Sunday, August 19, 2012

GODLOVE MULIAHELA‏ : MWANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA TANZANIA AISHIYE UJERUMANI

                Godlove Muliahela akifanya 'shooting' ya wimbo wake ambao utatoka hivi karibuni.
                     Ilikuwa ni wakati wa mapumziko hapa akiwa pamoja na 'producers' wake.
                                Kazi ya kuendelea kurekodi wimbo wake ikiendelea.
Akiwa pamoja na Mpiga picha wake wa video.

                                           ..akiwa pamoja na kwaya yake huko Ujerumani.

Kwa Taarifa zake zaidi Tembelea Website yake hapa http://www.god-love.de/

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA PREMIER LEAGUE NA PRIMERA DIVISION PAMOJA NA WAFUNGAJI WAKE AUG 19, CHELSEA NA MAN CITY.









'Baby J' ahamishia MABEGI Dar!


Toka kisiwani Zenji,  mwanadada anayefanya vyema kwasasa kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya Baby J, ameamua kuhamishia makazi yake  jijini Dar,  huku akielezea sababu ya kufanya hivyo ni kutafuta soko zuri la muzuki wake.

Kauli ya msanii huyo inaweza kuwa sawa na mwezake AT, ambaye amehamia rasmi dar kwa kufuata soko analoamini kuwa ni bora.

Hata hivyo Baby J alisema haoni sababu ya kutowashukuru mashabiki wake wa Visiwani na Bara kwa kumpa sapoti katika kila wimbo ambao amekuwa akitoa.

“Dar nimekuja kufanya muziki na kuchukua nafasi hivyo naamini sapoti kubwa ninayopata kutoka mashabiki ndiyo inayonipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi hivyo nawaahidi wale wote wanaopenda kazi zangu ni kwamba sitawaangusha kabisa,” aliongeza.

Mpinzani wa Wolper huyoo


Jasmin alisema kwamba toka anaanze kuigiza filamu zote, watayarishaji wamekuwa wakimkubali nakusema kwamba yeye uwezo wake ni mkubwa na anaweza kabisa kumpoteza Jacqueline Wolper.

Alisema Wolper ni mmoja kati ya wasanii wanaomvutia sana, yeye  na wasanii wengine kama Monalisa na Msanii Johari kwani hiyo yote ni kutokana na kupitia kazi zao.

Mbali na hilo alisema kwamba haofii ushindani, bali siku ya siku anatarajia kukimbiza wasanii wenzake kwenye sanaa ya Filamu hapa nchini.

Si mwingine bali ni yule Mwigizaji wa kike anayekuja wka kasi ya ajabu kwenye sanaa ya Filamu Swahiliwood Neema Oberlin Kimaro ‘Jasmin’, huenda akawa tishio kwa msanii anayeng'ara kwa sasa kwenye sanaa ya Filamu ambaye ni Jaqueline Wolper Massawe.

Mbali ya kuwa ni msanii anayetoka Mkoani Kilimanjaro anakotoka mpinzani wake Jack, kwa muda mfupi sasa toka aingie kwenye sanaa hiyo ya Filamu  ameonyesha uwezo mkubwa baada ya kushiriki kwenye Filamu ya Essau Hellen akiwa mhusika mkuu katika filamu hiyo.

Mara  nyingi  vipaji vya wasanii vimekuwa vikiibuliwa, lakini msanii huyu ameonyesha uwezo wa hali ya juu sana kwenye Filamu ya Essau Hellen na amecheza kama mhusika mkuu akiigiza kwa kutumia jina la Jasmin nafasi ambayo imechezwa na wahusika wawili yeye na msanii mkongwe Grace Mapunda (Mama Kawele).

Ofisi ya madame Rita yateketea kwa moto


Ijumaa ya August 17 2012 na ijumaa nyingine kabla ya hii ya August 17 zimekua siku mbaya kwa Madame Rita Paulsen Big boss wa Benchmark Production ambayo ndio muandaji wa mashindano ya Bongo star search.

August 17 shoti ya umeme imemsababishia hasara sio chini ya milioni hamsini za kitanzania baada ya nyumba iliyokua inatumika kama stoo ya vifaa vya production Benchmark kuteketea yote kwa moto pamoja na vitu vilivyokuwemo ndani.

Madame amesema shoti ya umeme ilitokana na transfoma ambayo ipo karibu na ofisi yao Kawe Dar es salaam ambapo ofisi yote ilikua iungue ila shoti ilipofika kwenye ofisi kubwa umeme ulijizima wenyewe kutokana na vifaa kifaa maalum kinachoweza kuzuia shoti, hivyo nyumba ndogo ya stoo iliyokua na vifaa vya productions vilivyokua vinatumika kwa miaka kumi Benchmark production ndio ikateketea.

Tanesco wamethibitisha kweli kwamba ajali ya moto imetokana na shoti ya umeme ambapo zimamoto walichelewa kufika kwenye eneo la tukio kwa zaidi ya saa moja na nusu huku wakisema foleni barabarani ndio iliyosababisha, hakukua na njia ya kuuzima huo moto hivyo Madame Rita na timu yake walibaki wakitazama tu nyumba ikiteketea.

Nilipomuuliza Madame kuhusu msg niliyotumiwa ya uwezekano wa BSS kusimamishwa kutokana na hiyo ajali ya moto, namkariri akisema “nahisi huyo jamaa labda alikua anataka hivyo lakini BSS haiwezi kusimama kuruka hata siku moja, hata nikifariki”


Madame Rita. Amesema anategemea wenye nyumba hiyo watakua wana insurance.

Kuhusu tukio la ijumaa iliyopita kabla ya hii ya August 17, Madame Rita amesema “wezi waliniibia begi langu lenye vitu vingi vya thamani, shilingi milioni tatu pamoja na kadi za benki, vitambulisho na funguo za gari Mercedes Benz ambayo mpaka sasa haliwezi kuwaka kwa sababu ufunguo ndio nilikua nao huo huo wa spea hivyo ilibidi libebwe mpaka nyumbani, walinipokonya wakati nimesimama nazungumza na mtu”

Madame alisha ripoti polisi lakini mpaka sasa hajapata chochote kati ya vilivyoibiwa, ameomba yeyote anaehusika arudishe tu hizo funguo hata kwenye ofisi za Clouds Fm mikocheni, aweke kwenye bahasha na hata akiandika Millard Ayo zitamfikia kwa sababu anashindwa kulitumia gari sasa hivi na inambidi aagize funguo mwingine kwenye kampuni ya Benz Ujerumani kitu ambacho kitatumia muda mrefu.
Chanzo:Millard Ayo.com

Magazeti ya leo Jumapili 19th August 2012





















MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA PREMIER LEAGUE NA WAFUNGAJI WAKE AUG 18 2012.








Rais Jakaya Mrisho kikwete Awasili Kutokea Msumbiji

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema baada ya kuwasili  usiku huu Agosti 19, 2012 kutoka Maputo, Msumbiji alikohudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe Agosti 17,  2021 na kumalizika jana jioni  Agosti  18 2012. Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola. Nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema baada ya kuwasili  usiku huu Agosti 19, 2012 kutoka Maputo, Msumbiji alikoambatana na Rais Kikwete katika  kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe Agosti 17,  2021 na kumalizika jana jioni  Agosti  18 2012. Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola. Nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja