Sunday, August 5, 2012

AJALI MBAYA YA MALORI YAUA WANNE KITONGA IRINGA

 
 Wananchi mbali mbali pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa (hayupo Pichani) MOhamed Mpinga wakitazama malori mawili yaliyogongana katika mteremko wa Kitonga Iringa usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu wanne baada ya kutumbukia katika korongo
 Gari ya kampuni ya Asas Iringa ikijaribu kutoa msaada wa kuvuta malori yaliyogongana ili kutoa maiti iliyonabanwa na malori hayo
                        Mwili wa dereva wa lori ukiwa umebanwa katika eneo hilo la tukio
      Askari polisi na wananchi wakitazama moja kati ya maiti zilizo naswa katika mabaki ya malori hayo
                    Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akiwa eneo la tukio
 Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga akipandisha mlima kutoka katika korongo la mlima Kitonga Iringa akitoka kushuhudia ajali mbaya ya malori mawili yaliyogongana na kutumbukia korongoni na kupelekea vifo vya watu wanne papo hapo usiku wa kuamkia leo
                      Hivi ndivyo malori hayo yalivyogangana eneo hilo la Kitonga leo
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga (kushoto) akiwa eneo la ajali mlima Kitonga leo

HUKU mkoa wa Iringa ukiwa umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka huu ,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda ashuhudia ajali mbaya iliyopelekea vifo vya watu wanne kufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam .

Hata hivyo dereva wa lori bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo hilo alipona katika ajali hiyo .

Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga alisema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la scania ambalo lilikuwa na mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo kugongwa na lori lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania ambalo lilikuwa limebeba shaba kuligonga lori lililokuwa limeegesha kando ya barabara hiyo.

Mpinga alisema kuwa katika ajali hiyo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja ambaye ni kijana alijeruhiwa vibaya na kuwa miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye inasadikika ni mkazi wa wilaya ya kilolo aliyekuwa amepanda katika lori hilo .

Alisema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na utingo wa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ambalo lilikuwa limebeba mali za dukani ambaye alikuwa nje ya lori hilo akifanya mawasiliano ya simu na mwenzake na hivyo kugongwa na lori hilo la Shaba ambalo breck zilionyesha kuwa na matatizo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na ajali hiyo kutokea Agosti 4 majira ya jioni ila zoezi la utoaji wa maiti ya dereva wa lori hilo lenye shaba bado ni gumu kutokana na mwili wa dereva huyo kubanwa vibaya ya tela la lori hilo lenye shaba .

Alisema kuwa kabla ya tela hilo lenye shaba kufunika kibini ya lori hilo kebini hiyo ilikatika na kutangulia korongoni na baada ya hapo tela lenye shaba kufuata nyuma na kutua juu ya kibini hiyo.

kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati mkoa wa Iringa unataraji kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Iringa huku akiwataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani kama njia ya kuepuka ajali kama hizo.

Aidha alisema kuwa kutokana na eneo hilo la mlima wa Kitonga kuendelea kuwa na eneo maarufu kwa ajili tayari mkakati umewekwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi en eo hilo pamoja na kufanya doria za mara kwa mara za miguu ya magari kwa askari wa usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali katika eneo hilo.

Alisema kuanzia sasa askari wa usalama barabara watawekwa eneo hilo ili kuweza kukagua magari yote ya abiria na mizigo ili kabla ya kushuka mteremko huo kuwa na uhakika wa breck kama njia ya kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ajali mbaya katika mteremko huo.

MPIGA PICHA MAARUFU IRINGA MLALAOHOI AGONGWA NA GARI LEO

 Daladala iliyomgonga mpiga picha maarufu mjini Iringa Misanjo Livigha aka Mlalahoi eneo la Miyomboni leo asubuhi
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo leo japo mpigapicha huyo hajapata majeraha makubwa sana.Tanzania Asilialive inakupa pole  Kamanda.

Chanzo:francisgodwin.blogspot.com

KENYA YAANZA KUNG'ARA MICHUANO YA OLYMPIC LONDON

Ikiwa ni wiki ya kwanza ya ikimalizika tangu kuanza kwa michuano ya 30 ya Olimpiki jijini London, huku Afrika Mashariki ikiwa bado hoi kwa kutonyakua hata medali moja kwa kuanza vibaya, mwanga wa matumaini umeonekana, baada ya Kenya kufungua ukurasa wa mafanikio kwa medali.Wawakilishi kadhaa wa nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda wakiwa wametolewa, na sasa wanariadha wa Kenya wamewafuta machozi.

Uganda nayo imejijengea matumaini, baada ya wanariadha wake kuvuka kwenye hatua za mchujo wa mbio za mita 3,000 na kuingia fainali.Tanzania inaweka tegemeo kwa wanariadha wake wanne, watakaopeperusha bendera yake Jumanne na Jumapili ya wiki ijayo, baada ya wanamichezo wake wengine watatu kutolewa.

Kwa Kenya, wikiendi imeanza vizuri kwa sababu Sally Kipyego amefanikiwa kunyakua medali ya fedha katika fainali ya mbio za mita 10,000 Ijumaa, ambapo dhahabu ilikwenda kwa bingwa mtetezi, Tirunesh Dibaba wa Ethiopia.
Dibaba hakuwa mshindani rahisi, kwani katika mashindano yaliyopita ya Olimpiki mjini Beijing alipata medali mbili za dhahabu

Kenya iling'ara zaidi kwenye mbio hizo za Ijumaa, baada ya mwanariadha wake mwingine, Vivian Cheruiyot kutwaa medali ya shaba, baada ya kupitwa na Kipyego katikati ya mbio jijini London.Kipyego alitumia dakika 30:26:37.

Cheruiyot ni bingwa wa dunia wa mwaka jana kwenye mbio za mita 10,000 na 5,000, ambapo juzi Ijumaa, kasi yake ilimfanya akamaliza mchezo kwa dakika 30:30.44. Kipyego hakuamini kupata medali hiyo muhimu ya fedha, na baada ya mbio aliishia kububujikwa machozi ya furaha."Nimelia kwa sababu ni safari ndefu, watu hawajaelewa bado ilivyo kazi ngumu na jinsi hisia zinavyochanganya kwenye mbio hizi. Unajiandaa kwa miaka mingi lakini hujui utakuja kuvuna nini siku ya mwisho.

"Mara unashitukia umekatiza mstari wa mwisho na kumaliza mbio. Kwa kweli kuna mengi yasiyoonekana tunayojinyima ili kufikia fahari hii. Kocha anaelewa na watu wachache, nashukuru sana kwa fursa nilizopata, nimefurahi sana," akasema msichana huyo mwenye umri wa miaka 26.

Kipyego anafundishwa na kocha Mark Rowland na anasema ndiye nguzo yake muhimu, kwa jinsi anavyompa moyo, ukiachilia mbali mafunzo ya muda mrefu. Kipyego ni mhitimu wa shahada ya uuguzi, na anasema kwa hatua aliyofikia, nguvu zilishamwishia na hangeweza kwa namna yoyote ile kufanya la ziada kumfikia Dibaba.

"Nilikuwa nachunga uhai wangu pia, nilijisema nikiongeza kasi huenda nisiweze hata kumaliza mbio hizi kwa hiyo ngoja niende pole pole."Nilipoangalia nikagundua Vivian (Cheruiyot) naye hakuwa anakuja kasi, nikajua naye kachona, nikaamua kumaliza taratibu," akasema akionesha uchovu wa kazi hiyo ngumu.Cheruiyot naye akizungumzia michezo hii, anasema anashukuru kupata medali ya shaba ambayo si ndogo, maana wengi wanaitafuta na kuikosa.

Anasema sasa analenga kutafuta medali kwenye mbio za mita 5,000 na kwamba amebaki kuwa mwenye furaha kubwa.
"Nilikuwa nimechoka niliposikia sauti ya kengele na sikuweza kuendelea kuwakimbiza. Kwa matokeo haya nafurahi, silalamiki wala kumlaumu yeyote, sasa najipanga kwa ajili ya mbio za mita 5,000.

 "Kupata medali ya shaba kwenye Olimpiki si kitu rahisi, hasa mnapokuwa na washindani wenye uzoefu na stamina kama hawa," anasema Cheruiyot anayepewa nafasi kubwa kushinda medali kwenye mbio za mita 5,000.
Kenya ilikuwa na mwanariadha mwingine kwenye mbio hizo, Joyce Chepkurui, lakini hakuweza kufurukuta, kwani aliishia kwenye mzunguko wa 17 na kuondolewa na wahudumu.

