Tuesday, March 5, 2013

JOHN MNYIKA APANGA KUITISHA MAANDAMANO MAKUBWA MACHI 26

Mbunge wa Jimbo la Ubungo JOHN MNYIKA amesema Ofisi yake imepanga kuitisha Maandamano makubwa Machi 16 Mwaka huu kuelekea Ofisi za Wizara ya Maji, kutokana na Wizara hiyo kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la upatikanaji wa Majisafi pamoja na uondoaji wa Majitaka katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo.

Akizungumza na CLOUDS FM, MNYIKA amesema kuwa tayari Ofisi yake imekamilisha hatua za msingi za uratibu wa maandano hayo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Jeshi la Polisi pamoja na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.

Amebainisha kuwa licha ya ofisi yake kulifikisha suala la tatizo la Maji katika baadhi ya maeneo ya Jimbo hilo Wizarani sambamba na kuwasilisha hoja Binafsi bungeni, hakuna hatua zozote za awali zilizochukuliwa huku Wakazi wa maeneo hayo wakitaabika kwa kukosa maji.

"HAZIPITI SIKU MBILI BILA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI:.....MAMA KANUMBA

Mama yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.

Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.

“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.

Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.

Monday, March 4, 2013

KUTOKA BBC KUHUSU UCHAGUZI KENYA MARCH 4 2013


Hii picha ni kutoka Daily Nation Kenya, baadhi ya wakazi wa Nairobi waliojitokeza kupiga kura.

PAPA AWAAGA RASMI WAUMINI WA KANISA CATHOLIC

 -UTUMISHI wake umekoma rasmi 28th ,02 ,2013, aaga kwa mawingu mazito, jua lawaka ghafla

ILE historia ambayo haijawahi kuwepo kwa miaka 600 iliyopita ya papa kujiuzulu inafikia tamati Alhamisi 28th February 2013 ambapo Papa Benedict XVI ameachia rasmi uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.

Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Vatican, maelfu ya waumini wa madhehebu hayo walijitokeza kumuaga wakati alipowabariki katika ibada yake ya mwisho wa utumishi ambapo alisema ilikuwa Februari 28, 2013.

Wednesday, February 27, 2013

RIHANNA NA CHRIS BROWN WARIDHIA KUFUNGA NDOA JULY MWAKA HUU

Jarida maarufu (Star Magazine) limeripoti kwamba mastaa wa muziki Chris Brown na Rihanna wanampango wa kufunga ndoa mwishoni mwa July 2013 nyumbani kwa kina Rihanna huko Barbados.

Jarida hili limeendelea kutiririka kwamba kwenye ndoa hiyo wamepanga kusherehekea na watu mbalimbali wakiwemo wanaoamini kwamba Chris Brown amebadilika kitabia.

Ni harusi ambayo watu wote walioalikwa watakua wamesimama na wahudumu watakuepo kumfata kila mtu alipo, pia wale wachoraji wa tattoo watakuepo pia.

MAAJABU: KITANDA KIMOJA CHA HOSPITALI YA BUTIAMA HULAZA WATOTO WANNE....

HALI ya hospitali ya Butiama iliyopo wilayani Musoma mkoani hapa, iliyofunguliwa rasmi mwaka 1972 na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere imezidiwa na wagonjwa kutokana na kuachwa kama ilivyoziduliwa enzi za Mwalimu Nyerere. Tanzania Daima limebaini.

Hali hiyo imebainika jana baada ya jopo la waandishi wa habari za afya ya Mama, Baba na mtoto nchini kutembelea hospitali hiyo.

Waandishi hao walitembelea na kujionea hali halisi ya hospitali hiyo yakiwemo mawodi ya wagonjwa na vifaa vilivyopo ndai ya hospitali hiyo huku wakijionea mlundikano mkubwa wa wagonjwa.

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD

Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

CHOCOLATE ZAMPONZA WEMA SEPETU NA KUMFANYA APOTEZE "MENO"

 CEO wa Endless Fame Films Wema Sepetu amelazimika kujisamilisha kwa daktari wa meno baada ya ulaji wa chocolate kumponza na hivyo kuozesha baadhi ya meno yake.

Tuesday, February 26, 2013

Redio mbili zafungiwa kwa uchochezi

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

Na Thehabari.com

LOWASSA: CCM ITASHINDA 2015

 Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Moh Edward Lowassa amesema kuwa iwaposerikali zote mbili ile Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya visiwani, zitatekeleza  kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa CCM juu ya suala la ajira basi chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015

 WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Breaking News


Magazeti ya leo Jumanne ya 26th February 2013





LULU MICHAEL AJIPANGA KUJIENDELEZA KIMASOMO

BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha.

Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu  familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI: KAMA UMEGUSWA MCHANGIE MTOTO HUYU AWEZE KUTIBIWA

 Mtoto Ombeni Mbeula akiwa na mama yake Kilaudia Kigaila wakiwa hospitali kama umeguswa na hali ya mtoto huyu tafadhari tuma choche kwa njia ya M-Pesa 0757 498336 ili apata matibabu.