Tuesday, October 2, 2012
AJALI HII IMEPOTEZA NDUGU ZETU
AJALI MBAYA IMETOKEA MBALIZI MBEYA AMBAPO MAGARI MAWILI YALIGONGANA NA KUWAKA MOTO, WATU 10 WANARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEMO KATIKA AJALI HIYO, KATIBU WAKE AMETEKETEA KWA MOTO.
Dar Express Lateketea kwa Moto leo
Basi la Dar Express kutoka Arusha kwenda Dar linateketea kwa moto eneo la Segera. hakuna abiria aliyepoteza maisha zaidi ya mizigo yote kuteketea kwa moto.
chanzo Tone Radio-Tz
chanzo Tone Radio-Tz
MELI MPYA YA KISASA YA AZAM MARINE YENYE UWEZO WA KUBEBA ZAIDI YA WATU 1000 NA MAGARI 200 YAWASILI NCHINI
Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.
Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar
Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.
Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratibu za mamlaka mbalimbali.
Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.
Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari.
Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.
Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.
Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.

MBUNGE WANGU MH. EDWARD LOWASSA ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NAFASI YA UJUMBE WA HALMASHAURI KUU WILAYA YA MONDULI.
Waziri mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,mh. Edward Lowassa
akipongezwa mara baada ya kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa
nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya Wilaya ya Monduli uliofanyika leo
katika ukumbi wa chuo cha ualimu Monduli,Mh Lowassa ameshinda kwa
kishindo kwa kuwabwaga wapinzani wake kwa idadi ya kura 709,mpinzani
mwingine ameta kura 44 na mshindi mwingine aliibuka na kura 7.
Mh Lowassa akizungumza na kuwashukuru wapiga kura wake waliompatia ushindi wa kishindo

RUFAA YA LEMA Yaendelea Kusikilizwa
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), inazilikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande.
Majaji wengine waliopo katika kusikiliza rufaa hiyo inayovuta hisia za watu wengi ni pamoja na Jaji Natalia Kimaro na Salum Massati, wote wa Mahakama ya Rufaa nchini.
Rufaa hiyo ambayo ilipaswa kusikilizwa Septemba 23, mwaka huu, ilisogezwa mbele hadi Oktoba 2, kutokana na mawakili wa pande zote mbili kupatwa na dharura, ambapo jopo hilo liliridhika na hivyo kusogeza mbele tarehe.
Jopo hilo lilizingatia barua iliyoomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, kutokana na mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji kufiwa na baba yao mzazi.
Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), anashirikiana na Wakili Mwandamizi Method Kimomogoro katika kumtetea mrufani, Godbless Lema.
Kwa upande wake Wakili Mughwai anashirikiana na Wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa katika shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo.
Wanachama hao walifungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, kwa kutumia lugha za matusi.
Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha katika mahakama hiyo hoja 18 za madai, akipinga ubunge wake kutenguliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Katika baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, huku akiitaka mahakama hiyo imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.
Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na gharama za kesi iliyomalizika katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Chanzo: Mtanzania

Watoto Wa Wassira Kujiunga CHADEMA; Ufafanuzi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU
Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA.
Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote.
Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu.
Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).
Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola.
Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Lilian Wasira 0719 604156 Esther Wasira 0655 048797

Subscribe to:
Posts (Atom)