Katika mbio za mita 400 kuryka vihunzi kwa, Joyce Zakari wa Kenya aliwashangaza wengi kwa kuvuka na kuingia nusu fainali. Hata hivyo Vincent Kiplagat Kosgei hakufanya vizuri, kwani alimaliza katika nafasi ya saba, huku mwenzake, Boniface Mucheru akishika nafasi ya sita kabla yake Wanariadha wengine wa Kenya waliofuzu ni bingwa mtetezi wa Olimpiki mita 3,000, Brimin Kipruto, bingwa wa dunia, Ezekiel Kemboi na Abel Mutai. Zakari alionesha furaha ya aina yake baada ya kufuzu, akisema; "mwili wangu upo katika hali nzuri, na ninachosubiri ni nusu fainali tu." Kipruto aliyeonekana kujawa furaha, alipohojiwa na waandishi wa habari alisema:

''Najihisi vizuri, zilikuwa mbio nzuri na sasa tunaangaza mbele ambapo suala si kukimbizana na muda bali medali."

Mfaransa Mahiedine Mekhissi, ambaye awali alijulikana kwa jina la Mekhissi-Benabbad, alionekana kuwaogopa Wakenya, kwani alisema atakuwa mpweke kwenye mbio hizo, kwa sababu atakuwa dhidi ya Wakenya watatu.
Mfaransa huyu aliyepata medali ya fedha Beijing, na hukimbia mita 1,500 na 3,000.
"Nitakuwa mwenyewe wakati Wakenya watakuwa watatu. Lakini hii hainiogofyi kwa sababu wote ni rafiki zangu," akasema kijana huyo mwenye umri wa miaka 27.

Benjamin Kiplagat afuzu kwa Uganda. Kwa upande wa Uganda, mwanariadha wake mahiri, Benjamin Kiplagat alifanya vizuri Ijumaa kwenye mbio za mchujo za mita 3,000 kuruka vihunzi, na kupata tiketi ya kuingia fainali Jumapili hii.
Kiplagat amefufua matumaini ya Waganda kwenye michezo hii. Baada ya kuanza mbio kwa kasi, katika hatua za mwisho aliteleza na kujigonga, hivyo kushindwa kufuzu moja kwa moja.Hata hivyo, kwa kuzingatia kasi yake, na kwamba alijigonga kwa bahati mbaya, alipewa nafasi moja kati ya mbili za ziada za kuingia fainali.

Kitaalamu, ikiwa hangejigonga angeweza kushika nafasi za mbele kabisa kwenye mchujo. Alikimbia kwa muda wa dakika 8:18.44, na alipewa nafasi hiyo kwa kuzingatia ni mmoja wa wanariadha wawili walioshindwa, lakini waliokwenda kasi sana.

Kiplagat alipata medali ya fedha kwenye mashindano ya vijana ya dunia yaliyofanyika 2008, lakini pia ana medali ya shaba ya ubingwa wa Afrika.Akizungumzia alivyojizuia kuanguka na kutoka kwenye mbio hizo katika tukio hilo, Kiplagat mwenye umri wa miaka 23 alisema alijipa moyo, akijua anaibeba nchi yake.

"Nilijaribu kwa nguvu zote niweze kufuzu, nashukuru nimefanikiwa kufanya hivyo, sasa najiandaa kwa ajili ya Jumapili," akasema na kuongeza kwamba amedhamiria kupata medali wikiendi hii.Simanzi kwa Uganda ilitokea baada ya mwanariadha wake mwingine, Jacob Araptany kushindwa kufuzu, alipotumia dakika 8:35.85 na kuwa wa saba.

Kama mwenzake Kiplagat, mwanariadha huyu alitawala vyema hatua za mwanzo za mbio, akionekana angemaliza katika nafasi za juu, lakini alishindwa kadiri mbio zilivyokaribia ukingoni.Araptany alifanya vizuri kwenye hatua za aali za mashindano ya riadha ya Afrika nchini Benin Juni mwaka huu, lakini tatizo likawa mwishoni, akashindwa kung'aa.Shujaa mwingine wa Uganda anayetupiwa macho niMoses Kipsiro (26) katika mbio za mita 5,000 anayesema iwe iwavyo, hatakimbia tena mita hizo, bali anahamia kwenye marathon Olimpiki ijayo.

Kipsiro mwenye rekodi ya kupata medali katika kila mashindano makubwa anayoshiriki, anatarajia kufanya vyema wikiendi hii."Sasa nabadilisha mbio, nitaingia barabarani mwishoni mwa mwaka huu nikikimbia marathon," anasema na kuongeza kwamba atasikitishwa sana akistaafu bila kupata medali ya Olimpiki.Kipsiro ana medali mbili za dhahabu za Jumuiya ya Madola na wikiendi hii anashiriki mbio za mita 10,000 kabla ya wiki ijayo kuingia zile za mita 5,000.

