Tuesday, June 18, 2013

Serikali imezuia mazishi ya waliouwawa kwa bomu arusha, polisi wanafukuza watu

Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo.

    Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha.

    Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

Habari isiyo rasmi AICC Imekataa uwanja wa soweto kutumika kuaga miili ya marehemu

Kuna taarifa zilizopo ni kwamba AICC ambao ni wamiliki wa uwanja wa soweto wameshinikizwa na serikali ya CCM kuzuia CHADEMA kutumia uwanja kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu! Huu ni unyanyasaji mwingine wa serikali ya CCM dhidi ya wananchi wa nchi hii.Ndiyo maana polisi wamejazana hapa kulinda uwanja usitumiwe na CHADEMA! Ikumbukwe kuwa AICC ni taasisi ya umma, ambayo pia inaendeshwa kwa kodi za wa Tanzania pamoja na kuwa ni shirika la umma. Muda huu nisiseme mengi kwani tunasubiria viongozi wetu pamoja na wabunge wapo kwenye mazungumzo!

Hati tete mjini Arusha Mabomu kila kona


Kufuatia mlipuko wa bomu lililorushwa tarehe kumi na tano kwenye mkutano wa chadema na kuuwa na kujerua leo hii mabumu yametawala kila kona kuwatawanyisha wafuasi wa chadema waliukua wakiomboleza misiba katika uwanjwa wa soweto. tunaendelea kuwaletea habari na picha za matukio.

Magazeti ya leo Jumanne ya 18th June 2013





"MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA ULIPANGWA NA CHADEMA WENYEWE".....NAPE NNAUYE

 Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22) -kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.

Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.

Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka.

KAULI YA SERIKALI KUHUSU KITITA CHA MILIONI 100 KWA MTU ATAKAYEMTAJA MTU ALIYERUSHA BOMU ARUSHA

 Zifuatazo ni nukuu za maneno yaliyotolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, sera, uratibu na bunge William Lukuvi kuhusu hilo bomu ambalo lililipuliwa kwenye mkutano cha Chadema Arusha.

“Mtu asiejulikana alirusha kitu katika kundi la watu kilichosababisha mlipuko mkubwa, mkutano huu ulikua na ulinzi wa jeshi la Polisi wakiwa na magari mawili… askari walisimama upande wa Kaskazini ya uwanja ambapo mrushaji alikua mashariki na alirusha bomu kuelekea Magharibi”

“Jaribio la Askari Polisi kutaka kumfata alierusha lilizuiwa na makundi ya Wananchi ambao walianza kuwashambulia polisi kwa mawe na kuwazomea na hivyo Polisi kulazimika kuanza kujiokoa badala ya kumsaka Muhalifu”

PICHA ZA MAZISHI YA MSANII LANGA KILEO