Saturday, October 13, 2012

Magazeti ya leo Jumamosi 13th October 2012

Mali na kanisa zachomwa Moto na waislam mbagala

                                                    Mlango ukiwa umevunjwa vioo na mawe
                                                              Katika madhabahu,pameharibiwa

                                                Mabenchi yamepinduliwa na kuvunjwa
                                                             Mimbari imechomwa na kuharibiwa


                                                             Ofisi ya Kanisa imechomwa moto

                                         Wachungaji wa kanisa hili wakisubiria taarifa kutoka polisi
                           Waumini wanafanya maombi wakiwaombea waislamu mungu awasamehe
                                                      Vifaa vya uimbaji vimechomwa moto
                                                   Washarika wakiwa kanisani kwaowakitafakari
                                                 Gari la mchungaji pia limeharibiwa kabisa

                                         Ofisi ya mchungaji na mwinjilisti zimeharibiwa kabisa
Kushoto ni msikiti walipotokea waislamu kabla ya kuvamia kanisa kulia.nyumba hizi za ibada ziko jirani zikitenganishwa na barabara tu

Hali ilivyokuwa Jana Mbagala jijini Dar es Salaam Udini Watawala




Vurugu kubwa zatokea Mbagala, jijini Dar es Salaam zenye mtazamo wa kidini, ambapo makanisa matatu yanadaiwa kuchomwa moto.

Kamanda Wa Polisi Mwanza Auawa

Habari za uhakika zinadai kwamba kamanda Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi usiku maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza. Chanzo: Mwandishi Fredrick Katulanda, Mwanza

Askari Polisi Wapewa Zawadi

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Stanslaus Mulongo akimkabidhi cheti cha utendaji bora wa kazi askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (ACP) Jane Warioba wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa michezo uliopo katika kambi ya polisi ya mjini Arusha tarehe 08/10/2012. (Picha zote na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa askari 37 wa mkoa huo waliofanya vizuri zaidi katika utendaji wao wa kazi za kila siku. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 08/10/2012 katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi ya jeshi hilo iliyopo mjini Arusha.
 Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti na fedha taslimu TSh 100,000 kila mmoja kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila siku.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ili aweze kutunuku vyeti na fedha taslimu TSh 100,000 kwa kila askari ambaye alikuwa amefanya vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi zilizopo mkoani humo. Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimtambulisha viongozi hao.