Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri
wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal ambaye pia ni mwanamuziki maarufu
duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo ,
Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini
Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini
mwake.
Saturday, February 9, 2013
Miss Utalii Tanzania 2013 kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii
Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Mtwara,Lindi na Pwani. Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari,maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa, uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere Air Port, Soko la Kariakoo, Mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.
JK atua msumbiji Jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi jumuiya ya Maendeleo
ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Maputo.Rais Kikwete yupo nchini Msumbiji kuhudhuria
mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
YALIYOJIRI BUNGENI
Mh Kigwangalla alimalizia kwa kusema “naomba atumie uungwana yeye
mwenyewe kusimama katika bunge hili.. aidha kuwaomba radhi Watanzania
kwa kudanganya ama kutimiza wajibu aliousema hapa yeye mwenyewe wa
kujiuzulu, uongo aliousema ni mkubwa sana.. naomba nitoe hoja kwamba Mh
Mbatia aadhibiwe kwa mujibu wa kanuni ya 63, asihudhurie vikao
visivyozidi 20 na aombe radhi kwa maandishi kwa Watanzania kwa kusema
uongo bungeni”
Subscribe to:
Posts (Atom)