Saturday, January 26, 2013
Friday, January 25, 2013
St.Johns university walipoandamana
Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo na usiku wa kuamkia leo wanachuo walivamiwa vyumbani baada ya kukata nondo ya dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.
Kwa hali hii imesababisha maandamano ili kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John kilichopo Dodoma mjini.
TAARIFA KUHUSU DHAMANA YA MWIGIZAJI LULU AMBAYO ILIKUA ITOKE LEO.
Elizabeth Michael.
Jana kwenye Exclusive on millardayo.com kulikua na stori kwamba uwezekano wa mwigizaji Lulu kuachiwa kwa dhamana january 25 2013 ulikuepo.
Ni kweli ilikua iwe hivyo lakini kwa taarifa zilizotolewa kwa Millard Ayo ni kwamba dhamana hiyo imeshindikana kutolewa leo.
Sababu kubwa ni leo kuwa sikukuu hivyo shughuli imesogezwa mbele mpaka jumatatu january 28 2013.
Mwanzoni Lulu ambae anatuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia ilidaiwa alikua anatakiwa apate dhamana ambayo milioni 20 zilihitajika (kwa mujibu wa taarifa za ndani) ila ikashindika sababu jaji alipata udhuru.
Lulu amekua chini ya ulinzi toka kifo cha mwigizaji staa wa movie Tanzania Steven Kanumba April 2012.
Chanzo:Millard Ayo

Sitta: Nafaa kuwa Rais
“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” Akizungumza katika mahojiano (soma zaidi hapa)
maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri. Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

MISS UTALII VIPAJI KUFANYIKA TAREHE 27.01.2012
Tamasha kubwa la vipaji litafanyika katika Ukumbi wa Ikondolelo Lodge Hoteli ya Kitalii Kibamba Jumapili hii, ambapo warembo zaidi ya Thelasini wataingia katika kuonesha vipaji mbalimbali vikiwemo na, Kucheza ngoma, Kuimba, pamoja kuonesha mavazi mbalimbali ya Asilia.
Katika Tamasha hilo Maalum Mgeni Rasmi atakuwa Muheshimiwa Iddy Azan Zungu Mbunge wa Jimbo la kinondoni. Sambamba na Hayo Muheshimiwa Zungu atazindua tuzo Mbalimbali za Utalii Tanzania, kama Tuzo ya Mazingira, Tuzo ya Utamaduni, Tuzo ya Jinsia, wanawake na watoto, Tuzo ya Polisi Jamii, Tuzo ya Elimu ya Jamii, Tuzo ya Hifadhi ya Serengeti, Tuzo ya Mlima Kilimanjaro, Tuzo ya Michezo pamoja na Tuzo zengine mbalimbali.
Viingilio katika Tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo, V.I.P 20,000 , Watu wa kawaida 10,000 na watoto 5,000.
Tamasha litaanza kuanzia sa nane mchana na kuendelea.
Asante.
Fredy Tony Njeje
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano

JAPAN YAIPA TANZANIA BILIONI 28.2 KUBORESHA BARABARA NA KILIMO, MAKUTANO YA TAZARA KUWA NA BARABARA ZA JUU KWA JUU
SERIKALI ya Japan imepatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 28.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya uboreshaji wa usafiri jijini Dar es salaam na kilimo hapa nchini.
Msaada huo umesainiwa (leo) jijini Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada kwa niaba ya Japan na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Waziri wa Fedha Dkt . Mgimwa alisema kuwa mradi wa kwanza utahusisha upanuzi wa barabara ya Kilwa na ile ya Bandari ambapo jumla ya shilingi bilioni 20 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.
Aliongeza kuwa mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa barabara za juu(flyover) katika makutano ya TAZARA ambapo jumla ya shilingi bilioni moja (1) na milioni 26 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mradi huo.
Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa eneo lingine ambalo litanufaika na msaada kutoka Japan ni kuunga mkono sera ya Kilimo kwanza ambapo Tanzania imepata shilingi bilioni sita(6) na milioni 92 kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo kwa usalama wa chakula cha kutosha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa upande wa eneo hilo lengo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wa kipato cha chini wanaboresha kilimo ambacho kitawahakikisha uhakika wa chakula wakati wote na hivyo kuondokana na umaskini.
Kwa upande wa Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada alisema kuwa wananchi wengi wa Tanzania hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamekuwa wakisubiri kwa hamu barabara za juu ili kusaidia kupunguza msongamano wakati wa kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.
Alisema kuwa utakapo kamilika mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la msongamano na hivyo kupunguza saa za mwananchi kusafiri kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.
Balozi Okada alisema kuwa hatua hii itakuwa muhimu katika kukuza uchumi kwani wananchi watakuwa na muda wa kutosha kuzalisha mali kutoka na miundombinu kuruhusu magari kwenda kasi pasipo kikwazo.

Thursday, January 24, 2013
YANGA YADHIHIRISHA UBABE WAKE KWA BLACK LEOPARDS, YAIFUMUA 2-1 CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo

RAIS WA ZANZIBAR DK. MOHAMED SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA, ALFONSO LENHARDT IKULU MJINI ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed
Shein, akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso
Lenhardt, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhardt, alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake.

(Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar)

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA FIFA MJINI ZURICH SWITZERLAND
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, akiwa katika picha ya Pamoja na Rais wa
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter na Rais wa
Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga (kulia)
wakati Rais Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Makao Makuu ya FIFA
mjini Zurich, Switzerland jana Januari 23, 2013 kwa Mwaliko maalum wa
FIFA.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter wakiwa katika mazungumzo wakati Rais Kikwete na Ujumbe wake walipotembelea Makao Makuu ya FIFA mjini Zurich, Switzerland Januari 23, 2013 kwa Mwaliko maalum wa FIFA.
Rais wa FIFA Joseph Sepp Blatter akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete bendera maalum ya FIFA.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, akimweleza jambo Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Joseph Sepp Blatter (kulia) kuhusiana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodgar Chilla Tenga. Tenga pia ni Mwenyeketi wa Baraza la Vyama vya Soka vya Afrika Mashariki (CECAFA).

Wednesday, January 23, 2013
Hii kali Aliyekamatwa na pembe za ndovu ni askari wetu - JWTZ
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kwamba mwanajeshi aliyekamatwa juzi katika tukio la ujangili mkoani Arusha ni askari wake. Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe jana alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba MT 59509 Sajenti, Azizi Athuman Yusufu ambaye alisema ni askari wa jeshi hilo na alikuwa dereva wa mkufunzi wa kijeshi kutoka Zimbabwe anayefundisha hapa nchini.
Hata hivyo Kanali Mgawe alisema mkufunzi huyo wa kijeshi, hakuwapo wakati wa tukio hilo. “Kweli huyo ni askari wetu. Alikuwa anamwendesha mkufunzi wakijeshi kutoka Zimbabwe. Siku hiyo alimrudisha nyumbani kwake saa saba mchana na kwenda kupaki gari. Lakini baadaye saa moja usiku, alikwenda kulichukua gari hilo na kutokomea nalo kusikojulikana hadi alipokutwa katika tukio hilo,” alisema Kanali Mgawe.

Kamati ya rufaa TFF itatenda haki
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF YAAHIDI HAKI
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahidi wadau wa mchezo huo kuwa itafanya kazi zake kwa misingi ya haki.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa Kamati hiyo uliofanywa Dar es Salaam leo mchana (Januari 23 mwaka huu) na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kwa niaba ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, Mwenyekiti wa Kamati hiyo yenye wajumbe watano Idd Mtiginjola amesema wapo kwa ajili ya kutenda haki.
Mtiginjola amesema Kamati yao inaundwa na watu waadilifu, hivyo watafanya kazi kwa kuzingatia kanuni zilizopo na sheria nyingine za mpira wa miguu ikiwemo Katiba husika.

Chadema wamrarua Nape, Mwigulu kuhusu kauli zao
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu CCM kuhusu kauli zake za hivi karibuni kuwa Chadema itakufa.Akihutubia Mwanza hivi karibuni, Nape Nnauye alikaririwa akisema Chadema itakufa kutokana na laana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kwamba ni chama kilichojaa ubaguzi.
Akijibu kauli hiyo jana, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema chama hicho hakiwezi kulumbana na Nape.
Kigaila alisema Chadema haina makundi na haitakufa kwa laana ya Mwalimu Nyerere.
“Tunataka kuwaambia kuwa Chadema haina ubaguzi hivyo haiwezi kufa leo wala kesho mpaka iwe imetimiza kazi yake ya kuwakomboa Watanzania. Kama ni suala la Mwalimu Nyerere, laana hiyo iko ndani ya CCM yenyewe,” alisema.

Subscribe to:
Posts (Atom)