengine ni Zakhia Meghji aliyeteuliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha, Mohamed Seif Khatib (Oganaizesheni), Dk Rose Migiro (Kimataifa) na Nape Nnauye (Uenezi).
Uteuzi huo ulitanguliwa na uchaguzi ambao ulimrejesha Kikwete kuwa Mwenyekiti wa chama wa Taifa akisaidiwa na Philip Mangula (Tanzania Bara) na Dk Ali Mohamed Shein (Zanzibar).
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanawatizama Mangula na Kinana kama viongozi makini, lakini wasioweza kumudu kasi ya siasa za sasa ambazo zimebadilika kulingana na wakati na aina ya ushindani kutoka upinzani.
Kadhalika wanakiona kikosi hicho kuwa hakiwezi kuisaidia CCM kupambana na rushwa, ambayo inaonekana kuota mizizi kiasi cha kuonekana kama sehemu ya utamaduni wa chama hicho.
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini alisema safu hiyo ya uongozi haina jipya akifafanua kuwa, tatizo kubwa la chama hicho ni mfumo wake wa utendaji kazi.
“Ni mfumo ambao wamejiwekea wa kulindana, hivyo uongozi huu hautaleta mabadiliko yoyote CCM,” alisema Kilaini.
Alisema viongozi waliochaguliwa hawatakuwa na sauti kwa kuwa nao wana udhaifu wao hivyo hawawezi kuwachukulia hatua wenzao kwa kuwa nao wataumbuliwa.
Askofu Kilaini alisema viongozi hao wataendeleza mfumo walioukuta na hakuna atakayeweza kumkosoa mwenzake aliyefanya makosa.
“Kati ya viongozi wa CCM waliochaguliwa hakuna atakayemnyooshea mwenzake kidole kwamba amefanya kosa fulani, ni vigumu mno kumwadhibu mwenzake kwa kuhofia kuwa, kwa vile yeye pia ni dhaifu akimwadhibu huyo matendo yake yatagundulika,” alisema.
Alisema licha ya Rais Kikwete kukemea rushwa kwa viongozi wote waliochaguliwa, lakini hakuna hatua yeyote aliyochukuwa kwa wale waliotuhumiwa kujihusisha na vitendo hivyo wakati wa chaguzi za ndani ya CCM.
“Rais wetu anazungumzia rushwa na kukemea lakini hakuna aliyemchukulia hatua yoyote kwa wale waliokutwa wakitoa rushwa katika uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi na Ujumbe wa Halmashauri Kuu (Nec),” alisema Kilaini.
Kauli za wasomi
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo alisema Watanzania wasitegemee mabadiliko katika safu mpya ya uongozi ya CCM kwa kuwa walioteuliwa hawana jipya.
Friday, November 16, 2012
RAIS KIKWETE AWASILI ARUSHA, VIONGOZI WA DINI WAMPONGEZA NA KUMUOMBEA MAFANIKIO ZAIDI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana jioni Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro jana Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha.
(PICHA NA IKULU)
Subscribe to:
Posts (Atom)