Friday, May 17, 2013

CD ZA UAMSHO NA ZILE ZA SHEIKH ILUNGA ZAPIGWA MARUFUKU....

Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamu  wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi CD  zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.

Agizo hilo lilitolewa na OCD  wa  zamani Murtad MKADAM ambae kwa  sasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif.

Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam.

OCD alibainisha kuwa mpaka sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha  na  kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani serikali ina mkono mrefu. ...

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.

SERIKALI YAAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI VIONGOZI WA WIZARA YA ELIMU WALIOSABABISHA UBOVU WA MATOKEO YA FORM FOUR

                                                                      Mizengo Pinda.
Serikali imeahidi kuwajibisha watendaji watakaobainika kwenda kinyume katika uingizaji wa mfumo mpya wa usahihishaji mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, ambao matokeo yake yamefutwa.

Akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kinachosubiriwa sasa, ni maelezo ya kina ya Tume ya Taifa aliyoiunda kuchunguza matokeo hayo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tume hiyo haijakamilisha kazi yake,  lakini muda si mrefu itakuwa imekamilisha na kuwasilisha maelezo ya kina yatakayoipa Serikali majibu kwa maeneo yote.

“Tusubiri kidogo, muda si mrefu tutakuwa tumekamilisha kazi …na kama wapo watu waliosababisha jambo hili, wala haitakuwa tatizo hata kidogo kuchukua hatua za kuwawajibisha. Ni dhahiri kwamba suala hili si dogo,” alisema Waziri Mkuu.

Majibu hayo ya Pinda yalitokana na maswali ya Mbunge Sakaya, ambaye alisema uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo kutokana na kubainika kulikuwa na mabadiliko ya upangaji wa alama bila kuandaa wanafunzi, si jambo dogo.

Beckham astaafu soka, amfuata Sir. Ferguson

Dili la kustaafu lazidi kuitikisa nchi ya Uingereza baada ya magwiji wa soka na kocha maarufu kustaafu kufundisha soka.

 Wiki moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID BECKHAM ametangaza kutundika daluga.

Beckham mwenye umri wa mika 38, ameisadia Paris Saint-Germain PSG Kutwaa mwari wa Ligue 1 nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19 mwishoni mwa wiki iliyopita Pamoja na kupewa ofa ya mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huu .

Alisema: “Shukrani sana kwa PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”

Beckham alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid. Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer. Chanzo: Baraka Mpenja

Tiketi za simba na yanga kuanza kuuzwa leo

TIKETI kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga litakalochezwa kesho (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza kuuzwa leo (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Vituo vitakavyouza tiketi hizo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, OilCom Ubungo, kituo cha mafuta Buguruni, BMM Barbershop Sinza Madukani, Dar Live Mbagala na Sokoni Kariakoo.

Tiketi hizo zitakuwa zikiuzwa katika magari maalumu yaliyoegeshwa katika vituo hivyo. Viingilio katika mechi hiyo ya kufunga msimu ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani, sh. 7,000 viti vya bluu, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B n ash. 30,000 kwa VIP A. Chanzo: TFF