Monday, June 17, 2013

DR. MARY NAGU ANUSURIKA KUCHOMWA MOTO NA WAFUASI WA CHADEMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu pamoja na Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni (CCM), wamenusurika kuchomwa moto na wafuasi wa Chadema usiku wa kuamkia jana.

Tukio hilo lilitokea usiku wa manane, baada ya wafuasi wa Chadema, wakiongozwa na Mbunge wa chama hicho Jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse, kuvamia nyumba waliyokuwa wamefikia Nagu na Soni, katika Kata ya Bashnet, Babati Vijijini, mkoani Manyara.

Wafuasi hao wa Chadema wanawatuhumu Dk. Nagu na Soni kukutana katika nyumba hiyo kwa nia ya kupanga mipango ya kutoa rushwa ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata hiyo, unaotarajiwa kufanyika leo, ikiwa ni pamoja na maeneo mbalimbali nchini.

Chanzo cha MTANZANIA Jumapili kilichokuwa eneo la tukio kililidokeza gazeti hili kuwa Dk. Nagu na Soni

BAADHI YA PICHA KWENYE MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA

 Uwanja wa Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.
 atika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema na  Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema   hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara  tu baada ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, hali inayoashiria mrushaji huenda alilenga kuwajeruhi viongozi hao.

Miili ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuawa.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUKIO LA BOMU ARUSHA


MKASA MZIMA KUHUSU KUPIGWA KWA MBUNGE NASSARI KATIKA KITUO CHA KURA MAKUYUNI

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na  kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi, kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.

"Lakini tulipofika hapo tulimkuta raia mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni...

"Huyo Baba alihamaki, akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma akaanguka damu ikaanza kumtoka puani...

"Baada ya hapo,tukalazimika kuingilia kati na kuondoka na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa Minjingu,