Monday, May 13, 2013

LADY JAYDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI

                                                        Judith Wambura 'Lady Jaydee'.

MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

Magazeti ya leo Jumatatu ya 13rd May 2013




MATOKEO MABOVU YA KIDATO CHA NNE YATACHELEWESHA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA

Matokeo ya mtihani wa kidato cha sita yaliyotarajiwa kutangazwa mwezi  huu yatachelewa  ili kutoa nafasi kwa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),  kurekebisha matokeo mabaya ya mitihani  kidato cha nne ya mwaka jana yaliyofutwa na serikali  mwezi huu.

Matokeo ya kidato cha sita ambayo huwa yanatangazwa mwanzoni  mwa mwezi Mei mpaka sasa hayajatolewa  na kwamba hayatatangazwa mpaka matokeo mapya ya kidato cha nne yatakaporekebishwa rasmi.

Alipoulizwa  juu ya suala hilo, Naibu Waziri   wa Elimu na  Mfunzo ya Ufundi  Philipo Mulugo alisema ingawa wakati huu ndio unaopaswa yatangazwe matokeo ya kidato cha sita haitafanyika hivyo hadi yatangazwe matokeo mapya ya kidato cha nne baada ya kufutwa.

TAARIFA MUHIMU KUHUSU AFYA YA MZEE SMALL

Kwa wote walioguswa na kuumwa kwa nguli wa sanaa za maigizo hapa nchini, Mzee Small, taarifa ni kuwa amepata nafuu na anatembea japo kwa fimbo ingawa mkono wake bado umelemaa.

Changamoto kubwa kwake ni dawa za kuchua, takribani 30,000/= kwa mwezi pamoja dawa za kusaidia kuyeyusha damu iligundulika kuganda kichwani mwake, takribani 50,000/= kwa mwezi pamoja na mengineyo madogo madogo, ANAWASHUKURU SANA WOTE MNAOGUSWA NA KUMJALI, Kwa msaada wowote tafadhali wasiliana na mkewe.

Angalizo; Bi Kidude aliteseka mno na hata nyumba aliyokuwa akiishi kwa muda mrefu ilikuwa pagale, na bila aibu alipofikwa na umauti, Rais wetu wa Serikali ya Mapinduzi aliongoza ujumbe wa Serikali na mengi mazuri yalisemwa juu ya nyota hii iliyoachwa ikaadhirika, NAULIZA TU HIVI MPAKA LINI?????????
By Matukio Chuma.

Saturday, May 11, 2013

NAIBU WAZIRI AINGILIA KATI UGOMVI WA LADY JAYDEE NA CLOUDS FM....RUGE AKIMBILIA MAHAKAMANI

IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari  Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba  na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’  Ruge ametoa ya moyoni.

Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.

“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize  pande zote mbili  hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”

ASKARI ALIYEMUUA MTOTO MDOGO WA RISASI AKAMATWA......CHADEMA WAANDAMANA, POLISI YAJIBU MAPIGO

ASKARI Polisi wa Kituo cha Tarime mkoani Mara mwenye namba D. 4662 Koplo Mathew, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kifo kwa risasi cha mwanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Rebu, Deus Jacob (9).

Kifo hicho kilitokea wakati polisi wakiwa kwenye harakati za kukamata mtuhumiwa, Marwa Bisara, mkazi wa kitongoji cha Songambele kata ya Sabasaba mjini hapa, aliyekuwa akituhumiwa kwa shambulio na kudhuru mwili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tarime/Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kitongoji cha Songambele, baada ya Koplo Mathew na askari wenzake wakiwa na mlalamikaji, wakifuatilia mtuhumiwa na kumkuta na wenzake katika pagala wakivuta bangi.

Wakati polisi wakijiandaa kumkamata, mtuhumiwa Bisara alimvamia Koplo Mathew akitaka kumnyang'anya bunduki na katika purukushani hiyo, risasi zilifyatuka na moja kumpata Deus kichwani na kumuua papo hapo baada ya kichwa kufumuka.

WIZARA YA ELIMU YATOA UFAFANUZI KUHUSU ZOEZI ZIMA LA KUYAPITIA UPYA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya   Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha  Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili  Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka   iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka  aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012.

