Tuesday, March 19, 2013

Magazeti ya leo jumanne ya 19th March 2013



RIPOTI MAALUMU KUHUSU KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA

Taarifa kutoka 254 zinasema tayari kesi iliyowasilishwa na mrengo wa CORD imesajiliwa na mahakama ya upeo nchini Kenya na tayari jopo la majaji watano limeteuliwa kusikiliza kesi hiyo akiwemo rais wa Mahakama ya Upeo Dr. Willy Mutunga huku msajili wa Mahakama akithibitisha kwamba watakaosalia kusikiliza kesi hiyo ni majaji sita kinyume na kawaida ambapo huwa ni saba.

Kesi inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo march 19 2013 Nairobi kenya na endapo mrengo wa CORD utatoa uthibitisho kwamba uchaguzi ulikua na dosari, duru ya pili ya uchaguzi itaandaliwa chini ya siku 60 ambapo mrengo wa CORD unawakilishwa na mawakili kama Mutula Kilonzo na Moses Wetangula ukidai tume huru ya uchaguzi haikuzingatia mipangilio wa uchaguzi kama vile kutambua wapiga kura kupitia mitambo ya kielektronik.

TUNDULISU AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA KUJIFUNGIA CHOONI

 ZIPO taarifa kwamba Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, wiki iliyopita alijifungia chooni kukwepa waandishi wa habari waliotaka kauli yake juu ya video hatari ambayo inadaiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Rwakatare, alirekodiwa akieleza njama za uhalifu.

Tundu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amesema kuwa maelezo yaliyotolewa kwamba alijificha chooni kwa muda wa saa mbili si kweli, kwani hawezi kufanya hivyo.

“Jamani mimi na umri wangu huu nawezaje kuwakimbia waandishi wa habari? Siku zote mimi nafanya kazi na waandishi wa habari,” alisema Lissu na kuongeza:

RIPOTI MAALUMU TOKA MAHAKAMA YA KISUTU ALIKOSHITAKIWA LWAKATARE WA CHADEMA

HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya ugaidi.

Mbali na Lwakatare mshitakiwa mwingine ni Ludovick Rwezaula Joseph ambao wanatetewa na mawakili wa kujitetemea Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Nyaronyo Kicheere.

Washitakiwa hao wakifikishwa jana saa mbili asubuhi mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ilala, Duwani Nyanda na kuifadhiwa nyuma ya jengo la mahakama hiyo tayari kwaajili ya kufikishwa kizimbani kosomewa mashitaka yanayowakabili.

LWAKATARE ASOMEWA MASHITAKA YA UGAIDI

                       Lwakatare akionesha alama ya vidole viwili wakati akipelekwa kizimbani.
          Wanachama na mashabiki wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili kabla ya kesi kuanza.

LULU MICHAEL ALIKUMBUKA PENZI LA STEVEN KANUMBA.....

Wakati zikiwa zimebaki wiki chache tu hadi kifo cha Stephen Kanumba kitimize mwaka mmoja, aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael aka Lulu kwa mara ya kwanza leo ameandika ujumbe kuhusiana na jinsi anavyomkumbuka.

Lulu aliachiwa kwa dhamana mwezi January mwaka huu baada ya kukaa mahabusu kwa takriban miezi minane kufuatia kukamatwa kwa kuhusika na kifo cha Kanumba.
Lulu ambaye hivi karibuni amekuwa akitweet mara kwa mara ameandika:

“Ulikuwa zaidi ya baba,kaka,mpenzi,mume,ndugu,rafiki….sitoacha kukulilia katika maisha yangu yote!!R.I.P daddy angu STEVEN KANUMBA.”

Akiambatanisha na picha ya Kanumba, Lulu ameongeza, “I will alwayz love u daddy angu!”