Tuesday, August 14, 2012

F.B.G [Fly But Ghetto] ft. Banx - Cypher [Lington Tv]


PICHA MBALIMBALI KATIKA HARAMBEE WA M4C YA CHADEMA JIJINI DAR ZILIPATIKANA JUMLA YA TSH MILIONI 323

                                     Mshehereshaji Bi. Rose akiendesha shughuli yenyewe.
 Mwenyekiti wa hakati za Movement for Change - M4C iliyo chini ya CHADEMA Bw. Alex Mayunga akiongea machache.
 Wanakamati wa hakati za Movement for Change - M4C iliyo chini ya CHADEMA wakiwa mbele ya wageni wakati mwenyekiti wao Bw. Alex Mayunga akiwatambulisha.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiingia ukumbini huku akiwa ameambatana na viongozi wenzake.

                               Wapambe wakiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa.
 Mweka hazina wa hakati za Movement for Change - M4C iliyo chini ya CHADEMA akiongea machache.
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akimtambulisha kwa wanaharakati  Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari wakati wa ufunguzi wa harambee ya Movement for Change - M4C iliyopo chini ya CHADEMA. Jumla ya shilingi Milioni 323 zimepatikana katika harambee hiyo ambapo katika hizo pesa taslimu ni shilingi milioni 70 na ahadi ni milioni 253. Hafla hiyo ya kuchangia ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar.
                                          Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari
 Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari huku pembeni yake akiwepo Mbunge mstaafu wa Jimbo la Arusha Godbless Lema.
                                           Mbunge mstaafu wa Jimbo la Arusha Godbless Lema.

Serikali kujenga hospitali teule Himo

Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri

SERIKALI imetenga kiasi sh. milioni 400 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali teule ya Wilaya kwenye Mji wa Himo.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Aggrey Mwanri wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Vunjo(TLP) Augustine Mrema lililouliza kuwa utekelezaji wa hospitali hiyo imefiki hutua gani? Na ni lini hospitali hiyo itakamilika.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema Serikali kwa kutambua umuhimu wa mradi huo imetenga fedha hizo mbazo zitatumika kuanza ujenzi wa hospitali hiyo. Hivyo zabuni zilitangazwa na kufunguliwa Julai 18, mwaka huu na mchakato wa kumpta mkandrasi mpya unaendelea.

Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa ni kusudio la seriklai kukamilisha ujenzi wa hospitali hii haraka iwezekanvyo ili kuwaondolea usumbufu wanananchi wa Vunjo.

Aidha Naibu Waziri huyo aliongeza kuwa Serikali iliamua kujenga hospitali ya Wilaya kwa kutenga fedha za ujenzi wa hospitali ya Himo katika mwaka wa fedha 2008/2009 kiasi cha sh. milioni 175. Fedha hizi zilikusudiwa kutumika katika ujenzi swa jingo la wagonjwa wan je (OPD) na kwa sasa jengo hilo, limekamilika na linatumika.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2009/2010 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi milioni 300, ambapo sh. milioni 200 zilitolewa na kupitia Mpango wa Ruzuku wa Serikali za Mitaa (LGDG) na sh. milioni 100 kupitia Mpango wa Maendeleo wa Afya Msingi (MMAM) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya uchunguzi(X-ray), utawala, huduma ya mama na mtoto, vyoo, na uzio wa eneo la hospitali hiyo.

Alisema kazi hiyo alipewa mkandarasi Edcat International ConstructionLtd. Hivyo wakti utekelezaji ilidhihirika kuwa mknadarasi huyo alifanya kazi chini ya kiwango na halimashauri iliamua kuvunja mkataba wa kuzingatia kanuni na makubaliano

Katika swali lake la nyongeza Mrema aliuliza kuwa ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya mkandarasi huyo, ikiwemo miradi mingine iliyochini nya kiwango.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema hatua iliyochukua ni kumsimamisha na pia watafanya tathimini ya fedha zilizotumika ili kungalia thamani yake, pia watatembelea miradi mingine na iliyochini ya kiwango ili kuwezackuchukua hatua.

