Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,alipowasili katika Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji
katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika
Ziara ya kiserikali.
Baadhi ya Viongozi wa Chuo cha Uvuvi wa Samaki ikiwemo na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,wakiwa katika mkutano na ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara maalum ya Kiserikali nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini China ambae anawakilisha Vietnam Philip
Sang’ka Marmo,(kutoka kushoto) Waziri wa Kilimo na Maliasili Suleiman
Othman Nyanga,na Mshauri wa Rais Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Balozi Mohamed Ramia,wakiwa katika Mkutano na Uongozi wa Chuo
cha Uvuvi wa Samaki na Ufugaji katika Jimbo la Quang Ninh Mjini Halong
nchini Vietnam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(wa tatu kulia) akiwa na ujumbe wake wakipata maelezo
walipotembela katika mabwawa ya ufugaji wa Samaki katika Chuo cha Uvuvi
wa Samaki na ufugaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini
Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakiwa na mazungumzo na Do Quang Sang,(kulia) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni ya Bidhaa za Baharini,wakiwemo Samaki,Kamba pia usindikaji katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,akiwa katika Ziara ya kiserikali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akiangalia Samaki na Kamba waliokiwisha sindikwa ikiwa ni tayari kwa usafirishaji, alipotembelea katika kiwanda cha (Quang Ninh Sea Products Import Export Company) katika jimbo la Quang Ninh Mjini Halong nchini Vietnam,alipokuwa katika ziara ya Kiserikali,(kushoto) Mkurugenzi pia Mwenyekiti wa Kampuni kampuni hiyo, Do Quang Sang,(katikati) Nguyen Ha Dieu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akiagana na Do Quang Sang,Mwenyekiti pia Mkurugenzi wa Kampuni ya
Import Export inayosindika na Bidhaa za Baharini katika Jimbo la Quang
Ninh Mjini Halong Nchini Vietnam,baada ya kutembelea Kampuni hiyo,akiwa
katika ziara ya Kiserikali.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
Tuesday, November 27, 2012
NAPE AWAKILISHA CCM KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MSANII WA BONGO MOVIES, JOHN MAGANGA
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akitoa salamu za
Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es
Salaam leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa msanii, John Maganga, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam leo.
Msanii wa Bongo Movies, Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movies, marehemu John Maganga leo.
Wasanii wa Bongo Movies wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba (kulia).
(Picha na Bashir Nkoromo)

Monday, November 26, 2012
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe,Adhibitisha Ajali ya sharo Milionea
Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.
Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.
Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.
“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa nje kupitia kioo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.
Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.
Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alinusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam.
Tanzania Asilialive inatoa salamu za Pole kwa Familia, wasanii wa Filamu, Vichekesho na muziki nchini kwa Msiba huo mzito hasa ukizingatia kuwa bado wapo katika Msiba wa Mcheza filamu John Stephen anaetarai kuzikwa kesho Makaburi ya Kinondoni.

INATISHA; ANGALIA PICHA YA SHARO MILIONEA BAADA YA AJALI...
Inatisha lakini hatuna jinsi zaidi ya kuamini kuwa ni kweli imetokea....hivi ndivyo ajali ilivyochukua maisha ya Sharo millionea!... R.I.P Sharo Milionea!
Breaking News Sharo Milionea Amefariki
Ripoti Ya Nchi Maskini Sana Duniani Ya Mwaka 2012
RIPOTI YA NCHI MASIKINI SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA TARAKIMU
Geneva, 26 Novemba 2012 – Ripoti ya Nchi Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121, yenye kichwa kidogo cha habari Kutumia Fedha Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa Uzalishaji, imetolewa leo.
Mwelekeo wa uhamiaji
Ø Idadi ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs) iliongezeka kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010. Hii ni sawa na 3.3% ya wakazi wote wa nchi hizo.
Ø Nchi Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya wahamiaji duniani kote---idadi ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote duniani (12.1%).
Ø Wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha
Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni 3.5 kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi duniani.
Ø Mwaka 2011 kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na kutoka Kenya dola milioni 2.5.
Ø Mwaka 2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15), na kiwango hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi Kutoka Nje, yaani ODA (dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje ya nchi.
Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja mmoja kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30 kati ya mwaka 2000 na 2010.
Ø Fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs ikilinganishwa na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha zinazotumwa na raia kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea (ambazo siyo LDCs).
Ø Kuanzia mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo kinalingana na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
Ø Tangu mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za nje kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata kutokana na mauzo ya bidhaa nje.
Ø Kwa LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi kile cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi za Bangladesh, Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen. Kwenye nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.
Ø Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
Ø Duniani kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha fedha kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja (12%).
Ø Kama nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato yao yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2010.
Ø Asilimia 66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na 2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na Sudan.
Ø Matumizi ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi 1,000) kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha kutoka ng’ambo.
Kuhama kwa utaalam

Jamani katika Wasani aliyekuwa anakuja kwa kasi ni huyu atimae Hatunae tena Dunuani
John Maganga
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa akipanda juu kwa kasi, John Maganga (22) amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokimbizwa akiwa hoi, inasikitisha sana.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baba mdogo wa John, Deogratius Shija alisema Ijumaa iliyopita, marehemu alipatwa na maumivu ya ghafla ya tumbo, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu ya Mwananyamala, Dar ambako vipimo vilidai utumbo wa mgonjwa huyo ulitoboka.
Shija: “Daktari akatuambia kutokana na hali hiyo watamfanyia upasuaji ili kuuziba utumbo huo lakini mara baada ya zoezi hilo daktari akasema tatizo halikuwa kutoboka kwa utumbo bali kuna kitu kingine.
“Ikabidi tumkimbize Muhimbili ambako madaktari wa pale walituambia wenzao wa Mwananyamala walikosea kumfanyia upasuaji John kwani tatizo halikuwa la kufanyiwa upasuaji bali alitakiwa apatiwe dawa.
“Madaktari wakatuambia tumwache pale ili waokoe maisha yake sisi ndugu turudi asubuhi. Tulipokwenda asubuhi tukaambiwa mgonjwa wetu alifariki dunia usiku uleule. Imetuuma sana.”
Hivi karibuni, John aliandaa filamu yake ambayo aliipa jina la Beautfools ambayo yeye alicheza kama mume wa ndoa wa Aunt Ezekiel ambaye alimtenda John wakati anasoma chuo.
Marehemu alikuwa akienda vizuri katika tasnia ya filamu na ilisadikiwa angeweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. Kifo cha John kimeacha pigo kubwa Bongo Movies ambayo mpaka leo vilio vimetawala.
Mazishi ya msanii huyo yalikuwa yakimsubiri mama yake mzazi aishie London Uingereza.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Subscribe to:
Posts (Atom)