"Sipo katika hali nzuri kama ambavyo ningependa kuwa, lakini nitapambana, pengine nikikosa medali itaniumiza kwa maisha yangu yote…nadhani nitafanya vizuri zaidi kwenye mbio za mita 10,000," akasema.Uganda ilileta wanamichezo 16 kwa ajili ya michezo mitatu katika Olimpiki ya London. Hao ni pamoja na Jacob Araptany,Thomas Ayeko, Abraham Kiplimo, Stephen Kiprotich, Moses Kipsiro, Geoffrey Kusuro na Julius Mutekanga.Wengine ni Janet Achola, Dorcus Inzikuru, Annet Negesa, Jane Suuto, Edwin Ekiring, Ganzi Mugula, Jamila Lunkuse na Charles Ssekyaaya.

Rwanda na Burundi hazijaona mwanga
Rwanda na Burundi bado zinasubiri majaliwa yao kwenye mashindano haya, zikiomba dua. Ndoto za Alphonsine Agahozo ambaye alikuwa tegemeo kubwa la Rwanda, ziliyeyuka Ijumaa. Alitarajia kufanya vyema kwenye kuogelea mita 50 'freestyle' kwa wanawake pale Aquatic Centre, lakini alitumia sekunde 30.72, akishika nafasi ya tatu miongoni mwa washindani wanane.Pamoja na kujitahidi huko, ufanisi wake haukutosha kumjalia nafasi kwenye nusu fainali, kwani katika kundi la waliokwenda kasi zaidi, wapo wawili waliomzidi, hivyo kumnyima nafasi. Rwanda waliokuwa wakijiandaa kwa mashindano haya huko Bury St Edmunds prior to the Games.Sasa Rwanda itabidi isubiri kwenye riadha kwa washiriki wake wa mbio ndefu za mita 10,000.Kocha wao, Innocent Rwabuhihi alisema alikuwa na matumaini ya kufanya vizuri.Mmoja wa wanariadha hao ni Claudette Mukasakindi, mwenye rekodi ya kukimbia kwa dakika 33:51.57.

Mwingine ni Robert Kajuga anayeshiriki mbio za mita 10,000 pia kwa wanaume. Hata hivyo, Kocha Rwabuhihi anasema wachezaji wake walikuwa na tatizo la kuzoea hali tofauti ya hewa ya London, ambayo hubadilika karibu kila siku.
Rwanda ilikuwa na washiriki saba, ambao ni Alphonsine Agahozo katika kuogelea, Robert Kajuga, Claudette Mukasakindi na Jean Pierre Mvuyekure kwenye riadha. Wengine ni Jackson Niyomugabo kwenye kuogelea, Adrien Niyonshuti katika mbio za baiskeli za milimani na Fred Yannick Uwase anayepambana kwenye judo.Burundi pia bado haijapata medali, licha ya kuwa na mmoja wa wakongwe wa Olimpiki, Venuste Niyongabo.

Huyu ni Mrundi wa kwanza kuwa bingwa wa Olimpiki, kwani katika Michezo ya Atlanta, Marekani mwaka 1996 alitwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza Burundi kushiriki Olimpiki, ikiwa na wanamichezo saba, na tangu hapo imeshiriki michezo yote ya majira ya joto ya Olimpiki.Mwaka 1996, Aloys Nizigama wa Burundi alikaribia kutwaa medali ya shaba, alipomaliza mbio za mita 10,000 akiwa nafasi ya nne.

Artehemon Hatungimana ana rekodi ya Mrundi wa kwanza kushiriki michezo mitatu ya Olimpiki, ambapo alishindana kwenye mita 800 mwaka 1996, tena akarudia mwaka 2000 na mwaka 2004.Kuanzia mwaka 2004, timu ya Burundi imekuwa ikijumuisha waogeleaji. Katika riadha, Joachim Nshimirimana ameshiriki nusu marathon mara mbili, mojawapo ikiwa mwaka 2008. Mwaka huu, washiriki wa Burundi ni Beni Bertrand Binobagira na Elsie Uwamahoro katika kuogelea; Olivier Irabaruta, Francine Niyonsaba na Diane Nukuri katika riadha; Odette Ntahomvukiye kwenye judo.Tanzania bado yajipa matumaini
Baada ya wachezaji wake watatu kuondolewa kwenye mashindano kwa kushindwa mbele ya washindani wao, Tanzania inawategemea wanne waliobaki. Waogeleaji wake, Magdalena Moshi na Ammaar Ghadiyali walitolewa, Moshi akishika nafasi ya mwisho kwenye mchujo kati ya washiriki saba. Ghadiyali alikuwa wa tatu, ambapo wawili wa mbele yake walivuka.

