Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi za Jumuiya uchumi na
maendeleo ya Kusini (SADC) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha
ikulu Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini ili kushiriki kikao cha
kamati hiyo.Pembeni ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete(watatu kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika
ikulu jijini Dar es Salaam leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni
Rais Wa Namibia Hifikepunye Pohamba, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya
kusini(kulia) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dr.Tomaz Salomao
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete( Wanne Kushoto) akiwa na viongozi SADC waliopo katika kamati hiyo.Wengine katika picha ni Rais Wa Afrika ya Kusini Jackob Zuma(Watatu kushoto), Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia(kulia),Rais Mstaafu wa Msumbiji ambaye pia ni msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Madagaska, Joachim Chissano(wapili kushoto) na kushoto ni Katibu mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao
(Picha na Freddy Maro).
Friday, December 7, 2012
Mnyika Mbunge Rasmi Ubungo
Mbunge wa Ubungo John Mnyika sasa ni mbunge rasmi wa Ubungo,baada ya Hawa Ng'umbi Kufuta rufani yake bila gharama.
Picha Ya Fullshangwe
Picha Ya Fullshangwe
CCM Iringa Wajitabiria Ugumu Uchaguzi Ujao
CHAMA Cha Mapinduzi mkoani Iringa, kimeshitshwa na taarifa ya Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani humo kuwa baadhi ya barabara zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa zingetengenezwa kwa kiwango cha lami kama angechaguliwa, hazijatengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.
Katibu wa CCM mkoani humo Emanuel Mteming’ombe, alisema hatua hiyo inakihatarisha chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 hasa ikizingatiwa kuwa Rais Kikwete atakakiwa kumnadi mgombea wa urais kupitia chama hicho.
“Hii ni hatari kama barabara hizo hazitatengenezwa na kukamilika, jambo hili litatusumbua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa sababu Rais atatakiwa kumnadi mgombea wetu na wananchi watauliza maswali hayo ya ahadi za barabara, ”alisema Mteming’ombe.
Hata hivyo Mteming’ombe alimpongeza Meneja wa Tanroads mkoani humo, Mhandisi Paul Lyakurwa kwa jitahadi za kuhakikisha kuwa barabara hizo zinatengenezwa.
Pia aliishauri Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Iringa iliyoketi chini ya mwenyekiti wake Dk Chritine Ishengoma akuihimiza Serikali kutekeleza ahadi hizo.
Akitoa taarifa ya utekeleza wa ahadi za Rais Kikwete katika kikao hicho, Lyakurwa alisema barabara kadhaa ambazo ujenzi wake uliandaliwa mwaka wa fedha wa 2011/13 umesimama kutokana na kutotengewa fedha katika bajeti ya mwaka 2012/13.
Alizitaja barabara hizo kuwa ni ya Rujewa, Madibira Mafinga yenye urefu wa kilometa 151 ambayo alisema upembezi yakiniufu ulishakamilika na kinachosubilrwa ni kupata mkandarasi.Mhandis Lwakurwa alizitaja barabara nyingine kuwa ni ya Ipogolo- Kilolo.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari

Wakili: Korti Ilikosea Kumvua Lema Ubunge
WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.
Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.
Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuini kuwepo kwa dosari za kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufaa.
Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine ya kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo, amri ambayo aliitekeleaza.
Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.
Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.
Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge.
Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa Jaji Nathalia Kimaro.
Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.
Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema), akisaidiana na Wakili Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu rufani ambao ni makada wa CCM.

