Wednesday, January 23, 2013

Hii kali Aliyekamatwa na pembe za ndovu ni askari wetu - JWTZ

 JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kwamba mwanajeshi aliyekamatwa juzi katika tukio la ujangili mkoani Arusha ni askari wake. Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe jana alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba MT 59509 Sajenti, Azizi Athuman Yusufu ambaye alisema ni askari wa jeshi hilo na alikuwa dereva wa mkufunzi wa kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha hapa nchini.

Hata hivyo Kanali Mgawe alisema mkufunzi huyo wa kijeshi, hakuwapo wakati wa tukio hilo. “Kweli huyo ni askari wetu. Alikuwa anamwendesha mkufunzi wakijeshi kutoka Zimbabwe. Siku hiyo alimrudisha nyumbani kwake saa saba mchana na kwenda kupaki gari. Lakini baadaye saa moja usiku, alikwenda kulichukua gari hilo na kutokomea nalo kusikojulikana hadi alipokutwa katika tukio hilo,” alisema Kanali Mgawe.

Kamati ya rufaa TFF itatenda haki

             TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF YAAHIDI HAKI

Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahidi wadau wa mchezo huo kuwa itafanya kazi zake kwa misingi ya haki.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa Kamati hiyo uliofanywa Dar es Salaam leo mchana (Januari 23 mwaka huu) na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kwa niaba ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, Mwenyekiti wa Kamati hiyo yenye wajumbe watano Idd Mtiginjola amesema wapo kwa ajili ya kutenda haki.

Mtiginjola amesema Kamati yao inaundwa na watu waadilifu, hivyo watafanya kazi kwa kuzingatia kanuni zilizopo na sheria nyingine za mpira wa miguu ikiwemo Katiba husika.

Chadema wamrarua Nape, Mwigulu kuhusu kauli zao

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.

Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.

Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu Nyerere, laana hiyo iko ndani ya CCM yenyewe,” alisema.

MAMA SALMA KIKWETE, ATEMBELEA AMREF NA POUR FOUNDATION

 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwanzilishi na Rais wa Foundation Pour  l¨ Enfrance Mama Anne Aymone Giscard d’ Estaing na Mke wa Rais Mstaafu wa Ufaransa Bwana Valery Giscard d’ Estaing, wakati Mama Salma alipotembelea makao makuu ya taasisi hiyo jijini Paris Ufaransa tarehe 22:1:2013: Mama Salma yupo nchini Ufaransa akifuatana na Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini humo:
Rais wa AMREF France Bwana Nicolas Merindol akimkaribisha Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwenye makao makuu ya shirika hilo jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 22, 1, 2013 na baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo juu ya ushirikiano zaidi wa taasisi hizo katika masuala ya afya na elimu:

Wakala ya kusimamia mji mpya kigamboni yaanzishwa

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africajijini Dar es salaam  leo wakati alipotangaza rasmi kuanzishwa kwa Wakala wa kusimia maendeleo ya mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA) Kushoto ni Christian Mwangaja Kaimu Kamishna mambo ya Ardhi na katikati ni Sellasie Mayunga Upimaji na Ramani.

JK. AMALIZA ZIARA YAKE YA UFARANSA LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orly, Ufaransa, baada ya kumaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo leo Januari 23, 2013



PICHA NA IKULU

Matata mwanamitindo bora afrika 2012

 MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ambaye ameng’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).

Ndege ya ATCL yaanza tena safari za Kigoma

 ATCL 2Kapteni  Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8 Q300 .

Magazeti ya leo Jumatano 23rd January 2013



BALOZI WA UINGEREZA AMTEMBELEA KINANA

 Kinana akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Uingereza

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner aliyemtembelea  Januari 22, 2013, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. kwa ajili ya  mazungumzo maalum ya kikazi.
Kinana, Migiro na Balozi

Mh lowassa atoa maoni katiba mpya

Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Lowassa, Mhe. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nje ya ofisi za Tume hiyo leo (jumanne januari 22, 2013)Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutoa maoni na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya. Wengine pichani ni Wajumbe wa Tume, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Bi. Maria Kashonda na Dkt. Sengondo Mvungi.