Bondia pekee, Selemani Kidunda alipoteza mchezo wake Belous wa Moldova kwa pointi 20-7. Kidunda hakuonesha kiwango kizuri, hivyo mpinzani wake hakuwa na kazi ngumu ya kumshinda. Wanariadha waliobaki kwa upande wa Tanzania ni Zakhia Mrisho anayekimbia Jumanne hii mbio za mita 5,000, kujaribu kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Wengine watatu wataingia kwenye marathon barabarani jijini London Jumapili ikayo. Hawa ni Samson Ramadhani, Mohamed Msenduki na Faustine Musa. Mwaka 2006 Ramadhani alitwaa medali ya dhahabu kwenye Michuano ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Melbourne, Australia, alipotumia 2:11:29.

Msenduki naye ameshinda mashindano mbalimbali ya Marathon, na anatarajiwa kutumia uzoefu huo jijini London. Musa anashiriki marathon kwa mara ya pili, baada ya mbio za Warsaw, Poland alikoshika nafasi ya tatu.Tanzania haijawahi kufanya vizuri kwenye Olimpiki tangu mwaka 1980, wanamchezo wake, Filbert Bayi na Suleiman Nyambui walipotwaa medali za fedha katika mashindano yaliyofanyika nchini Urusi.Marekani na China zinachuana vikali kwenye nafasi za mwanzo, huku wenyeji Uingereza nao wakichomoza kwa medali kadiri michezo inavyoendelea.Afrika Kusini ndiyo pekee barani iliyopata medali za dhahabu (tatu), pia ina moja ya fedha. Afrika Mashariki ikisubiri kuona watakacholeta wanamichezo wake baada ya medali za Kenya.

Habari kwa hisai ya Israel Saria, BBC

JAJI MARK BOMANI AONGEA NA WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba (kulia) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wajumbe wa Tume kabla ya kumkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu Jaji Mark Bomani (kushoto) kubadilishana uzoefu na Wajumbe wa Tume jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid na Naibu Katibu Bw. Casmir Kyuki (kulia).
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Kwanza Mzalendo Jaji Mark Bomani akibadilishana uzoefu na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya Tume jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba na kushoto ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim.
Baadhi ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakifuatilia maelezo ya Jaji Mark Bomani aliyekutana nao kwa lengo la kubalishana uzoefu kuhusu Katiba. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam jana

JANUARI MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANABUMBULI JIJINI DAR ES SALAAM JANA

 Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akiongea na wakazi kutoka wilaya ya  Lushoto jimbo la Bumbuli katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo mkutano huo ulikuwa  unajadili maendeleo ya jimbo la  Bumbuli na kutambulisha shirika la maendeleo la  Bumbuli, January Makamba amesema katika kipindi cha mwaka 2011-2012 kiwango cha elimu ya wilaya hiyo imekuwa chini na kusababisha vijana wengi katika mkoa wa Tanga kuwa na sifa ya kuuza chipsi na kubeba mizigo badala ya kufanya kazi kwenye makampuni.
   Wakazi kutoka jimbo la bumbuli wakiwa katika mkutano huo wa kujadili maendeleo ya wilaya ya Bumbuli
          Kikundi cha ngoma kijulikanacho Mount  Usambara Voice kikitoa burudani katika mkutano huo
 Mkurugenzi wa shirika la Bumbuli Bw. Najim Msenga (kushoto), mwenyekiti mteule wilaya ya Bumbuli Bw. Amiri Sheiza (kulia)katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (katikati)wakijadiliana jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (kushoto)na mwanakamati wa shirika la Bumbuli Bw. Naaman Shauri wakifuatilia kwa umakini mada iliokuwa ikendelea katika mkutato huo Jana

HAPPY BIRTHDAY MR OBAMA


Magazeti ya Leo Jumapili 5th 2012

Sitta Atafuta "Kumkimbia" Lowassa-Gazeti Mwananchi

ATAKA WIZARA YAKE IONDOLEWE KAMATI YA LOWASSA

Habel Chidawali, Dodoma
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amependekeza kuwa wizara yake iondolewe chini ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na iundiwe kamati yake.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni, mjini Dodoma juzi usiku wakati akihitimisha hoja za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2012/13.

