Friday, April 12, 2013

Magazeti ya leo Ijumaa ya 12th April 2013

             


RIPOTI KUHUSU WATOTO WA NELSON MANDELA KUGOMBANIA MALI

 Zenani ndio huyu wa nyumba ya Mzee Mandela, hawa wengine ni wajukuu na vitukuu wa Mandela.

 BBC wameandika kwamba watoto wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela Makaziwe na Zenani Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki  wakidai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1

Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ambae aliondoka hospitali baada ya kutibiwa mapafu akiwa tayari kalazwa hospitali mara nne katika kipindi cha miaka miwili.

WEMA WEPETU AMFIKISHA POLISI MAMA YAKE BAADA YA KUMFANYIA VURUGU NYUMBANI

 NI kivumbi! Kuna madai kwamba, staa wa Bongo asiyechuja, Wema Sepetu amemfikisha mama yake, Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani mbalimbali...

Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilijiri usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,” kilisema chanzo.

Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

TATIZO LA ELIMU TANZANIA SIYO VIBOKO.....BORESHENI MIUNDO MBINU KWANZA BADALA YA KUFIKIRIA KUTEMBEZA VIBOKO

 Taifa liko katika wakati mgumu juu mustakabali wa sekta ya elimu kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili.  Kuna mengi yanazungumzwa, yamependekezwa na mengine bado yanaendelea kutolewa juu ya njia sahihi ya kukoa elimu ya watu wa taifa hili.

Kuna hoja zinatolewa kwamba sekta ya elimu imeachwa kuporomoka hadi kufikia hali mbaya ya sasa kutokana na kuminywa kwa bajeti ya sekta hiyo, matokeo yake ni janga la kufeli kwa wananfunzi wengi katika mitihani yao kama ilivyodhihirika kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza elimu ya sekondari mwaka jana kwa zaidi ya asilimia 60 kupata daraja sifuri.

HAKUNA SHERIA INAYOMLAZIMISHA MTU KUPIMA UKIMWI ILI AFUNGE NDOA AU APATIWE AJIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul habib Fereji

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema suala la kupima Ukimwi ni la hiari kwa hivyo hakuna mwananchi wala mgeni atakayelazimishwa kufanya hivyo endapo akitaka kufunga ndoa au akipatiwa ajira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Fatma Abdul habib Fereji aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe ( CUF) Salim Abdalla Hamad aliyetaka kujuwa kwa nini Serikali isipime afya za wananchi kwa lazima kujuwa kama wapo salama na ugonjwa wa Ukimwi.Fereji alisema Zazibar hakuna sheria inayoilazimisha Serikali kuwapima wananchi afya zao kwa lazima kuhusu ugonjwa wa Ukimwi na kwa kuwa hilo ni suali la mtu binafsi serikali yake ni kutoa elimu na kuwahamasisha wapime afya zao lakini sio kuwalazimisha.