Saturday, May 11, 2013

ASKARI ALIYEMUUA MTOTO MDOGO WA RISASI AKAMATWA......CHADEMA WAANDAMANA, POLISI YAJIBU MAPIGO

ASKARI Polisi wa Kituo cha Tarime mkoani Mara mwenye namba D. 4662 Koplo Mathew, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kifo kwa risasi cha mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Rebu, Deus Jacob (9).

Kifo hicho kilitokea wakati polisi wakiwa kwenye harakati za kukamata mtuhumiwa, Marwa Bisara, mkazi wa kitongoji cha Songambele kata ya Sabasaba mjini hapa, aliyekuwa akituhumiwa kwa shambulio na kudhuru mwili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime/Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kitongoji cha Songambele, baada ya Koplo Mathew na askari wenzake wakiwa na mlalamikaji, wakifuatilia mtuhumiwa na kumkuta na wenzake katika pagala wakivuta bangi.

Wakati polisi wakijiandaa kumkamata, mtuhumiwa Bisara alimvamia Koplo Mathew akitaka kumnyang'anya bunduki na katika purukushani hiyo, risasi zilifyatuka na moja kumpata Deus kichwani na kumuua papo hapo baada ya kichwa kufumuka.

WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI KUHUSU ZOEZI ZIMA LA KUYAPITIA UPYA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya   Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha  Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili  Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka   iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka  aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

PONDA AANZA UCHOCHEZI TENA....ANATAKA SERIKALI IANZE KUUA WAKRITO NA AMEDAI NECTA HUWAFELISHA WAISLAMU

Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho.

Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!

KAULI ZA SHEIKH PONDA.

Habari Zilizopo Magazetini leo Jumamosi 11st May 2013





Friday, May 10, 2013

LADY JAYDEE AFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI.....JOTO LIMEPANDA NA ANAMUOMBA MUNGU ASIKAMATWE MAY 31

Bado joto ya show ya mika 13 ya Lady JayDee inazidi kupanda kutokana na mengi yanayohofiwa kutokea siku hiyo.

Kwanza kulikuwa na tetesi kuwa huenda Clouds Fm wakafanya show nyingine siku hiyo, kitu ambacho Ruge Mutahaba alikifafanua vizuri kwa kusema mtu ukiwa na shughuli haimaanishi kuwa wengine wasifanye shughuli nyingine kama hiyo.

Lakini sasa kuna jingine ambalo limejitokeza, na amelisema mwenyewe Lady JayDee....

Kupitia akaunti yake ya Twitter Jide ameandika:

“Nimepata taarifa zisizo rasmi kuwa nimefunguliwa kesi mahakamani natumaini sitaitwa kizimbani tar 31 May ambayo ndio siku ya show.”

WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU KANISANI WAZIKWA KWA HUZUNI KUBWA

Misa ya Mazishi ya wahanga wa mlipuko wa bomu la Jumapili iliyopita kwenye parokia teule ya Olasiti ilianza katika eneo lile lile mlipuko ulipotokea.

Misa  hiyo  iliongozwa na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Maandamano yalianzia toka chumba cha kuhifadhia maiti, miili ikapelekwa makao makuu ya Asofu Mkuu, Burka  na  baadaye  ikawasilishwa kanisani .....

Mahubiri ya Kardinali Pengo
Ndugu zangu,

Nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo.

Mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema. Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Magazeti ya leo Ijumaa Ya 10th May 2013




HAYA NDO MAJINA 9 YA WATUHUMIWA WALIOLIPUA BOMU KANISANI ARUSHA

Imeripotiwa kuwa jumla ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Ripota wa WAPO FM radio alisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-

    1- Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    2- Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    3- George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)
   4-  Mohammed Suleiman Said (38, mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, aliyewafuata kwa gari binafsi washukiwa wa ugaidi kutoka kiwanja cha ndege na kuwepeleka hadi hoteli ya Aquiline iliyopo Arusha)
   5-  Said Abdallah Said (28, mkazi wa Abu Dhabi, Nchi za Falme za Kiarabu)
   6-  Abdelaziz Mubarak (30, Nchi za Falme za Kiarabu)
   7-  Jassini Mbaraka (29 mkazi wa Bondeni, Arusha)
   8-  Foud Ahmad (28, Nchi za Falme za Kiarabu)
   9-  Said Mohsen (Najran, Saudi Arabia)

Hata  hivyo, himaya ya Imarati, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE - United Arab Emirates)  inasema maafisa wake wamekanusha kuhusu raia wake watatu kuhusika na mlipuko wa bomu la Olasiti, Arusha.