Familia Ya Sharo Yaibua Mazito
FAMILIA ya msanii Hussein Ramadhani Mkiety (Sharo Milionea) aliyekufa katika ajali wilayani Muheza wiki
iliyopita imedai kuwa haiamini kwamba kifo cha mtoto huyo kilitokana na ajali, hivyo kulitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kubaini ukweli.
Mjomba wa marehemu , Mohamed Msenga alisema jana kwamba familia imekuwa na shaka juu ya mazingira ya kifo hicho baada ya kurejeshewa nguo za msanii huyo zilizokuwa zimeibwa baada ya ajali lakini hazikuwa na damu.
Msenga alisema muda mfupi baada ya mama mzazi wa Marehemu Zaina Mwaimu Mkiety (54), kuitwa polisi na kukabidhiwa vitu mbalimbali zikiwamo nguo ambazo marehemu alikuwa amevaa siku ya ajali hawakuona hata alama ya damu jambo ambalo liliwashangaza.
Alisema shaka hiyo ilianzia katika eneo ambalo ajali hiyo ilitokea akisema walipofika na kuonyeshwa mahala alipokuwa ameangukia, hawakuona damu jambo ambalo liliwatia shaka.
Alisema begi la nguo za msanii huyo lilikuwa na udongo mwingi likionyesha kwamba walioiba walikuwa wamelifukia kabla ya kusalimisha lakini hakuna damu zilizoonekana.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Teule Muheza, Dk Julius Mjema aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Sharo Milionea alisema sababu ya kifo chake ni kichwa kupondeka.
“Mimi ndiye niliyefanyia ‘postmoterm’ (uchunguzi), mwili wa Sharo Milionea, ni kwamba kichwa kilikuwa kimepondeka huku mifupa ya kichwa ikiwa imepondeka pia,” alisema Dk Mjema.
Kuhusu madai ya nguo kutokuwa na damu, alisema marehemu alipata mpasuko wa ndani kwa ndani na siyo wa nje, ndiyo maana alipofikishwa chumba cha maiti damu zilionekana zikiwa zimeganda masikioni.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alipoulizwa kuhusu madai hayo ya familia alisema: “Hiyo ni taarifa ambayo jeshi la polisi litaifanyia kazi kwa kuingia kwa kina katika kuchunguza ili kuridhisha pande zote.”
Mama yake alia kukosa mjukuu
Katika hatua nyingine, mama mzazi wa msanii huyo amesema kutoachiwa mjukuu na tarehe za mwisho wa mwezi ni alama ambazo zitasababisha awe akimkumbuka mwanaye huyo milele. Akizungumza nyumbani kwake, katika Kitongoji cha Jibandeni Kijiji cha Lusanga wilayani hapa alisema kila ulipokuwa ukifikia mwisho wa mwezi ulikuwa ni muda wake wa neema kwani Sharo Milionea alimtumia fedha za matumizi yake binafsi pamoja na familia nzima nyumbani hapo.
“Pamoja na kwamba kila mara alikuwa akinitumia fedha za kutatua shida zangu mbalimbali nilizokuwa nikimweleza lakini kila mwisho wa mwezi alikuwa akihakikisha anatuma fungu la matumizi yangu na ndugu zake hapa nyumbani,” alisema mama huyo. Alisema mwisho wa mwezi itakuwa ni alama ya kudumu ya kumbukumbu ya mwanawe kwa sababu ni wakati ambao alikuwa akimtumia fedha za matumizi yake pamoja na familia nzima.
Kuhusu mjukuu alisema: “Sharo ni mwanangu wa pekee wa kiume, amekufa bila kuniachia mjukuu.. hii inaniuma sana lakini namshukuru Mungu kwani amechukua kiumbe chake na ndiye ajuaye siri iliyofichika mbele yangu,” alisema.
Alisema hadi alipofariki hakuwahi kumdokeza juu ya kuwa na mtoto wala kumpa mimba msichana yeyote... “Unajua Sharo Milionea alizaliwa pacha na mwenzake Hassan lakini mwenzake alifariki dunia siku tano baada ya kuzaliwa kwa hiyo katika kizazi changu mwanangu pekee wa kiume alikuwa Sharo Milionea ambaye nilitumaini kwamba angeniletea wajukuu,” alisema Zaina.
Na: Burhani Yakub, Muheza

BABA ANAETUHUMIWA KUZINI NA KUZAA NA MWANAE WA KUMZAA ATINGA MAHAKAMANI BAADA YA KESI KUAIRISHWA AZOMEWA NA KINA MAMA NA KUKIMBIA KAMERA ZA WANDISHI WA HABARI
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf
Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(16) jina lake
limehifadhiwa. akiingia mahakamani leo mbele yake ni mke wake na mtoto
wake aliyezaanae ambao sura zao tumefunika
Bwana Yussuf Hamad anaetuhumiwa kuzaa na bintie akitaka kumpokonya kamera mwandishi wa gazeti la majira Rashid Mkwinda ili asimpige picha
Jamaa kuona amezidiwa akaamua kujifunika na shati lake huku akitoa maneno makali kuwa nyie waandishi mmekosa cha kuandika mmeona hii ndiyo habari hakuna habari nyingine? alihoji mtuhumiwa huyo
Huyoooo anatoka nje ya mahakama
Sasa anavaa kofia yake ili watu wasimtambue huku akisema nifuateni niwaonyeshe kazi
Njooni sasa huku kashika jiwe

Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
daktari ambaye alithibitisha kuwa binti huyo ana ujauzito.
Binti huyo amejifungua mtoto wa kike ambae sasa anamiezi mitatu mtoto huyo kaletwa leo mahakamani kama ushahidi kesi hiyo imeairishwa mapaka tarehe 12/12 mwaka huu,
http://mbeyayetu.blogspot.com/

Thursday, December 6, 2012
Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite akutwa amekufa hotelini
MFANYABIASHARA wa madini aina ya Tanzanite mkoani Arusha,Ngerii Olerumwa anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ndani ya hoteli ya Premier Palace ambayo timu ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano imeweka kambi hotelini hapo jijini Arusha.
Maiti ya mfanyabiashara huyo iligundulika majira ya saa 3 ;30 asubuhi leo mara baada ya mhudumu wa hoteli hiyo kugonga kwa muda mrefu mlango wa chumba alichokuwa amefikia marehemu huyo bila mafanikio na kisha kubaini alikuwa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo meneja wa hoteli hiyo ambaye alikataa kutaja jina lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo aliwasili hotelini hapo mnamo desemba 3 mwaka huu majira ya saa 1 ;00 jioni na kukodi chumba kimojawapo hotelini hapo.
Meneja huyo akisimulia tukio hilo alisema kwamba marehemu aliwasili akiwa peke yake hotelini hapo na kubainisha kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kukodi chumba hotelini hapo.
Hatahivyo,alidai kwamba ilipotimu leo majira ya saa 3 ;30 asubuhi wakati mhudumu wa hoteli hiyo akigonga mlango wa chumba alichofikia marehemu kwa lengo la kufanya usafi mlango huo haukuweza kufunguliwa kwa wakati hali iliyowapelekea kufanya juhudi za kuufungua mlango huo kwa lazima.
Alisema kwamba baada ya kufanikiwa kuufungua mlango huo walijaribu kumwamsha marehemu lakini hakuweza kuamka hali iliyowapelekea kuliarifu jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.
Mwandishi wetu ilipofika maeneo ya hoteli hiyo iliwashuhudia askari wa upepelezi kutoka jeshi la polisi mkoani hapa wakichukua maelezo kwa baadhi ya watumishi wa hoteli hiyo wakiwemo walinzi wa hoteli hiyo huku baadhi ya wabunge wanaounda timu ya wabunge wa bunge la jamhuri wakitaharuki kutokana na tukio hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndugu wa marehemu ambao walikusanyanya nje ya hoteli hiyo walisema kwamba wameshtushwa na kifo cha ndugu yao na wanahisi kwamba aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha huku wakilitaka jeshi la polisi kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.
Akihojiwa na waandishi wa habari kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas,alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kwamba jeshi lake linachunguza kwa kina kifo hicho.
Sabas,alisema kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya mkoa ya Mt,Meru na atatoa taarifa kamili ya tukio hilo kuanzia leo mbele ya waandishi wa habari.

