Monday, November 26, 2012

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe,Adhibitisha Ajali ya sharo Milionea

Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.

Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.

Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.

Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.

“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa nje kupitia kioo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.

Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.

Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alinusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam.

Tanzania Asilialive inatoa salamu za Pole kwa Familia, wasanii wa Filamu, Vichekesho na muziki nchini kwa Msiba huo mzito  hasa ukizingatia kuwa bado wapo katika Msiba wa Mcheza filamu John Stephen anaetarai kuzikwa kesho Makaburi ya Kinondoni.

INATISHA; ANGALIA PICHA YA SHARO MILIONEA BAADA YA AJALI...

Inatisha lakini hatuna jinsi zaidi ya kuamini kuwa ni kweli imetokea....hivi ndivyo ajali ilivyochukua maisha ya Sharo millionea!... R.I.P Sharo Milionea!

Breaking News Sharo Milionea Amefariki

 leo 26,11,2012 majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”

Ripoti Ya Nchi Maskini Sana Duniani Ya Mwaka 2012

RIPOTI YA NCHI MASIKINI SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA TARAKIMU

Geneva, 26 Novemba 2012 – Ripoti ya  Nchi Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121, yenye kichwa kidogo cha habari Kutumia Fedha Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa Uzalishaji, imetolewa leo.

Mwelekeo wa uhamiaji
Ø  Idadi ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs) iliongezeka kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010. Hii ni sawa na 3.3% ya wakazi wote wa nchi hizo.

Ø  Nchi Maskini Sana Duniani  zinatoa 13% ya wahamiaji duniani kote---idadi ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote duniani (12.1%).
Ø  Wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha

Ø  Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni 3.5 kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi duniani.
Ø  Mwaka 2011 kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na kutoka Kenya dola milioni 2.5.
Ø  Mwaka 2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15), na kiwango hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi  Kutoka Nje, yaani ODA (dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje ya nchi.
Ø  Kiwango cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja mmoja kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30 kati ya mwaka 2000 na 2010.

Ø  Fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs ikilinganishwa na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha zinazotumwa na raia kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea (ambazo siyo LDCs).

Ø  Kuanzia mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo kinalingana na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
Ø  Tangu mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za nje kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata kutokana na mauzo ya bidhaa nje.

Ø  Kwa LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi kile cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi kutoka nje  (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi za Bangladesh, Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen. Kwenye nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.

Ø  Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
Ø  Duniani kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha fedha kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja (12%).

Ø  Kama nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato yao yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6  mwaka 2010.

Ø  Asilimia 66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na 2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na Sudan.

Ø  Matumizi ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi 1,000)  kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha kutoka ng’ambo.

Kuhama kwa utaalam                                   

Jamani katika Wasani aliyekuwa anakuja kwa kasi ni huyu atimae Hatunae tena Dunuani

                                                                        John Maganga
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa akipanda juu kwa kasi, John Maganga (22) amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokimbizwa akiwa hoi, inasikitisha sana.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baba mdogo wa John, Deogratius Shija alisema Ijumaa iliyopita, marehemu alipatwa na maumivu ya ghafla ya tumbo, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu ya Mwananyamala, Dar ambako vipimo vilidai utumbo wa mgonjwa huyo ulitoboka.

Shija: “Daktari akatuambia kutokana na hali hiyo watamfanyia upasuaji ili kuuziba utumbo huo lakini mara baada ya zoezi hilo daktari akasema tatizo halikuwa kutoboka kwa utumbo bali kuna kitu kingine.

“Ikabidi tumkimbize Muhimbili ambako madaktari wa pale walituambia wenzao wa Mwananyamala walikosea kumfanyia upasuaji John kwani tatizo halikuwa la kufanyiwa upasuaji bali alitakiwa apatiwe dawa.

“Madaktari wakatuambia tumwache pale ili waokoe maisha yake sisi ndugu turudi asubuhi. Tulipokwenda asubuhi tukaambiwa mgonjwa wetu alifariki dunia usiku uleule. Imetuuma sana.”      

Hivi karibuni, John aliandaa filamu yake ambayo aliipa jina la Beautfools ambayo yeye alicheza kama mume wa ndoa wa Aunt Ezekiel ambaye alimtenda John wakati anasoma chuo.

Marehemu alikuwa akienda vizuri katika tasnia ya filamu na ilisadikiwa angeweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. Kifo cha John kimeacha pigo kubwa Bongo Movies ambayo mpaka leo vilio vimetawala.

Mazishi ya msanii huyo yalikuwa yakimsubiri mama yake mzazi aishie London Uingereza.

Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Magazeti ya leo Jumatatu 26th November 2012

Michoro Ya Kampasi Ya Muhimbili Itakayojengwa Mloganzila Kisarawe

Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini Kwembe katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam. Hii ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, ujenzi wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Kwa maneno mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila inategemewa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2015. Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600).

Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeshaanza na kufikia hatua ya juu na ambapo pia hospitali hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba mchakato wa kufanikisha uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali.

Chuo hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni mikakati kabambe ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi ina wataalamu wengi na huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa udaktari na huduma za afya kwa mwaka.

Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila na Kampasi ya afya ya UDOM utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani wa wagonjwa kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.

Na Michuzi