Thursday, April 4, 2013

CCM YAKANUSHA JITEGEMEE KUINGIA MKATABA TPA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, 2013, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana Aprili 3, 2013, mmoja wa Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema alitoa tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa kupitia kampuni ya Chama ya Jitegemee Trading Company, CCM imeingia mkataba na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kwenye mradi wa upanuzi wa Bandari kavu kwa kutumia eneo la SUKITA lililopo maeneo ya makutano ya barabara ya Kawawa na Mandela ambalo ni mali ya CCM.

HATIMAYE WAKILI NYAGA MAWALLA AMEZIKWA NAIROBI

                                        DEATH AND FUNERAL ANNOUNCEMENT
Familia ya Wakili Nyaga Mawalla imeridhia ndugu yao azikwe jijini Nairobi, Kenya na kumaliza mvutano wa suala la mazishi ya wakili huyo.Mawalla alifariki dunia jijini Nairobi baada ya kuanguka kutoka kwenye ghorofa katika hospitali alikokuwa akitibiwa Machi 23, mwaka huu.

Hata hivyo, kulizuka mvutano wa mazishi yake baada ya Wakili Fatuma Karume kupeleka wasia wa marehamu uliokuwa umeelekeza kuwa ikitokea amefia nje ya nchi azikwe huko au akifia ndani ya nchini basi azikwe kwenye shamba la Momella, Arusha wakati wazazi wake walitaka azikwe kwao Marangu mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana msemaji wa familia hiyo, Joseph Nuwamanya alisema wameamua kuheshimu wasia wa marehemu.

Jaji Mstaafu Ernest Mwipopo Amefariki Dunia

JAJI MSTAAFU ERNEST MWIPOPO AMEFARIKI DUNIA JANA ALASIRI KWA AJALI YA GARI MKOANI MOROGORO: TAARIFA ZAIDI TUTAZIWEKA HUMU KADRI TUKAVYOZIPOKEA.

Yaliyojiri leo Magazetini Alhamisi ya 4th April 2013





WATUHUMIWA 11 WA GHOROFA LILILOANGUKA DAR WAFIKISHWA MAHAKAMANI...

 Mtuhumiwa namba moja wa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia Raza Hussein Ladha (aliyevaa kanzu nyeupe) na watuhumiwa wenzake 10, wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

 HABARI  2  MUHIMU:

    Hakimu aagiza mtuhumiwa wa wa mauaji ya padre Evaristus Mushi

Hakimu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Isaac Sepetu, ameagiza mtuhumiwa Omar Yusuf Makame wa mauaji ya Padre Evaristus Mushi afikishwe mahakamani mara moja siku ya Jumatatu wiki ijayo, ikiwa ni pamoja na nyaraka zinazoeleza ni kwa nini hakupandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka ndani ya saa 24 kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 390 cha mwenendo wa makosa ya jinai, sura na. 7 ya mwaka 2004. Maombi ya kufikishwa mahaknani yametoka kwenye jopo la mawakili watetezi wa mtuhumiwa.

    Watuhumiwa wa jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Gandhi, Dar, wafikishwa mahakamani

PICHA ZA MATUKIO YA VURUGU HUKO TUNDUMA......DIWANI ( CHADEMA ) NA MCHUNGAJI KKKT WANASAKWA NA POLISI



Happy Birthday to Me Mama wa Asilialive

Asante Mwenyekiti wangu Kwa jiugonjwaaa la ukweli nikitoka job tunasababisha