Mkongwe huyo wa siasa alieleza kuwa moja ya sababu za kupendekeza hivyo ni Kamati hiyo ya Mambo ya Nje kukabiliwa na majukumu mengi hata wakati mwingine kushindwa kuitendea haki wizara yake.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Lowassa, ambaye mara kadhaa ametajwa kuwa ni mwiba kwa Wizara za Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na ile ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inayoongozwa na Sitta.

Iliripotiwa kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kuwa Lowassa akiwa kwenye vikao vya kamati yake alitaka kukwamisha bajeti za wizara hizo mbili akidai maelezo ya ufafanuzi kuhusu matumizi ya mwaka uliopita pamoja na masuala kadhaa ya kiutawala.

Kufuatia hali hiyo, kamati ililazimika kumwita Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe mbele ya kamati ili kutoa maelezo ambapo alifanya hivyo na kukubaliana na kamati hiyo.

Kauli ya Sitta inatafsiriwa kuwa ni dalili za kumkimbia Lowassa kutokana na misuguano ya kisiasa ya muda mrefu ndani ya chama chao CCM na Serikali, ambayo imekuwa ikielekezwa katika kuwania nafasi ya juu ya uongozi ndani ya Taifa.

Lowassa alijiuzulu uwaziri Mkuu, Mwaka 2008, kutokana na kuibuka kwa kashfa ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond baada ya Bunge lililokuwa chini ya uongozi wa Spika Sitta kuunda kamati teule kuchunguza kashfa hiyo.

Ingawa Sitta hakutaja moja kwa moja nini hasa atakachofanya, lakini inaonyesha kuwa hakubaliani na Kamati ya Lowassa kuisimamia wizara yake, huku akiwapoza wabunge kuwa anafanya hivyo ili kuipunguzia mzigo kamati hiyo.

Akijenga hoja ya kuundiwa kamati yake, Sitta alitoa sababu kuwa Kamati ya Mambo ya Nje inashughulikia masuala mengi ya msingi hivyo inashindwa kuwa karibu na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

“Napendekeza kuwa iundwe Kamati ya Kudumu ya Bunge itakayoshughulika na masuala ya Afrika Mashariki tu, kwani hii iliyopo sasa imekuwa na mambo mengi sana,’’ alisema Sitta na kuongeza:

“Unaweza kuona kuwa hawa wanaangalia Mambo ya Nje, wanaangalia Ulinzi na Usalama, sasa kuwapa na Afrika Mashariki ni mzigo mzito sana.’’

Hata hivyo, haijulikani kama kamati aliyopendekeza Sitta itaundwa kwa Kanuni ipi kwa kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge hakuna kamati hiyo na karibu kamati zote zimekuwa zikihudumia zaidi ya wizara moja.

Maelezo ya Lowassa
Lowassa alipoulizwa na gazeti hili jana juu ya pendekezo la Sitta, alisema kuwa, haoni kama kuna tatizo endapo kamati hiyo ikiundwa kwa ajili ya kuisaidia wizara hiyo.

“Kimsingi mimi sikuwepo, lakini kama alisema yawezekana alilenga kutoa nafasi kwa Wizara hiyo kupata chombo cha kuisemea kwa karibu.”...www.mwananchi.co.tz

Maelezo Ya Mnyika Juu Ya Muswada Wa Dharura Aliouwasilisha Bungeni

TAARIFA KWA UMMA
Tarehe 03 Agosti 2012 kwa mujibu wa Kanuni ya 68 (7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge na kwa kuzingatia kuwa marekebisho yamefanyika kwenye ratiba ya bunge ambapo Mkutano wa Bunge sasa umepangwa kuahirishwa tarehe 16 Agosti 2012 na hoja za wabunge zimeondolewa kwenye ratiba.

Nimeomba muongozo ama Serikali itoe kauli bungeni ya kutengua tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kuwezesha mafao ya kujitoa kuendelea kutolewa au uongozi wa Bunge uruhusu niwasilishe muswada binafsi wa sheria kwa hati ya dharura tarehe 16 Agosti 2012 kwa ajili ya kufanya marekebisho kwenye sheria husika ili kuruhusu mafao ya kujitoa kuendelea kutolewa.

Pamoja na hatua hiyo ya kuomba muongozo nimechukua hatua ya ziada ya kumwandikia Katibu wa Bunge kumweleza kusudio la kuwasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Sheria za Hifadhi ya Jamii (The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 kwa hati ya dharura kwa mujibu wa Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007).

Lengo la Muswada huo ni kufanya marekebisho yenye kuwezesha kurejeshwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits) ili kuruhusu kuendelea kutolewa kwa mafao kwa mwanachama wa mfuko ya hifadhi ya jamii anapoacha kazi na kuhitaji kupewa mafao yake kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

Nimeomba kupatiwa ushauri na usaidizi wa kisheria kwa mujibu wa Kanuni ya 21 (1) (d), (e) na (2) ili kuweza kuandaa Muswada Binafsi wa Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (1), Taarifa ya Muswada huo kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (2), hati ya kuwasilisha muswada kwa dharura na hoja ya kutengua masharti kuhusu muda wa utangazaji wa Miswada ya Sheria kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Mwaka 2007).

Kwa mujibu wa Kanuni ya 81 (5) masharti kuhusu muda wa utangazaji wa Miswada ya Sheria yanaweza kuwekwa kando na kutenguliwa kwa hoja kutolewa na kuamuliwa kama kutawasilishwa Bungeni hati iliyowekwa saini na theluthi mbili ya Wajumbe wote wa Kamati kama ni Muswada wa Kamati na kwa Muswada wa Mbunge hati iliyowekwa saini na Wabunge wasiopungua kumi inayoeleza kuwa muswada binafsi uliotajwa katika hati hiyo ni wa dharura.

Naomba kutoa taarifa kwamba kuanzia jumatatu tarehe 6 Agosti 2012 nitaanza kukusanya saini za wabunge wanaounga mkono kuwasilishwa kwa muswada tajwa kwa hati ya dharura kufanya haraka marekebisho yenye kuwezesha kurejeshwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits) ili kuruhusu kuendelea kutolewa kwa mafao kwa mwanachama wa mfuko ya hifadhi ya jamii.

Nimeomba pia kwa Katibu wa Bunge kwa mujibu kifungu cha 10 cha Sheria ya ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Cap 296 R.E 2002 kupatiwa nakala ya taarifa na nyaraka zifuatazo kwa ajili ya kujiandaa kuwasilisha muswada husika: Social Security Ammendment Act no.5 ya mwaka 2012, Sheria za Hifadhi ya Jamii zinazohusika, Taarifa na mapendekezo yaliyowasilishwa na kupelekea kufutwa kwa mafao ya kujitoa (withdrawal benefits) na maelezo kuhusu hatua ambayo kifungu husika kiliingizwa na hatimaye kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili 2012.

Pamoja na kuomba taarifa na nyaraka kupitia kwa Katibu wa Bunge natoa mwito kwa wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii kutunipatia maoni na mapendekezo kwa ya kuzingatiwa kwenye Muswada Binafsi wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Sheria za Hifadhi ya Jamii (The Social Security Laws (Ammendments) Act wa mwaka 2012 katika kipindi cha wiki moja.
Ikumbukwe kwamba kifungu cha kufuta mafao ya kujitoa kilichozua mgogoro hakikuwepo wakati muswada uliposomwa kwa mara ya kwanza bungeni tarehe 1 Februari 2012 bali kiliwasilishwa kupitia jedwali la marekebisho ya Wizara lililowasilishwa tarehe 13 Aprili 2012 bila malengo na madhumuni yake kuelezwa kwa ukamilifu.

Kupitishwa kwa kifungu hicho kumethibitisha maneno niliyoyatoa bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kutokana na ‘uzembe wa bunge na wabunge’ na kwa hili pamoja na mchango nilioutoa bungeni kwa maandishi siku hiyo juu ya haja ya kuwa mfumo mpana zaidi wa pensheni na hifadhi ya jamii (universal pension and social security) pamoja na kuwa sikuunga mkono kifungu husika kilichoingizwa kinyemela naomba radhi kwa wananchi wa Ubungo na wafanyakazi kwa kutokuwasilisha jedwali la marekebisho kupinga kifungu hicho kuingizwa.

Izingatiwe kuwa ili kurekebisha hali hiyo tarehe 27 Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali itoe maelezo maelezo kuhusu taarifa zilizotolewa bungeni tarehe 13 Aprili 2012 kuwa wafanyakazi ikiwemo wa migodini kupitia vyama vyao walihusishwa kutoa maoni yaliyopelekea kufutwa kwa fao la kujitoa (withdrawal benefits); suala ambalo Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini (TAMICO) kililikanusha.

