Thursday, May 16, 2013

Rais kikwete azindua kampeni ya lishe


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua   kitabu cha kampeni ya Lishe Tanzania baada ya kukizindua leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe Peniel Lyimo akifuatiwa na Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi ya Chakula na Lishe Mzee Lema. Kushoto ni Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mama Maria Nyerere
 Mama Maria Nyerere akifurahia tuzo maalumu aliyopokea kwa niaba ya Baba wa Taifa aliyotunukiwa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa mchango wake mkubwa kwa kukuza na kuendeleza sera ya lishe nchini wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya Lishe Tanzania leo Machi 16, 2013 katika bustani ya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Wadau wa utalii wakutana arusha

Wadau wa utalii kutoka halmashauri ya Wilaya ya Longido wamekutana leo hii katika mkutano wa Siku Mbili wenye lengo kuu la kuthamini na kutambua mchango wa Rasilamali zinazo wazunguka wafugaji wa halimashauri hiyo katika kujiletea uchumi kwa njia nyingine tofauti na ile iliyozoeleka.

Mkutano huo wa Wadau hao wa Utalii kutokandani ya Halimashauri ya Wilaya ya Longido ambao ulifunguliwa na Afisa wa Mazingira ya Ikolojia kutoka

mamlaka ya Hifadhi za Taifa Bwana  Alibert Mziray ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kujua jinsi ya kutumia Rasilimali zilizopo hasa hasa kwa Wafugaji hao wa Loliondo.

Magazeti ya leo Alhamis ya 16th May 2013




MWANA FA AVUNA MILIONI 18 NDANI YA MIEZI MITATU KWENYE RINGBACK TONE

Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.

Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.

Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.

DR. SLAA AMKIMBIA NAPE NNAUYE KATIKA OFISI ZA ITV

Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.

Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.

Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.