Abu Dhabi ni mji mkuu wa Imarati (UAE), ambazo zina imirati saba -- Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Fujairah, Ras al Kaimah, Ajman na Umm a Quwain. Nchi jirani na UAE ni Qatar, Saudi Arabia na Oman.

Mapya bomu la Arusha:Majeruhi aeleza bomu lilivyokuwa

Bomu lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa lilitengenezwa kienyeji.

Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.

Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.

Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.

R.I.P ALL

Hali tulivu,baridi kiasi, majonzi yakiwa yametawala kila kona jijini arusha Tukiwasindikiza wapendwe wetu waliotangulia mbele ya haki siku ya jumapili 5/5/2013 katika mlipuko wa bomu kanisa la mtakatifu joseph olasiti.Hii ni chachu kwa wakristo wote Tanzania na dunia, sali kila sekunde uliyonayo kuombea AMANI nchi yetu.Mungu uwaangazie mwanga wa milele wapumzike kwa Amani Amina.

Thursday, May 9, 2013

Magazeti ya 9th May 2013




MTOTO WA MIAKA 9 AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI HUKO TARIME

Polisi mkoani Tarime wameua mtoto wa miaka 9, Deo Yakob, katika kilichoripotiwa kuwa pilikapilika za kukamata majambazi wanaoiba na kuua watu mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Bado hakuna maelezo zaidi, kuhusu ni kitu kani kilichopelekea mtoto huyo kuuawa katika juhudi za polisi kukamata majambazi hayo. Pia haijafahamika kama polisi hao walifanikiwa  kuwakamata majambazi...

Pichani ni wananchi wakiwa na mwili wa mtoto huyo ambaye alikua ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mturu, mjini Tarime.

Mlipuko wa Kanisani Arusha: saba wapelekwa dar kwa matibabu zaidi

 Wagonjwa saba ambao ni majeruhi wa mlipuko wa bomu kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi eneo la Olasiti jijini Arusha wamehamishiwa kwenye Hospitali za Muhimbili na LUgalo jijini Dar es Salaam.

Majeruhi hao wamesafirishwa mchana majira ya saa tisa kwa ndege ya shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwenda kuendelea na matibabu zaidi baada ya hali zao kuonekana bado zinahitaji vifaa vyenye uwezo wa hali ya juu.

Miongoni mwa walisafirishwa wapo watoto watatu wakike wawili na wakiume mmoja huu wakina mama walisafirishwa wakiwa wawili na kinababa wawili ambao hali zao bado mbaya licha ya matibabu walikuwa wakiyapata tokea juzi.

Wasamaria wema kutoka makampuni mbali mbali wameendelea kutoa misaada mbali mbali ya hali na mali ikiwemo madawa na vifaa tiba na mablanketi na mashuka,na Magodoro iliviisaidie hospitali za Mt.Meru na St,Elizabeth.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MIKUTANO YA DINI YENYE "VIRUSI" VYA UCHOCHEZI

Waziri wa MAmbo ya Ndani ya NChi, EMmanuel NChimbi, ameliagiza jeshi la polisi kuanzia IGP, RPC, OCD na OCS kuwachukulia hatua wale wote wanaoendesha mihadhara ya kidini yenye kuchochea vurugu na mifarakano katika jamii. ...

Nchimbi amesema kuwa kiongozi yeyote ambaye atabainika kutochukua hatua licha ya taarifa kuripotiwa kwake basi atakwenda na maji.. ...

Kauli  hiyo  ameitoa   jijini dar es salaam jana wakati akiongea na wawakilishi wa viongozi wa dini na vyombo jeshi la polisi mkoa wa dar es salaam

Waziri Nchimbi amewatahadhalisha vijana wanaoshinda kwenye mitandao na wanaotumia simu kutuma ujumbe wenye lengo la kuhamasisha chuki za kidini. Amesema kuwa kuanzia sasa serikali itachukua hatua   stahiki

Chanzo: taarifa  ya  habari ya TBC1

BRAKING NEWS: SHEIKH PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA CHA NJE

 Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam leo  imemuhukumu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kifungo cha nje cha mwaka mmoja, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru