Monday, June 3, 2013

HUTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JUNE 3, 2013

 HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJI JOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE, DAR ES SALAAM.


UTANGULIZI

Ndugu Wananchi,

Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii ya leo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfa hii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.

Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwa mabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu wa Kifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewa miezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayo ilikuwa Mei 2, 2012.

Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyo Tume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitano kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga. Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.

ALBERT MANGWEA AAGWA NA WATANZANIA WALIOKO AFRIKA KUSINI.....MWILI WAKE UTALETWA KESHO SAA NANE

 Watanzania waishio nchini South Africa wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa Albert Ngwea kuelekea katika safari ya mwisho wakiongozwa na Msanii Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru, Kinjeketile wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini Afrika kusini...
Mwili  wa  marehemu  utaletwa Tanzania  kesho  saa  nane.....

MSHIRIKI WA TANZANIA ( FEZA KESSY) KATIKA BIG BROTHER YUKO HATARINI KUTOLEWA...KURA ZAKO ZINAHITAJIKA

Kama hisia za wengi zilivyokuwa kuhusiana na Betty kulipiza kisasi, mambo yameenda hivyo..Betty ambaye ni Head of House wa Diamond house amemuokoa Bolt na kumuweka kikaangoni Feza..Katika Ruby house, Selly ambaye ni Head of house huko, naye ametumia ukuu wake wa kaya kumuokoa Biguesas na kumtia kitanzini Koketso..Wiki hii Feza, Dillish, Hakeem, LK4 na Koketso wako kikaangoni..Wakati wa kupiga kura kwa nguvu zote umewadia.. Kazi kwetu watanzania kumpigia kura wakwetu..Tuwahimize pia marafiki zetu Africa kumpigia kura Feza kwani kura zao ni muhimu sana.. -- Kila nchi inahesabiwa kama kura moja.

Kupiga kura tembelea --> http://bigbrotherafrica.dstv.com/vote/

NEYMAR ATUA RASMI BARCELONA

 Klabu ya Barcelona imemtambulisha rasmi mshambuliaji wake mpya, Neymar da Silva Santos Júnior 'Neymar' klabuni hapo kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuanza kuitumikia timu hiyo. Pichani juu ni baadhi ya taswira za mchezaji huyo akiwasili klabuni hapo.

GARI LA WEMA NYANG’ANYANG’A

GARI la Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ limepata ajali na kuwa nyang’anyang’a huku dereva aliyekuwa akiliendesha akiumia vibaya.


Gari la Wema kwa ndani baada ya ajali hiyo.

Habari zilisema kuwa ajali hiyo ilitokea maeneo ya Morocco, Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo dereva huyo ambaye inadaiwa ni ‘jamaa wa Wema’ aliyetajwa kwa jina moja la Robby aliumia mguu wa kushoto na taya hivyo kukimbizwa hospitali (jina halikupatikana mara moja).

KAMATI YA NGWEA YAKUSANYA MILIONI 32....MAMA MZAZI APANDWA NA PRESHA BAADA YA MWILI WA NGWEA KUZUIWA HUKO AFRIKA KUSINI

KAMATI ya Mazishi ya aliyekuwa Msanii wa Bongo Fleva, Albert Mangwea ‘Ngwea’, mpaka jana mchana ilikuwa imekusanya jumla ya Sh milioni 32 kutoka kwa wadau mbalimbali.

Kamati hiyo inahitaji Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu kutoka Afrika Kusini mpaka Morogoro kwa ajili ya mazishi. Fedha hizo pia zinahitajika kwa ajili ya kuratibu shughuli nzima ya mazishi.

Mangwea alifariki dunia Jumanne iliyopita nchini Afrika Kusini akiwa usingizini kwa madai ya kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya.

Alitarajiwa kuwasili nchini jana lakini kushindwa kutoka kwa ripoti ya uchunguzi wa madaktari kwa wakati, kumesababisha isijulikane atatua lini, licha ya kudaiwa kuwa anaweza kutua leo.

Kamati ya Mazishi bado inaendelea na mchakato wa kuratibu shughuli hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu akiwa Mbezi Goig jijini Dar ambako ndiko kwenye msiba huo, mmoja wa waweka hazina wa kamati hiyo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, alisema mpaka sasa kamati yake imefikisha Sh 32,259,000 ingawa wanatarajia kuendelea kupokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau.

Miongoni mwa watu wa kwanza kutoa michango yao katika msiba huo ni P-Funk aliyetoa Sh milioni tano, Clouds Media Group (Sh milioni tano) na Push Mobile (Sh milioni tano).

Juzi Kampuni ya Global Publishers ilitoa Sh milioni moja.
“Nawasisitiza Watanzania waendelee kutoa michango yao kwa ndugu yao ili kuonyesha umoja tulionao. Fedha zikiwa nyingi tunataka kumfanyia kitu mama yake ili kuendelea kumfariji kwani kipindi hiki ni kigumu kwake,” alisema P-Funk.

Wakati huohuo jana  taarifa zilisema mama mzazi wa Mangwea aishie Morogoro, Denisia Mangwea, alipandwa na presha baada ya jana kupata taarifa kuwa mwili wa mwanaye umezuiwa Afrika Kusini kutokana na uchunguzi wa madawa ya kulevya. Alikimbizwa hospitali na inadaiwa anaendelea vizuri.

Mangwea aliwahi kutamba na nyimbo kadhaa kali zikiwemo Gheto Langu, She Got a Gwan, Mikasi na Tupo Juu.