Hata hivyo, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya Hotuba yake tarehe 28 Julai 2012 hakutoa majibu yoyote bungeni kuhusu suala hilo hali ambayo imesababisha migongano kuendelea katika migodi mbalimbali kuhusu madai hayo hali ambayo kwa taarifa nilizozipata tarehe 1 na 2 Agosti 2012 inaweza kusababisha migomo migodini. Kufutwa kwa fao la kujitoa kumelalamikiwa pia na wafanyakazi na wadau wa hifadhi ya jamii katika Jimbo la Ubungo na katika taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, suala hili na tukio husika litumike kama rejea ya bunge na wabunge kuikatalia Serikali kuwasilisha marekebisho yenye athari kubwa kipindi cha mwisho na hivyo wabunge kukosa fursa ya kupata maoni ya wananchi na pia Serikali itakiwe kuomba radhi kufuatia kulipotosha bunge kuwa wadau wa hifadhi ya jamii hususan wafanyakazi na vyama vyao

walishirikishwa na kuridhia wakati ambapo wamejitokeza na kukanusha madai hayo yaliyotolewa na Wizara bungeni.
Kwa upande mwingine kufutwa kwa mafao ya kujitoa msingi wake haupo kwenye marekebisho ya sheria yaliyofanyika tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali ni udhaifu katika mfumo mzima wa kisera na kisheria wa hifadhi ya jamii nchini hali ambayo inahitaji wadau kutaka mabadiliko makubwa.

Hivyo, naungana na wote wenye kutaka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kutengua taarifa kwa umma iliyotolewa ya kueleza kuwa “kufuatia kuanza kutumika kwa Sheria hiyo (ya 13 Aprili 2012) maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo itakapotolewa ili kuwezesha Mamlaka na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau”.

Aidha, pamoja na Mamlaka kueleza kwamba sitisho la fao la kujitoa si kwa sababu za Kiserikali au Mifuko kufilisika ni vizuri mamlaka ikaeleza kwa uwazi na ukweli sababu zingine za kufanyika kwa marekebisho hayo zaidi ya ile ya kutimiza malengo ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa Mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha ya uzeeni. Tahadhari za

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa za Hesabu za mwaka 2010/2011 na miaka mingine zinaashiria masuala ya ziada ambayo yanaweza kuwa yameisukuma Serikali kuja na mbinu zingine za kuhakikisha uendelevu wa mifuko ikiwemo kupitia marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii.
Ili bunge liweze kutimiza wajibu wa kuishauri na kuisimamia serikali kufanya marekebisho yanayostahili ya sheria husika kwa haraka ni muhimu ratiba ya bunge ikabadilishwa.

Tafsiri ya marekebisho ya ratiba yaliyofanyika ni kuwa hoja binafsi niliyoiwasilisha kwa katibu wa Bunge kutaka bunge lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka haitapata nafasi ya kujadiliwa bungeni. Aidha ratiba hiyo mpya hoja binafsi iliyoelezwa kuwa itawasilishwa na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo kuhusu kufutwa kwa mafao ya kujitoa kufuatia marekebisho ya sheria za Hifadhi za Jamii nayo haitawasilishwa kwenye mkutano huu wa Bunge unaoendelea kama ratiba haitafanyiwa marekebisho.

Hata hivyo, izingatiwe kuwa chanzo cha kufutwa kwa mafao ya kujitoa ni marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii hivyo ufumbuzi wa kurejesha fao la kujitoa unapaswa kuwa ni marekebisho ya sheria hatua ambayo njia ya haraka ya kuifikia ni kuwasilishwa kwa muswada wa sheria ama na serikali au kamati au mbunge badala ya hoja binafsi.

Hoja binafsi inaweza kuwezesha bunge kujadili na kupitisha maazimio ya kuitaka Serikali kuwasilisha marekebisho ya sheria au kuishauri na kuisimamia serikali na mamlaka zake katika utekelezaji wa sheria lakini sheria itaendelea kuwa palepale mpaka marekebisho yatakapofanywa kwa kuwasilishwa muswada wa sheria hatua ambayo nimeamua kuanzisha mchakato wa kuwezesha ichukuliwe.

Wenu katika kuwawakilisha wananchi,