PRECISION AIR YAZINDUA NDEGE YAKE MPYA AINA YA ATR 42-600
Waziri wa Uchukuzi (wa tatu pichani) kutoka kulia, Mh.Dkt Harisson
Mwakyembe akikata keki kuashiria uzinduzi wa ndege yao mpya aina ya ATR
42-600, kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar, kulia kwake ni
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Michael Shirima na shoto kwake ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Alfonse Kioko kwa pamoja
wakishuhudia tukio hilo adhimu.
Waziri wa Uchukuzi (wa tatu pichani) kutoka kulia, Mh.Dkt Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Shirika la Ndege la Precision, wakati wa uzinduzi wa ndege yao mpya aina ya ATR 42-600.
Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa ndege hiyo mpya aina ya ATR 42-600 wakiipanda.
Precision Air yazindua ndege yake mpya aina ya ATR 42-600.
.Yaanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kilimanjaro
.Hatua hiyo ni miongoni mwa mwendelezo wa uboreshaji wa huduma zake
Shirika la Ndege la Precision limezindua ndege yake mpya aina ya ATR 42-600, ikiwa ni hatua ya mwendelezo wa maboresho ya miundombinu ya shirika hilo kwa maslahi ya wateja wake. Hata hivyo uzinduzi huu ni sehemu tu ya mkakati wa miaka mitatu, ambapo katika kipindi hicho, shirika limepanga kuongeza aina kama hii ya ndege za (ATR) hadi kufikia idadi ya ndege 5, mradi utakaogharimu kiasi cha Dola milioni 95.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Michael Shirima, alipongeza hatua ya uzinduzi huo, ambapo alisema itasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mapinduzi katika sekta ya usafirishaji wa anga. “Ndege hii mpya na ya kisasa ya ATR 42 - 600 ina zaidi ya viwango vinavyohitajika katika huduma ya usafiri wa anga, ina muundo wa kipekee uliotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, na inaweza kufanya huduma zake hata kwenye maeneo ya miundombinu duni,” alisema Shirima.
Katika mwendelezo wa uboreshaji wa huduma zake, Precision imeendelea kupeleka ndege zake ndogo mikoani na kuahidi kuendeleza azma yake ya kuwa kitovu cha utoaji wa huduma bora za anga nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Alfonse Kioko, alisema upanuzi wa wigo wa huduma za anga katika shirika hilo, ni miongoni mwa mikakati ya kuhakikisha wateja wake wanafurahia ufanisi na huduma za usafiri huo, sanjari na kupunguza adha na usumbufu kwa wateja . “Ni fahari kubwa kwa Tanzania kupitia shirika la ndege la Precision kuwa taifa la kwanza katika bara
la Afrika kuingiza ndege hii ya kisasa na iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu,”alisema Kioko.
“ATR 42-600 inakidhi matakwa na mazingira ya ukuaji wa miundombinu katika maeneo mengi barani Africa jambo ambalo linatupa hamasa ya kuongeza masafa na uboreshaji wa huduma zetu katika hali ya ufanisi zaidi.” Precision Air ina wigo mpana na imejiimarisha zaidi katika kuhakikisha inafikisha huduma zake katika mikoa yote. Shirika hilo ni la kwanza kati ya mengi yaliyopo nchini, kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam, DSE.
Aina hiyo ya ndege itasaidia kupanua wigo wa usafiri wa anga unaofanywa ndani ya shirika hilo kwa safari za ndani na nje ya Tanzania. Hata hivyo shirika liko mbioni kuanzisha safari zake katika mikoa inayokua kwa kasi kama Mtwara.
“Maeneo mengine tunayoyatazama ni mkoa wa Mbeya punde tu uwanja wake mpya utakapozinduliwa mwakani, Bukoba na Kigoma ambapo viwanja vyake bado vipo kwenye matengenezo.”

DAKTARI WA ‘MOI’ MUHIMBILI, NESI WAKE MBARONI KWA RUSHWA
Daktari Matiko (katikati) akiongozwa na Afisa wa Takukuru (nyuma yake). Aliyetangulia ni wakili anayemtetea, Paschal Kamala.
…Akielekea kizimbani kwa upole.
Nesi KImwomwe (kulia) naye akielekea kizimbani kusomewa mashitaka yake.
Uchungu wa safari ya kuelekea kizimbani.
Ndugu na jamaa wakifuata nyuma kwa ajili ya kusikiliza kesi za wapendwa wao.
DAKTARI wa hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI), Deodata Kisasi Matiko (30) na nesi wake, Erick Petro Kimwomwe (28), leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakishitakiwa kwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja waliyomwomba Stanford Aaron Mhina ili wamfanyie upasuaji wa mgongo ndugu yake aitwae Fanuel Daniel Gideon aliyelazwa Wodi ya Sewa Haji namba (18) Kitengo cha Mifupa (MOI). Imedaiwa kuwa mgonjwa huyo alipelekwa MOI baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani ambapo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Kibaha na kuvunjika mgongo.
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

HAPPY BIRTHDAY JACQUELINE WOLPER
MSANII Jacqueline Wolper ambaye pia ni Ijumaa Sexiest Girl 2012, leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Wolper alizaliwa mkoani Moshi Desemba 6, mwaka 1988 na leo ametimiza umri wa miaka 24. Mtandao huu unamtakia kila la heri katika siku hii muhimu katika maisha yake. Happy Birthday Jaque!
Wananchi Watembelea Banda La Tume Ya Katiba
Mkazi wa Jijini la Dar es Salaam, Bw. Joseph Msindai akizungumza na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Amour Kagya (kulia) katika banda la Tume hiyo leo (alhamisi Disemba 6, 2012) wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA TUME YA KATIBA)
(PICHA NA TUME YA KATIBA)
Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI
Ndugu wapendwa, DSM City Press Club imepata taarifa za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club (DCPC). Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia. Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani, wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili apone majeraha
Walimu Wakimbia Shule Kwa Kubakwa Na Wanafunzi
WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.
Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.
Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.
“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.
Mwalimu huyo alidai kuwa walimu: http://www.mwananchi.co.tz/

Subscribe to:
Posts (Atom)