Tuesday, November 27, 2012

Ziara Ya Kiserikali Ya Rais Wa Zanzibar Dk Shein Nchini Vietnam

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili katika Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali.
 Baadhi ya Viongozi wa Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,wakiwa katika mkutano na ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara maalum ya Kiserikali nchini humo.
 Balozi wa Tanzania nchini China ambae anawakilisha Vietnam Philip Sang’ka Marmo,(kutoka kushoto) Waziri wa Kilimo na Maliasili Suleiman Othman Nyanga,na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Mohamed Ramia,wakiwa katika Mkutano na Uongozi wa Chuo cha Uvuvi wa Samaki na Ufugaji katika Jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakipata maelezo walipotembela katika mabwawa ya ufugaji wa Samaki katika Chuo cha Uvuvi wa Samaki na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakiwa na mazungumzo na Do Quang Sang,(kulia) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni ya Bidhaa za Baharini,wakiwemo Samaki,Kamba pia usindikaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akiangalia Samaki na Kamba waliokiwisha sindikwa ikiwa ni tayari kwa usafirishaji, alipotembelea katika kiwanda cha (Quang Ninh Sea Products Import Export Company) katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,(kushoto) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni kampuni hiyo, Do Quang Sang,(katikati) Nguyen Ha Dieu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Do Quang Sang,Mwenyekiti pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Import Export inayosindika na Bidhaa za Baharini katika Jimbo la Quang Ninh Mjini Halong Nchini Vietnam,baada ya kutembelea Kampuni hiyo,akiwa katika ziara ya Kiserikali.

Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

NAPE AWAKILISHA CCM KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MSANII WA BONGO MOVIES, JOHN MAGANGA

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salamu za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa msanii, John Maganga, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam leo.
 Msanii wa Bongo Movies,  Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movies, marehemu  John Maganga leo.
 Wasanii wa Bongo Movies wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba (kulia).

(Picha na Bashir Nkoromo)

Magazeti ya leo Jumanne 27th November 2012