Wakati huo huo, Serikali imepanga kununua gari la zimamoto kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa majengo yenye urefu wa kufikia ghorofa 37, ambao ndio urefu wa mwisho wa gari hilo duniani katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014.

Taarifa hiyo imetolewa Agosti 13, 2012 bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima wakati akijibu swali la Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya (CUF) akitaka kujua ujenzi wa majengo mapya sasa unafikia ghorofa 20 unazidi kuongezeka ilhali hakuna vifaa vya kuweza kuzima moto kulingana na ujenzi huo.

Chanzo: www.thehabari.com

Bodi ya Mikopo, TCU yawaengua 3074 walioomba

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi 3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) mwezi huu (Agosti 10 na 12, 2012) zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari mbalimbali.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo ya vyuo.

Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.

Kwa upande wake TCU imewaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha katika taarifa yake.

Miongoni mwa dosari ambazo zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O’ level na A’ level Index number), miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji (Contact information e.g. Mobile phone number, email address and postal address) pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).

Waweza kuingia katika linki hii hapo chini na kuona majina ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika maombi yao kwa TCU http://www.tcu.go.tz/uploads/file/LIST%20OF%20APPLICANTS%20FOR%202012-2013%20ADMISSIONS%20WITH%20MISSING%20INFORMATION.pdf

Pia waweza kutembelea linki zifuatazo na kushuhudia majina ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika maombi yao kwa bodi ya mikopo;- http://www.heslb.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=365&Itemid=66 http://www.heslb.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=366&Itemid=67 http://www.heslb.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=367&Itemid=68
post graduate;- http://www.heslb.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=363&Itemid=65

Hata hivyo taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz na www.tcu.go.tz

Habari hii imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)

MICHUANO YA MBIO ZA BOTI YA ‘MERCEDES CUP 2012′ YARINDIMA JIJINI DAR ES SALAAM

 Washiriki wa mashindano ya Mercedes Cup 2012 ya Boti zinazokwenda na Upepo (Sailing Boat) wakiwa wamekusanyika Yatch Club jijini Dar kabla ya kuanza mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors yanayofanyika kila mwaka.
                                   Pichani ni Boti zinazotumika katika mashindano hayo.
                    Washiriki wakianza mashindano hayo kuzunguka fukwe karibu na kisiwa cha Bongoyo.
                                                              Washiriki wakichuana.
                      Boti iliyombeba Refarii wa mashindano hayo pamoja na wasimamizi wengine.
                                                                 Tuzo za washindi zikiwa mezani.
 Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed(katikati) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) pamoja Catamaran Representative wa Dar es Salaam Yatch Club Andrew Boyd.
                          Washiriki na familia zao wakisubiri kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi.
 Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh akimkabidhi zawadi Refarii wa mashindano hayo.
 Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (Kulia) na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) katika picha ya pamoja ya washindi wa kwanza hadi wa tatu walioshiriki mashindano ya Boti zinazokwenda kwa upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 baada ya kukabidhiwa vikombe na zawadi zao yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
                                 Washindi wa tatu David na Sarah Scott wakipokea zawadi na tuzo.
                    Katika picha ya kumbukumbu na wadhamini wa mashindano CFAO Motors.
        Pichani Juu na Chini Washindi wa pili Paul na Kim Troll wakipokea zawadi kutoka CFAO Motors.
 Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akikabidhi Kombe kwa timu ya washindi wa kwanza wa mashindano ya Boti zinazokwenda kwa kutumia upepo (Sailing Boat) ya Mercedes Cup 2012 Al Bush na Jeppe yaliyofanyika katika fukwe za Yatch Club Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh. Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yamedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.

                        Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akigawa Champagne kwa washindi.
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (katikati) akizungumza machache baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo amewataka watu kujitokeza kwa wingi kila mwaka na kutoa shukrani zake kwa wote walioshiriki kufanikisha mashindano hayo. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed na kulia ni Andrew Boyg wa Dar es Salaam Yatch Club.
                                          Mshindi wa kwaza akifungua Champagne.

TAIFA STARS YAWAFUATA WABOTSWANA LEO

 Washambuliaji wa timu ya taifa, (Taifa Stars) Mrisho Ngassa (kulia) na Haruna Moshi Boban wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano.
 Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars Juma Kasseja akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano .
Wachezaji wa timu ya Taifa,Taifa Stars wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya safari ya kwenda Gaborone, Botswana kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kesho Jumatano.

Mgogoro wa Ziwa Nyasa na tamaa ya Malawi katika mafuta na gesi


                            Wanafunzi wakivuka ziwa Nyasa kuelekea shule.

SASA ieleweke wazi kwamba hali si shwari kati ya Tanzania na Malawi. Pengine ni vizuri kujiuliza leo ni kwa nini mtafuruku uchukue nafasi kubwa leo. Kivipi Mtanzania wa kawaida, aoneshwe kama ni jambo lililokuja ghafla?

Kimsingi, mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi umekuwapo kwa zaidi ya nusu karne. Hivi sasa umechukua sura mpya baada ya nchi hiyo jirani kusema ndiyo inayomiliki sehemu yote ya ziwa hilo.

Pengine kauli hiyo peke yake, isingeleta shari. Alama ya hatari imetokana na kauli ya vitisho, iliyotoka Serikali ya Malawi kwamba itafanya kila linalowezekana, ikiwamo kutumia nguvu za kijeshi kuhakikisha ziwa hilo linabaki kwenye himaya yao.

Picha iliyopo ni kwamba Malawi wameshaona Watanzania ni wapole. Kwamba ni waoga wa kupitiliza, kwa hiyo wakiambiwa kuhusu nguvu ya kijeshi, watarudi nyuma. Sijui uthubutu huu wameupata wapi lakini ninachowaza ni kwamba viongozi wa Malawi, wanahisi sisi ni mazezeta.

Vile ambavyo madai yao yalivyo hayana msingi na hayakubaliki hata kidogo, ndivyo ambavyo ukitafakari wanachokitaka kiwe, huku wakitoa vitisho vya kupigana vita, unaweza kujiuliza kuhusu wigo wa uelewa wao. Ni rahisi kuamini ndugu zetu hao wana dosari za kiufahamu.

Kweli Ziwa Nyasa lote ni lao? Huo mpaka ni wa namna gani hasa, kiasi kwamba eti Mtanzania akikanyaga tu maji ya ziwa hilo, anakuwa yupo Malawi. Muda wa kutafuta maelewano hawataki, wanakimbilia kwenye vita. Malawi wanahitaji kuwaheshimu Watanzania. Ni ukweli ulio wazi kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Malawi kutoa madai hayo, lakini ni mara yake ya kwanza kutumia kauli yenye vitisho vya kiwango hicho kinachoashiria vita kati ya Tanzania na wao. Madai hayo yalitolewa kwa mara ya kwanza na Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, Dk. Kamuzu Banda.

Madai hayohayo, yalirudiwa na wanasiasa mbalimbali, akiwemo mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani, Chakufya Chiana. Baadhi ya maswali yanayoulizwa ni haya yafuatayo;

Chukua dakika mbili tu Kusoma Hii Kutoka Gazeti la Uwazi "INASIKITISHA"

TUKIO la mwanamke Rehema Nungu kukutwa ameteketea kwa moto ndani ya gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 883 BLA katika msitu wa Mabwepande, jijini Dar Agosti 1, 2012 linazidi kugusa akili za wengi hasa kutokana na utata wa tukio lenyewe na hii ndiyo ripoti kamili.

Taarifa zilizopenyezwa na ndugu mmoja wa Simon Sakilu ambaye ni mume wa marehemu, zinadai kuwa kabla ya tukio hilo, Rehema na mumewe walikuwa kwenye ugomvi mzito usiokuwa na dalili ya kumalizika.

MAELEZO YA UPANDE WA MWANAUME
Habari zinadai kwamba marehemu alikuwa akidaiwa fedha na mfanyabiashara mmoja (hakutajwa jina) lakini mumewe hakulijua deni hilo mpaka siku za mwisho za uhai wa Rehema ambapo hata hivyo hakumuuliza.
Aidha, ikadaiwa kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa akimdai marehemu kwa vitisho kwamba asipolipa atamwambia mumewe, jambo ambalo mwanamke huyo hakutaka litokee.

Siku ya tukio, habari zinadai kuwa marehemu aliamka mapema na kufanya shughuli za nyumbani na baada ya muda inadaiwa alikunywa sumu ambayo haikujulikana ni ya aina gani.

Ikazidi kudaiwa kuwa baada ya kitendo hicho, mumewe alifanya juhudi za kumnywesha  maziwa ili kuokoa uhai wake lakini ilishindikana kufuatia mke kumzidi nguvu mumewe na kukimbilia kwenye gari na kuondoka nyumbani kwenda kusikojulikana.

 “Mwanamke alipokunywa sumu, mumewe (Simon)alifanya juhudi za kumpa maziwa ili kuokoa maisha yake lakini alizidiwa nguvu, mke akatoka na gari na kwenda kusikojulikana.

“Simon alikwenda kukutana na mdai wa mkewe na kumlipa fedha zake akiamini mkewe alikunywa sumu kwa sababu ya deni, baada ya malipo akampigia simu mkewe ili kumtaarifu lakini simu hiyo ilikuwa inaita na kukatika, baadaye haikupatikana kabisa,” alisema ndugu huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake gazetini.
Kuanzia hapo, ndugu walianza kumsaka Rehema mpaka Agosti 2 mwaka huu habari zilipopatikana habari  kwamba kuna gari limekutwa limeteketea kwa moto kwenye msitu wa Mabwepande. Mtu aliyedaiwa ndiye alikuwa dereva naye alikuwa ameungua na kubaki majivu na fuvu likiwa sehemu ya kiti.

Hata hivyo, ndugu hawakutaka kuweka msiba wakiamini aliyefariki dunia kwa moto huo anaweza asiwe Rehema. Ili kujiridhisha na hilo, walichukua mabaki hayo na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa vipimo vya DNA. 

MUME ANA SIRI NZITO?
Habari zaidi kutoka ndani ya familia hiyo zinadai kuwa huenda Simon ana siri nzito juu ya kifo cha mkewe Rehema kwani haingii akilini mume kuzidiwa nguvu na mkewe wakati wa kumsaidia kumnywesha maziwa.
Aidha, mpenyesha habari huyo aliendelea kufunguka kwamba ilikuwa ni kawaida kwa wanandoa hao kutibuana na mke kwenda anakojua hata kwa siku tatu bila mwanaume kujishughulisha kumtafuta.

MAELEZO UPANDE WA MKE
Agosti 6, 2012  mapaparazi wetu walifika nyumbani kwa marehemu Rehema, Mbezi Beach, Dar na kukuta watu wachache ikidaiwa hali hiyo ilitokana na wengi kutoamini kama Rehema alifariki dunia. Mume wa marehemu hakuwepo msibani hapo bila kujulikana alikokwenda.

Alipotafutwa ndugu wa marehemu kuzungumzia suala hilo, kila mmoja aliruka na kudai mwenye uwezo wa kuzungumzia jambo hilo ni mama mzazi ambaye naye aligoma kusema lolote.

“Mwenye uwezo wa kuzungumzia suala hilo ni mama mzazi lakini amegoma kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa vile  anahisi kuna mchezo mchafu umefanyika,” alisema ndugu mmoja.
Hata hivyo, mtu mmoja wa karibu na familia ya marehemu alisema kuwa habari kamili juu ya msiba huo zitapatikana mara baada ya kupata vipimo kutoka kwa mkemia mkuu kubaini kama kweli aliyekutwa ameteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema.

“Ni vigumu kulizungumzia suala hili kwani linatatanisha, unaweza kusema aliyekufa ni Rehema na matokeo ya mkemia mkuu yakitoka yakaonesha tofauti, inaweza kuleta shida, tusubiri majibu kwanza,” alisema mtu huyo bila kutaja jina lake.

MAJIBU YA MKEMIA MKUU YATOKA
Agosti 10, 2012 mmoja wa ndugu wa marehemu alimpigia simu mwanahabari wetu na kumweleza kuwa majibu ya Mkemia Mkuu wa Serikali yametoka na kubaini kwamba aliyekufa ni Rehema Nungu.
“Kama unavyosikia vilio hivyo, nipo msibani, majibu ya mkemia mkuu yamebaini aliyekufa ni Rehema Nungu, taratibu za mazishi zinafanywa sasa ila naomba muende nyumbani kwa Simon mtapata habari kamili,” alisema ndugu huyo na kusisitiza kuwa kama msiba utafanyika kwa mume wa marehemu, hawatakwenda ila watakwenda makaburini tu.

NYUMBANI KWA SIMON
Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu walifika nyumbani kwa Simon, Tegeta Nyuki, Dar na kumkuta msemaji wa familia hiyo aliyejulikana kwa jina moja la Dedu.

Dedu alipopewa pole ya msiba na kutakiwa kueleza sababu za kifo cha marehemu, alisema waulizwe polisi yeye hawezi kusema chochote licha ya kukutwa na picha ya marehemu mkononi.

“Siwezi kusema chochote, kamuoneni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ana habari zote za msiba huu, naomba mniache niendelee na taratibu za hapa,” alisema Dedu.

HUYU HAPA KAMANDA WA MKOA WA PWANI

Agosti 10, 2012 mwandishi wetu alitinga katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu kwa lengo la kujua chochote kuhusu kifo cha mwanamke huyo lakini hakuwepo, ikabidi apigiwe simu yake ya kiganjani ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli majibu ya tukio hilo yametoka, mtu aliyeteketea kwa moto ndani ya gari ni Rehema lakini sipo katika nafasi nzuri ya kuongea kwani niko Muhimbili nashughulikia majeruhi wa ajali ya wanakwaya wa kutoka Kenya.

“Hata kesho (Agosti 11) sitakuwa ofisini kwani nitakuwa bado nashughulikia suala hilo, waliofariki ni raia wa nje hivyo ni vyema nikahakikisha wanasafirishwa kurudi kwao,” alisema Kamanda Mangu.

UTATA
Asubuhi ya Agosti 11, 2012, wanahabari wetu walidamkia nyumbani kwa Simon ili kutaka kujua taratibu za mazishi.
Nje ya nyumba alikuwepo Dedu na mzee mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake, akasema yeye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya mazishi. Wawili hao waligoma kuongea chochote kwa madai yaleyale, suala liko polisi.

Hata hivyo, muda huohuo simu ya Dedu iliita, alipopokea ilionekana kupigwa na ndugu mmoja wa marehemu ambaye alisema mazishi ya mabaki ya mwili wa Rehema (fuvu na majivu) yangefanyika Jumamosi au Jumapili iliyopita lakini baada ya kupata kibali kutoka kwa mkemia mkuu.
Baadaye habari kutoka ndani ya familia ya Rehema zilisema kibali cha kuzika masalia ya mwili wa marehemu kilikuwa kipatikane jana Jumatatu.

Marehemu Rehema ameacha watoto wawili, Ngimba na Muheri.

Chanzo: Uwazi - George Kayala na Haruni Sanchawa

Wasomi UDSM Waikosoa Bajeti Ya Elimu ‘Live’

                                            Baadhi ya maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu
TAASISI ya HakiElimu leo jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla ya kutoa maoni yao.

Wadau hao wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye mkutano kisha baadaye kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa walimu wa juzi pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni tatizo kwa elimu na kuiingiza kama changamoto.

“Binafsi kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa walimu katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara hiyo…na hata migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa akijadili katika mkutano huo.

Alisema wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na sekondari kwa kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha tano na sita eneo ambalo limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni. Alikosoa kiwango cha uwiano kati ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya walimu wapo shule za mjini huku hali mbaya ikiwa vijijini.

Aidha aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika bajeti yake. “…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu imesababishwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa katika bajeti ya waziri,” alisema msomi huyo.

Kwa upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM akizungumza katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya kawaida hivyo ni vigumu kumaliza changamoto lukuki za elimu zinazoikabili wizara hiyo.

Alisema bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa kuonesha ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa, bila udhibiti. “…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni tatizo lingine. Pia uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa kulinganishwa na waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia kiwango kinapanda kumbe tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,” alisema msomi huyo.