Friday, November 23, 2012

Mkewe Gbagbo Kufikishwa The Hague

Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.

Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.

Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa urais.

Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya rais.Anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka mengine mjini Abidjan.

Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumeo kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC. Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.

Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63, walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya.Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka huko the Haque.

Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Mahakama Yaamuru Madiwani Watano Kuilipa Chadema Sh15 Milioni

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru madiwani watano waliotimuliwa Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo jana baada ya Chadema kushinda kesi hiyo.Hakimu Magesa alisema madiwani hao wanapaswa kulipa Sh15 milioni ndani ya miezi miwili, wakishindwa watapelekwa gerezani.

Madiwani hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu.

Pia, katika kesi hiyo ya madai Chadema walikuwa wakiwakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, wakati wadaiwa hao walikuwa wakijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa wakili wao kujitoa.Akisoma uamuzi huo, Hakimu Magesa alisema baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, imeona wadaiwa hao wanapaswa kulipa zaidi ya Sh15.1 milioni, kila mmoja anatakiwa kulipa zaidi ya Sh3.2 milioni katika kipindi kisichozidi miezi miwili.

Awali, kulikuwa na mvutano kati ya wadaiwa hao jambo lililosababisha kesi hiyo kusikilizwa kwa kipindi kirefu ambapo walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu ya kutokupelekwa gerezani, huku kila mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho angeweza kulipa kwa mwezi.

Kwa upande wake, Ngowi alisema ana uwezo wa kulipa Sh25,000 kwa mwezi, Mpanda Sh20,000, Mallah Sh20,000, Rehema Sh15,000 na Bayo Sh15,000 kwa mwezi bila kuonyesha mchanganuo wa kipato chao, jambo lililopingwa vikali na Wakili Kimomogoro kwamba kiwango hicho ni kidogo.

Hakimu Magesa alisema kisheria mtu akishinda kesi ana uwezo wa kuchagua hukumu ya kulipwa kwa kuchukua mali za mdaiwa au mlalamikiwa kupelekwa kifungoni.

“Kimsingi mtu anaposhinda kesi lazima alipwe gharama aliyotumia na iwapo mahakama itaridhia alipwe kwa kiwango hicho, itachukua muda mrefu kati ya miaka 10 na 16 kumaliza deni hilo, jambo litakalosababisha aliyeshinda kushindwa kuona matunda ya ushindi wake,” alisema Magesa.

Alisema fedha hizo wanapaswa kuzilipa mara mbili,  awamu ya kwanza inatakiwa kila mmoja kulipa zaidi ya Sh1.5 milioni na  wawe wamemaliza kwa miezi miwili na kwamba, iwapo watashindwa mdai anaweza kupeleka mchanganuo wa gharama za kumtunza mfungwa na mahakama kuupitia na baadaye kutoa amri wapelekwe gerezani

 Na:Na Mussa Juma

Majambazi Yafariki Kabla Ya Kufikishwa Hospitali

 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la Polisi na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali leo asubuhi




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia leo asubuhi (Picha na Mahmoud AhmadArusha                                                  

Mbeki Alia Mabilioni Yaliyofichwa Nje

RAIS Mtaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amesema Bara la Afrika linapaswa kudhibiti utoroshaji wa rasilimali zake kwenda nje ya bara hilo, kwani ni moja ya sababu za maisha ya watu wake kuendelea kuwa duni.

Rais Mbeki alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa rasilimali zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 50 hutoroshwa kila mwaka kutoka nchi za Afrika na kwenda kuwanufaisha watu wengine nje ya bara hilo.

“Taarifa zinaonyesha kuwa rasilimali zenye thamani zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 50 hutoroshwa kila mwaka kwenda nje ya Afrika, lakini kwa mtizamo wangu mimi ni kwamba thamani halisi inaweza kuwa hata mara mbili (Dola za Kimarekani Bilioni 100) kwa mwaka,”alisema Mbeki.

Mbeki alikuwa akizungumza kwenye mjadala kuhusu “uongozi wenye malengo kwa ajili ya mabadiliko ya Afrika” ulioandaliwa kwa pamoja baina ya taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) ya hapa nchini na Mbeki Faoundation ya Afirka Kusini.
Kiongozi huyo alisema utoroshaji wa rasilimali hizo ni matokeo ya udhahifu katika usimamizi wake, na kwamba lazima Serikali za Afrika zichukue hatua kudhibiti utoroshaji huo.

Kauli ya Mbeki imekuja wakati Tanzania ikiwa katika mjadala mkali kuhusu taarifa kwamba baadhi ya vigogo wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, hivyo kuwapo shinikizo la kutaka wahusika watajwe na fedha hizo zirejeshwe nchini.
Taarifa hizo ziliibuliwa na mapema mwaka huu na baadhi ya vyombo vya habari likiwamo Gazeti hili na baadaye ilibainika kwamba fedha hizo ni mali ya Watanzania 27 wakiwemo wanasiasa na wafanyabiashara. Gazeti hili pia lilibaini kwamba mmoja wa walioficha fedha hizo anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Katika uchunguzi wake, Mwananchi imebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (Karibu Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa Dola ya Marekani.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni).

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa

Kinana Ashtukiza Ziara Tabora

                           Kinana akimsalimia Fatma Mwasa, Wengine, Nape, Khatib na Mwanri.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia viongozi wa mkoa wa Tabora alipotua kwa muda mkoani humo akiwa akitoka Rukwa kwenda Geita leo
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akipotua kwa muda mkoani humo akiwa akitoka Rukwa kwenda Geita Leo

Waziri Wa Habari Afungua Kikao Kazi Cha Sekta Ya Utamaduni....






















Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Kikao Kazi cha tisa cha  Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini  (hawapo Pichani).Kikao hicho kilifanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kauli mbiu ilikuwa ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe Chachu ya Maendeleo

























                                             








Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
                                             
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa  Kikao kazi cha tisa cha Sekta  ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaa.
                                               
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akisisitiza jambo kwa katika Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko
                                 
Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM

JK. Apokea Cheti Chake Cha Udaktari Wa MUHAS


 Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam

                                       
     Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.                                  
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.                              Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Ardhi Prof Anna Tibaijuka, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi na viongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili baada ya kukabidhiwa Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.

PICHA ZOTE NA IKULU

Magazeti ya leo Ijumaa 23rd November 2012