MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa
jina la Mzee wa Upako ametamba kwamba yeye ni tajiri tishio kuliko
watumishi wenzake kwani anamiliki magari sita ya kifahari na nyumba
ambayo ina kiyoyozi (AC) Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako'.
Akihubiria waumini wake kanisani hapo juzikati, Ubungo- Kibangu,
jijini Dar es Salaam na kuoneshwa na Kituo cha Runinga cha C2C na
Channel Ten hivi karibuni, Mzee wa Upako alisema magari yake hayo ya
kifahari yote yana viyoyozi na si ya kutoka Japan, akimaanisha ya
gharama kubwa zaidi.
“Mimi ndiye Mzee wa Upako, nikitoka nje nakuta
magari yote sita yapo, nachagua leo niendeshe hili au lile. Najiambia
hapana hili nililiendesha jana, nachukua lingine,” alitamba kiongozi
huyo.
Range Rover Vogue.
“Inawezekana vipi mabomu yapigwe madhabahuni
halafu wewe kama mtume na nabii usifanye jambo lolote la Kimungu dhidi
ya waliofanya kitendo kile madhabahuni?” alihoji Mchungaji Lusekelo.
Alidai
kuwa kuna mitume hapa nchini kazi yao ni kugombania ardhi. “Kama kweli
wewe ni mtume na nabii halafu unagombania ardhi ya mashamba na Wazaramo,
huo ndiyo utume tulioitiwa? Ndiyo maana hata serikali haitutambui,”
alisema Mzee wa Upako huku akishangiliwa na waumini wake.
Ford Escape.
Wachambuzi wa mambo wameichambua hesabu hiyo na
kugundua kwamba mchunga kondoo huyo hutumia zaidi ya shilingi 25,000,000
kwa mwezi kulipia vipindi hivyo.
Kiongozi huyo ana kanisa kubwa la
ghorofa Ubungo Kibangu na mabasi makubwa kadhaa ambayo hutumika
kuwasomba waumini bure kutoka Barabara ya Mandela hadi kanisani kwake.
Hivi
karibuni Mzee wa Upako amewahi kuwakemea wachungaji wenzake wa makanisa
ya kiroho kwa kujitajirisha kwa kujiita manabii na mitume akidai kwamba
kufanya hivyo ni kuwatapeli waumini.
Land Rover Discovery.
“Magari yote nimeandika kwa jina langu ili niyalipie kodi, situmii mwamvuli wa kanisa kwa kukwepa kodi.”
Aliwaambia
waumini wake kuwa kazi yake ni kugawa upako wa baraka za utajiri na
kwamba kupitia kanisa lake watu wengi wameneemeka kimaisha.
“Nasisitiza
kuwa kila mtu anatakiwa kuwa tajiri lakini utajiri wa halali siyo ule
wa kudhulumu, ndiyo maana nasimama hapa kutaja mali zangu, magari hayo
si mali ya kanisa ni yangu,” alisema.

BMW X5.
Pia aliyachambua makanisa kwa kusema: “Makanisa yetu haya
ya kiroho ni hovyo, wameingia matapeli na ninayasema haya kwa kuwa
ninayajua, nipo ndani, ndiyo maana najua kitu ninachokisema na mtu
akitaka tubishane kwa hoja hii hawezi kunishinda.
“Najua hili
ninalozungumza ni jambo zito na sasa ninaposema haya maneno ni sauti ya
Mungu mwenyewe inatoka kupitia kinywa changu.”
Mzee wa Upako aliwahi
kusema kwamba amekuwa akitumia zaidi ya shilingi 300,000,000 kwa mwaka
kwa ajili ya kuendesha vipindi vyake katika runinga na fedha hizo
huchangisha kupitia akaunti zake, akasisitiza vipindi vya runingani ni
mali yake na si kanisa.
Mercedes Benz.
Aliyataja magari hayo kuwa ni Mercedes Benz, Land
Rover Discovery, Range Rover Sport, BMW X5, Ford Escape na Range Rover
Vogue ambayo Uwazi linatafiti bei zake na kuwapelekea wasomaji siku
zijazo.
Aidha, mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kutamba kuwa
nyumbani mwake mna viyoyozi ‘vikali vya kufa mtu’ na kubainisha kwamba
huwa akitoka kwenye gari lenye kiyoyozi anaingia katika nyumba yenye
kiyoyozi.
“Mimi nasema hayo kwa sababu ni mlipaji mzuri wa kodi za
serikali, sioni sababu ya kuficha mali zangu, kwa nini nifiche?” alihoji
na kuongeza:
* MAGARI YANAYOONEKANA PICHANI JUU NI MIFANO YA MAGARI ANAYOMILIKI MZEE WA UPAKO.