UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John Mnyika kuwa serikali ilipeleka
maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru mbunge wa
jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu
waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu.
Mnyika
alisema kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe)
akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada
baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu
na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia drip aliyohisi ilikua na lengo
la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa.