Tuesday, April 9, 2013
MWAKYEMBE ASHANGAZWA NA ONGEZEKO KUBWA LA NAULI.... ..AMETOA AMRI NAULI ZA TRENI ZISIPANDE
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewatuliza Watanzania kuhusu kupanda kwa nauli akisema ameyapokea malalamiko yao na atayafanyia kazi.
Kwa kuanzia ameagiza nauli za treni jijini Dar es Salaam zisipande bali ziendelee kutozwa za zamani mpaka taarifa zaidi itakapotolewa.
Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipozungumza kwenye Bonanza la Vyombo vya Habari lililofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Alisema ni kweli Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra|) ilitangaza nauli mpya, lakini kwa kilio cha Watanzania ataangalia sababu za kupandisha huku akishirikiana na wasafirishaji kujua ukweli.

WAKATI UHURU AKIAPISHWA KENYA LEO, RAILA NA WENZAKE WANADAIWA KUJA HUKU, TAZAMA PIA HII WEBSITE ILIYOFUNGULIWA KWA AJILI YA UHURU
Wako kwenye mbuga za wanyama Afrika Kusini wanakula bata ni Raila Odinga na wenzake wawili akiwemo Kalonzo Musyoka.
SERIKALI YAKUBALI KURUDISHA ADHABU YA VIBOKO SHULENI
Serikali imesema itarudisha adhabu ya viboko kwa wanafunzi shuleni ili kujenga nidhamu na kujituma.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua tovuti ya www.shledirect.co.tz inayowezesha wanafunzi kujisomea kwa njia ya mtandao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kuondolewa kwa adhabu ya viboko shuleni kumewafanya wanafunzi wengi kukosa nidhamu na wakati mwingine kujifanyia mambo kienyeji.
“Wasipotandikwa mambo hayaendi, nilipokuwa mwalimu mkuu nilikuwa nawatandika kweli ndiyo maana shule yangu ilikuwa ikiongoza Mkoa wa Mbeya hivihivi hawaendi...” alisema huku akishangiliwa na wageni waalikwa.
Alisema watoto wa siku hizi wamekuwa wakitumia vibaya teknolojia ambayo ingeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao... “Tovuti kama hiyo ingewasaidia kwa masomo, lakini wao wanakimbilia kwenye facebook na mambo mengine yasiyofaa.”

RAIS KIKWETE AWASILI NAIROBI KENYA KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA RAIS UHURU KENYATTA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakilakiwa kwa
heshima zote baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais
wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William
Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi tayari kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Nne wa Kenya Mhe Uhuru Muigai Kenyatta na Naibu Rais wake Mhe William Ruto katika uwanja wa michezo wa Kasarani .

PICHA: LULU MICHAEL, MAMA YAKE NA MAMA KANUMBA WATEMBELEA KABURI LA MAREHEMU KANUMBA
Muigizaji Lulu, mama yake, na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba
walikua miongoni mwa watu walioshiriki katika misa ya kumbukumbu ya
mwaka mmoja tangu marehemu Kanumba afariki dunia, na kutembelea kaburi
la msanii huyo Kinondoni, Dar. Lulu, ambaye ana kesi ya kuhusika na kifo
cha msanii huyo, yuko nje kwa dhamana. Zifuatazo ni baadhi ya picha za
tukio hilo
Subscribe to:
Posts (Atom)