PONDA AANZA UCHOCHEZI TENA....ANATAKA SERIKALI IANZE KUUA WAKRITO NA AMEDAI NECTA HUWAFELISHA WAISLAMU

Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho.

Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!

KAULI ZA SHEIKH PONDA.

Habari Zilizopo Magazetini leo Jumamosi 11st May 2013





Friday, May 10, 2013

LADY JAYDEE AFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI.....JOTO LIMEPANDA NA ANAMUOMBA MUNGU ASIKAMATWE MAY 31

Bado joto ya show ya mika 13 ya Lady JayDee inazidi kupanda kutokana na mengi yanayohofiwa kutokea siku hiyo.

Kwanza kulikuwa na tetesi kuwa huenda Clouds Fm wakafanya show nyingine siku hiyo, kitu ambacho Ruge Mutahaba alikifafanua vizuri kwa kusema mtu ukiwa na shughuli haimaanishi kuwa wengine wasifanye shughuli nyingine kama hiyo.

Lakini sasa kuna jingine ambalo limejitokeza, na amelisema mwenyewe Lady JayDee....

Kupitia akaunti yake ya Twitter Jide ameandika:

“Nimepata taarifa zisizo rasmi kuwa nimefunguliwa kesi mahakamani natumaini sitaitwa kizimbani tar 31 May ambayo ndio siku ya show.”

WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU KANISANI WAZIKWA KWA HUZUNI KUBWA

Misa ya Mazishi ya wahanga wa mlipuko wa bomu la Jumapili iliyopita kwenye parokia teule ya Olasiti ilianza katika eneo lile lile mlipuko ulipotokea.

Misa  hiyo  iliongozwa na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Maandamano yalianzia toka chumba cha kuhifadhia maiti, miili ikapelekwa makao makuu ya Asofu Mkuu, Burka  na  baadaye  ikawasilishwa kanisani .....

Mahubiri ya Kardinali Pengo
Ndugu zangu,

Nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo.

Mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema. Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Magazeti ya leo Ijumaa Ya 10th May 2013




HAYA NDO MAJINA 9 YA WATUHUMIWA WALIOLIPUA BOMU KANISANI ARUSHA

Imeripotiwa kuwa jumla ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Ripota wa WAPO FM radio alisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-

    1- Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    2- Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    3- George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)
   4-  Mohammed Suleiman Said (38, mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, aliyewafuata kwa gari binafsi washukiwa wa ugaidi kutoka kiwanja cha ndege na kuwepeleka hadi hoteli ya Aquiline iliyopo Arusha)
   5-  Said Abdallah Said (28, mkazi wa Abu Dhabi, Nchi za Falme za Kiarabu)
   6-  Abdelaziz Mubarak (30, Nchi za Falme za Kiarabu)
   7-  Jassini Mbaraka (29 mkazi wa Bondeni, Arusha)
   8-  Foud Ahmad (28, Nchi za Falme za Kiarabu)
   9-  Said Mohsen (Najran, Saudi Arabia)

Hata  hivyo, himaya ya Imarati, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE - United Arab Emirates)  inasema maafisa wake wamekanusha kuhusu raia wake watatu kuhusika na mlipuko wa bomu la Olasiti, Arusha.

Abu Dhabi ni mji mkuu wa Imarati (UAE), ambazo zina imirati saba -- Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Fujairah, Ras al Kaimah, Ajman na Umm a Quwain. Nchi jirani na UAE ni Qatar, Saudi Arabia na Oman.

Mapya bomu la Arusha:Majeruhi aeleza bomu lilivyokuwa

Bomu lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa lilitengenezwa kienyeji.

Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.

Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.

Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.

R.I.P ALL

Hali tulivu,baridi kiasi, majonzi yakiwa yametawala kila kona jijini arusha Tukiwasindikiza wapendwe wetu waliotangulia mbele ya haki siku ya jumapili 5/5/2013 katika mlipuko wa bomu kanisa la mtakatifu joseph olasiti.Hii ni chachu kwa wakristo wote Tanzania na dunia, sali kila sekunde uliyonayo kuombea AMANI nchi yetu.Mungu uwaangazie mwanga wa milele wapumzike kwa Amani Amina.